Vita ya Chalamila dhidi ya madanguro Dar ina viashiria vya ubaguzi

Vita ya Chalamila dhidi ya madanguro Dar ina viashiria vya ubaguzi

Kwa kuwa wengi wetu tukienda baa huwq tunataka wake zetu au michepuko yetu ijipigilie vimini na nguo matata, na polisi wanashindwa kutofautisha kimavazi wake zetu na vingasti, na wale wauzaji, namshauri Chalamila atoe tangazo la serikali wanawake wote wa Dsm waende wamevaa madela au vitenge kwenye mabaa na kumbi za starehe.

Hii itawaondolea ugumu Polisi wetu kwa kuwa Sasa wakiona nguo fupi kwa mwanamke aliye baa, wanamkamata
Wewe unavyoona Mama yako angevaa dera Chiembe angepatikana kweli?..[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Labda kama walitumia wale askari kidole. Ila tofauti na hivyo waliwakosea sana .. halaf hiyo ni kazi ya kijinga sana..
 
Maelekezo yake yamepelekea mauaji.
Nakataa.Polisi anapopewa mafunzo anaeleweshwa kutumia akili zaidi ya chochote.Nguvu/silaha ya moto ni jambo la mwisho kufanya na ikibidi awe anajilinda.Sasa askari mpumbavu na mlevi ambaye ameagizwa kukamata "nyonyoo zinazojiuza" baa ambapo hakukuwepo na tishio,ametumia bunduki halafu lawama ziende kwa mwingine?Hapana.Chalamila alikuwepo hapo kwenye hiyo baa na akamuamuru kwa kumtisha huyo askari aue?Ni upumbavu mtupu wa askari mvuta tutu/bangi.
 
Lakini kahaba ana effect gani? Biashara kongwe hiyo hawezi icontrol ndio maana saiv anahangaika na wavaa vimini
Madhara hasi ya kahaba ni kweli hauyajui mkuu?Unatania.Kuhusu kuimudu na kuuondosha hiyo biashara haramu,hapo mimi sina jibu.Nilijikita kuhusu wale askari wapumbavu na wauaji wa raia ambaye hakuwa amewatishia hata kijinga cha moto. Askari wameua kwa sonona na ushamba wa kutojimudu kwa ulevi kwenye kutumia silaha ya moto na shida zao zinazowasumbua kwenye kota zao.
 
Nakataa.Polisi anapopewa mafunzo anaeleweshwa kutumia akili zaidi ya chochote.Nguvu/silaha ya moto ni jambo la mwisho kufanya na ikibidi awe anajilinda.Sasa askari mpumbavu na mlevi ambaye ameagizwa kukamata "nyonyoo zinazojiuza" baa ambapo hakukuwepo na tishio,ametumia bunduki halafu lawama ziende kwa mwingine?Hapana.Chalamila alikuwepo hapo kwenye hiyo baa na akamuamuru kwa kumtisha huyo askari aue?Ni upumbavu mtupu wa askari mvuta tutu/bangi.
Kwa kuanzia Polisi hata hawatakiwi kutumwa kwenda kukamata wanaojiuza au waliovaa nguo fupi popote, sio tu bar.
 
Unatakiwa ujiajiri bila kukinzana na sheria za nchi.Ukahaba si ajira halali.
Ukahaba ni suala la kushughulikiwa na makanisa na misikiti, halipaswi kuwa jambo la msing kwa serikali kulifuatilia. Nchi hii ni tofatuti sana na Iran, Saudia, Afghanistan n.k
 
Ukahaba ni suala la kushughulikiwa na makanisa na misikiti, halipaswi kuwa jambo la msing kwa serikali kulifuatilia. Nchi hii ni tofatuti sana na Iran, Saudia, Afghanistan n.k
Kwa Sasa,mimi najikita kwenye mauaji ya askari.Ukahaba unahitaji kipengere chake.
 
Kwa kuanzia Polisi hata hawatakiwi kutumwa kwenda kukamata wanaojiuza au waliovaa nguo fupi popote, sio tu bar.
Swali la kujiuliza:Je,ni kweli waliagizwa kuwakamata waliovaa nguo fupi(wanawake tu)au walijianzishia mradi wao kivyao?Nguo fupi tu/mini skirts?
 
Sasa si ndiyo yeye aliyewatuma hao polisi kupitia matamko yake ya kupambana na kitu asichokijua !! Anakwepa vipi lawama?
Yawezekana aliwaagiza(mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa)kuwakamata makahaba.Ni kweli kwamba aliwaagiza wawatwange risasi pia?Aliwasimamia na kuwashurutisha?Kulikuwa na uvunjifu wa amani uliotishia uhai wa hao askari?Je,hawakudhamiria kutenda uhalifu,kwa sababu walionekana wakiwa wamelewa/intoxicated?Na kitendo cha kuindea silaha ya moto kwenye gari alimaanisha nini kama si nia yake ovu ya kutaka kuua huyo askari?Askari muuaji amedhihirisha ukosefu wa matumizi mema ya akili,nguvu na weledi.Hawakutumwa kuua.
 
Ukahaba mkoani Dar es Salaam na nchi hii kwa ujumla unafanyika kila mahali, sio katika madanguro ya Mwananyamala tu. Ukahaba unafanyika katika Lodges, Hoteli kubwa, maofisini kwa watu, katika magari na hadi nyumbani kwa watu.

Kwanini vita vya ukahaba hapa Dar vimelenga madanguro tu ya aina ya Mwananyamala ambayo yanaonekana ni ya masikini hoehahe wa kipato badala haya maeneo yote kwa ujumla?

Usawa katika kudhibiti ukahaba ulipasawa kujumuisha kutaka nyumba zote za kulala wageni hata hotel kubwa zisiruhusu mwanaume na mwanamke wasio na cheti cha ndoa kulala chumba kimoja, kupiga marufuku wanaume kuhonga katika mapenzi au kutoa pesa kwa wanawake wasio wake wa ndoa baada ya kufanya mapenzi.
Uko sahihi lakini haitawezekana kwa sababu bado idadi ya Wanawake ni kubwa kuliko Wanaume hivyo kuingia guest na Cheti cha ndoa ni ukiritimba.Maisha binafsi ya mtu hayaongozwi na serikali bali roho na moyo wa mhusika akiwa na akili timamu na sababu zake za msingi.Kila siku tunalalamikia hilo jambo ambalo yeyote mwenye akili timamu na upeo wa kimungu anaogopa kwa sababu ni dhambi.Ila kuna wanaume wanaweza kaa hata mwezi bila ya tendo la ndoa kwa sababu wenzi au wake zao ni makaidi au wababe,suluhisho mtu anatafuta pa kujifariji na hao madada poa wamekua ni faraja kwa baadhi ya watu na maisha yanasonga.
 
Nadhani angeanza kukamata wateja wa madanguro. Akikamata sita tu atakua ametia kitumbua mchanga.
Mimi napinga hilo wazo kwa sababu kukamata wateja ni kuwaonea.Suluhisho hao madada wawekewe kodi kubwa ambazo zitawafanya kupandisha viwango kwa wateja wao na hivyo kuua hiyo biashara haramu bila kutumia nguvu.Atakayeshindwa kulipa kodi afungwe miezi sita ili akasaidie taifa katika uzalishaji na akishatoka itakua fundisho kwa wengine.
 
Back
Top Bottom