Vita ya Kiuchumi: Ningekuwa Rais wa Tanzania ningeanzisha ujenzi wa reli ya SGR kutokea Bandari ya Tanga hadi Kagera, Rwanda na Uganda

Vita ya Kiuchumi: Ningekuwa Rais wa Tanzania ningeanzisha ujenzi wa reli ya SGR kutokea Bandari ya Tanga hadi Kagera, Rwanda na Uganda

Uganda cargo zao nyingi zinapitia Mbombasa. Na Uganda anafanya mapinduzi makubwa sana ya Viwanda.

Pia South Sudan still ni potential kibiashara maana anahutaji sana bidhaa kwa ajili ya kuijenga nchi yake. Wao ni landlocked na wanategemea sana Kenya na Uganda.

Congo upande wa mpaka wake na Uganda pako active zaidi kuliko upande wa border yake na Rwanda pamoja na Burundi hivyo kuna faida zaidi kuingia Congo kupitia Border yake na Uganda.

Bidhaa nyingi zinazoenda Congo kupitia Tanzania zinapitia njia ya Tunduma then Zambia ambapo pia TAZARA inaboreshwa.

It's a matter of time but the future is promising. Tunahitaji tu kufanya maamuzi magumu
unajua boss, hadi leo huwa natafuta surveyor aliyepewa kazi ya kuchora ramani ya africa aliipendelea sana tanzania, ukiondoa africa ya kusini tanzania ndio yenye ukanda wa bahari mrefu sana africa, ndio yenye bandari zaidi ya moja, Tanzania imepakana na malawi zambia congo burundi rwanda uganda, pia ipo karibu kilogistic na zimbambwe sudan ya kusini Northen mozambique, congo brazaville

Tungeliweza kutumia geografia yetu vizuri tusingekuwa tunalima wananchi wangepewa cupon kila ijumaa wanaenda supermarket kupata mahitaji, hakuna mwananchi angehangaika kujenga nyumba, vijana akibalehe tu anapewa nyumba gari na mke kwa gharama za serikali, vijana wangefanyaka,i ya jeshi ya kuchunga nchi yetu, hizi za manamba wangefanya wapakistani wahindi na wajaluo
 
Mwisho haya yote yatazishawishi zaidi nchi za Uganda na Rwanda na baadae Sudan Kusini kupitisha mizigo yao Tanzania endapo tukianza sasa kujenga kipande cha SGR kutoka Bandari ya Tanga kuelekea Tabora-Geita- Kagera - Rwanda- Uganda ambapo ni rahisi kwa usafirishaji wa mizigo kuelekea na kutoka nchi za Asia na Australia kuliko ilivyo kwa Bandari ya Mombasa na hata Lamu
'Actually', nilipo bandika maoni yangu ya mwanzo nilikuwa sijasoma mada yote ilivyo wasilishwa.
Hii ni mada 'sustandard'; ni kama imeletwa na mtu asiyejuwa mambo mengi ya miunganiko ya miundo mbinu.
Kwa mfano: utapeleka vipi SGR toka Tanga iende "Tabora, Geita, Kagera, halafu ndiyo uende Rwanda?
 
kabisa, na mizigo hii ya zambia drc south africa wanainyemelea na angola nao wanaitizama kwa hamu, hivyo tukifocus kwenye hizi nchi ni more important kuliko uganda na rwanda ambavyo hamna chochote porojo tu
Hata gari nyingi za IT zinazotoka bandarini nyingi zinaenda Congo DR kupitia boda ya Zambia Congo, Kasumbalesa. Reli ya kisasa ikienda Zambia inaunganisha na Congo. Zambia wana madini ya copper, hivyo treni ikienda kule inarudi na mzigo wa madini kupekeka bandarini.
 
Ni mawazo mazuri ila watakuambia hakuna hela,, kikubwa ujumbe umefika mkuu 💪🏽💪🏽
 
Amani iwe nanyi wanabodi!

Kupitia Northen Corridor Kenya anataka kuingia DRC, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini kwa Reli ya SGR.

Sisi Tanzania tunajenga SGR yetu kuingia Burundi na baadae Congo.

Kwa hesabu za haraka huko mbeleni SGR ya Kenya ndo itakayoleta faida zaidi kwa Kenya kuliko SGR yetu maana wao wataingia Congo pia tunapotaka kuingia sisi huku wakiingia Rwanda, Uganda na Sudan Kusini.

Kijiografia ni gharama ndogo sana kuingiza SGR Rwanda kutokea Tanzania compared na gharama zitakazotumika kuiingiza SGR Rwanda kutokea Kenya kupitia Uganda ambapo mpaka sasa ujenzi haujaanza.

Pia ni faida na rahisi zaidi kwa Rwanda kufanya biashara kupitia Tanzania endapo watatumia SGR yetu hasa pale tutakapoweza kuifikisha Rwanda.

Sio hivyo tu, ni rahisi kwetu zaidi kuipeleka SGR Kagera alafu ikaingia Uganda jambo ambalo linaweza kuishawishi zaidi Sudan Kusini kutumia SGR hii na kupitisha mizigo yake Tanzania

Mwisho haya yote yatazishawishi zaidi nchi za Uganda na Rwanda na baadae Sudan Kusini kupitisha mizigo yao Tanzania endapo tukianza sasa kujenga kipande cha SGR kutoka Bandari ya Tanga kuelekea Tabora-Geita- Kagera - Rwanda- Uganda ambapo ni rahisi kwa usafirishaji wa mizigo kuelekea na kutoka nchi za Asia na Australia kuliko ilivyo kwa Bandari ya Mombasa na hata Lamu.

Soma Pia:
Kwa Dunia ilipofika sasa hasa kiushindani katika kupata maendeleo ya kiuchumi ni lazima Tanzania ichukue hizi Drastic measures haraka sana ili kujihakikishia nafasi ya juu kiuchumi miaka mingi ijayo na kama the logistic hub for East and Central Africa.

Rais Samia
Rais wangu kipenzi. Itisha kikao cha Baraza la Mawaziri, ridhieni na anzisheni mambo yafuatayo;

1. Ujenzi wa kipande cha SGR kutoka Bandari ya Tanga kueleka Kagera- Rwanda na Uganda

2. Kuanzisha haraka mradi wa kupanua zaidi Bandari ya Tanga

3. Kuanza kuwashirikisha Rwanda, Uganda na Sudan Kusini mpango huu haraka sana.


Duniani hapa principle kuu ya maendeleo ni Ubaya Ubwela. Maximise your potentials mje kukumbukwa na vizazi vyote vya Tanzania hadi mwisho wa dunia kwa kufanya maamuzi ya maana yenye faida kwa nchi hii.

Lord denning Dar es Salaam!

Pesa ungelizipata wapi
 
Mbona sgr hii ya sasa( Dar-Mwanza ) ita ingia hadi Rwanda?
Sema ikitoka Rwand ndo inaingia UG ila ni muhimu tuwe na connection pia ya UG bila kutumia nchi nyingne au ziwa.!
 
Back
Top Bottom