Kwa taarifa yako mkuu, ushindi wa vita hautokani tu na wingi wa jeshi, au ubora wa vifaa, bali ushujaa na uzalendo wa wapiganaji. Taswira iliopo sasa ninyi ndio mnawachokonoa Warwanda, vikazuka vita, wale watapigana sana kiuzalendo na hadi wa mwisho na mtaumia sana. Jeshi lao linaogopwa hadi hata na mijitu ya Congo. Hata Waganda na Museveni hawawezi jimudu. Kama alivyozingua Hitler kwenye vita vya pili vya dunia, jeshi lake lilipigana sana kiuzalendo tofauti na vifaa.
Ikumbukwe kuwa JWTZ hawajapigana vita wenyewe kama jeshi, historia ya Kagera inatueleza jinsi Watanzania walitoka wote kwenda kupigana, yaani JWTZ, Polisi vitengo vyote, wanamgambo, wanavijiji, hata waasi wa Kiganda wengi maana vita vilikua vyao. Na iliwagharimu Wabongo sana kiuchumi hadi panya vijijini walijua njaa ni nini, hadi Museveni amewalipa tu hivi majuzi. Kipindi kile Watanzania walikua wazalendo chini ya mwalimu Nyerere na ilikua rahisi kuwahusisha kwenye vita. Tofauti na leo wametajika kwenye ufisadi wa kila aina ikiwemo akaunti za banki Uswizi, mateja na wanyama mbugani, wapo kimaslahi zaidi. Raia wa aina hiyo huwezi shinda vita vyovyote nao.
Juzi pia JWTZ wamejihusisha kwenye vita na watoto wa M23. Ieleweke pia hapa hawakupigana vita wenyewe, Congo ilihusika pakubwa maana vita vilikua vyao pia, Afrika Kusini na Wamalawi hawakuchelewa kuhusika. Rwanda nayo ikapigwa mkwara na Umoja wa Mataifa hadi haikuwasaidia hao vijana. Na zaidi, M23 waliwahusisha watoto tokea vijijini vitani na kwa lazima.
Kwa ushauri wangu, na uendelevu wa nchi yenu kiuchumi, wacheni hizi chokochoko zenu dhidi ya Warwanda maana mtaumia sana. Pia kuna kipindi niliskia fununu kuwa wapo raia wenye asili za Kirwanda kwenye nyanja nyingi serikalini mwenu, na ikatokea kuzuka sijui vipi uzalendo wao watauelekeza wapi. Kagame ni mjanja sana na naskia aliwahi ishi Tanzania na hata kusomea kijeshi huko, hivyo anawajua sana ninyi zaidi ya mnavyojifahamu.