Vita ya kibiashara ya Marekani yawezesha uwazi na biashara kati ya China na kanda ya magharibi

Vita ya kibiashara ya Marekani yawezesha uwazi na biashara kati ya China na kanda ya magharibi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1723161571576.png

Biashara ya nje ya China imeendelea kukua licha ya vitendo vya nchi za Magharibi vya kujilinda kibiashara, hususan vita ya kibiashara ya China iliyoanzishwa na Marekani. Kuna mambo kadhaa ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa biashara hiyo. Chini ya shinikizo la Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi, China inatafuta uhusiano wa kibiashara na ushirikiano na kanda ya magharibi chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kupitia maendeleo ya viwanda katika nchi za kanda ya magharibi, ili kuufanya mfumo wa biashara ya nje ya China kuwa na maana zaidi.

Biashara ya nje inayofanywa na China katika kanda hiyo, ambayo inahusisha mikoa 12 na manispaa moja, ilifikia dola za kimarekani bilioni 270 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho, na kuifanya kuwa kabda yenye ukuaji wa kasi zaidi katika biashara ya nje ya China.

Ukuaji huu wa kidhahiri katika shughuli za kibiashara katika sehemu ya magharibi ya China unaonyesha mfano wa mkakati wa nchi hiyo wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na kuongezeka kwa vitendo vya kujilinda kibiashara katika mazingira ya biashara ya kimataifa. Ukomo unaotokana na mfumo wa kawaida wa biashara ya kigeni unaonyesha haja ya China kutumia vizuri utaratibu wake wa biashara na kutafuta fursa za masoko mapya.

Zamani, eneo la pwani ya mashariki ya China lilikuwa maarufu sana kwa biashara ya nje ya nchi hii, lakini sasa eneo la magharivi linashuhudia ongezeko la biashara ya nje, na kuashiria kuhama kwa mwelekeo wa biashara ya nje ya China kuelekea kupunguza pengo la maendeleo ya kikanda. Ukuaji wa biashara ya nje katika eneo la magharibi linanufaika na kuboreshwa kwa sera ya serikali ya China kuhusu kanda ya magharibi, huku pia ikionyesha fursa ya maendeleo na uhai wa soko katika kanda hiyo. Hali hii ni sehemu muhimu ya kuhakikisha biashara ya nje ya China inadumu kuwa imara na nyumbufu kwa muda mrefu.

Maendeleo ya mtandao wa usafiri, hususan kutambulishwa kwa treni za mizigo kati ya China na Ulaya na Ushoroba Mpya wa Biashara ya Kimataifa ya Baharini na Ardhini, vimeboresha kiuhalisia ufanisi wa ugavi katika kanda ya magharibi, kupunguza gharama za biashara, na kuimarisha uhusiano na soko la kimataifa. Treni ya mizigo ya China na Ulaya kwa sasa inatoa huduma kwa miji 110 kati ya Ulaya na Asia, huku Ushoroba Mpya wa Biashara ya Kimataifa ya Baharini na Ardhini ukiunganisha bandari 490 katika nchi na sehemu 120. Miradi hii ya uchukuzi ambayo inachukuliwa kama moyo wa uchumi, imeiunganisha kanda ya magharibi mwa China kudumu kuwa na uhai. Ukuaji wa biashara ya nje katika kanda ya magharibi mwa China pia unachochewa na nafasi muhimu ya kanda hiyo katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja. Ikitumia nafasi yake ya kipekee ya kijiografia na hazina kubwa ya rasilimali, kanda ya magharibi imejitokeza kama mlango muhimu unaounganisha bara la Ulaya na Asia na kuvutia kampuni mbalimbali kujihusisha na biashara ya kimataifa kupitia kanda hiyo.

Kwa kujihusisha na masoko mapya na sehemu zilizo kando ya njia ya BRI, kanda ya magharibi ya nchini China inaweza kukabiliana na changamoto kutoka masoko ya Magharibi licha ya kuongezeka kwa vitendo vya kujilinda kibiashara na kuimarisha unyumbufu wake dhidi ya hatari zinazoweza kutokea.

Kwa hiyo, ili kuboresha zaidi maendeleo ya biashara ya nje katika kanda ya mashariki, ni muhimi kutekeleza hatua zaidi zenye malengo kama vile kuharakisha mambo ya kisasa na kukarabati sekta ya viwanda, na pia kuunga mkono zaidi na kutoa mwongozo kwa biashara za huko ili kuwezesha ushindani wao wa kibiashara duniani.
 
Back
Top Bottom