Vita ya Urusi na Ukraine: Akili na malengo ya Putin nchini Ukraine


Hii mkono mfu inakuaje? Akipigwa Nuke tokea Baltic na nyambiz ikasogea hii system inarudishaje shambulizi?
 
Unachosema ni kweli kuwa Ukraine wanapambania uhuru wao na pia ni kweli Urusi wanapambania usalama wa taifa lao katika hali hii kitakachoamua ni mkono wa chuma, ni lazima mmoja ashinde kwa nafasi ya mwingine.
 
Mkuu huko nyuma tangu kuvunjika kwa USSR na kuzaliwa Urusi uchumi haukuwa mzuri na pia hali ya kisiasa ya ndani haikuwa njema. Moja ya hatua za mwanzo kabisa alizochukua Yeltsin na Putin kwa nafasi zao zilikua ni kurekebisha uchumi wa Urusi maana bidhaa muhimu zilikua haba huku bei ikiwa juu sana na wafanyakazi walikua hawalipwi kwa wakati wakati mwingine hawalipwi kabisa, kulifanya jeshi liwe la kisasa maana muundo wa jeshi lao ulikua ni wa kizamani, na kuleta umoja wa kitaifa sababu kulikua na vurugu za ndani kama vugu vugu la chechenya lilozua vita miaka ya 1999-2000. Haya yote yaliitia ugumu Urusi kusimamia kwa nguvu madai yao ya kutotaka majirani zake kujiunga NATO.
Mbali na hayo walijitahidi kukemea hatua za NATO kwa mdomo tu maana hawakua na ubavu wa kubishana nao.
 
Hii mkono mfu inakuaje? Akipigwa Nuke tokea Baltic na nyambiz ikasogea hii system inarudishaje shambulizi?
Huu mfumo upo complicated kuliko nilivyoueleza. Lakini una uwezo wa kutambua eneo shambulio lilipotoka hata kama nyambizi ndio imetuma pigo hilo basi majibu yatarudi kutoka kwenye coordinate zile pigo lilipotoka. Kwenye muktadha huo nchi za Baltic zitawajibika.

Ubaya wa silaha hizi ni kwamba ukiwa nazo tayari inakuwa rahisi kushambuliwa.
 
Uchambuzi mzuri sana, ila umesahau kuelezea mkataba urusi walioingia na ukraine kwamba asijiunge na nato,yeye baada ya kupelekwa gesti juzi kati na mbwa mkubwa (U.S.A) akatumia akili ya chini akajisahau ndio matokeo yake haya na mbwa mkubwa karudi kwa mkewe...
 
Mchambuzi uko bright Sana......

But kila mtu anayechambua lazima mizani iegemee kwa RUSSIA.....inawezekana Hawa jamaa ni hatari
 
Umechambua vizuri ila hapo kwa Israeli kwa Palestine sio kweli. Pale ni survive of the fittest . Hawa jamaa kihistoria anaeshinda vita ndio mwenye nchi. Cku wapalestine wakishinda vita Israeli inapotea outomaticaly. Na hii ni kwasababu wote ni wenyeji hapo.
 
Mkuu, umechambua "briefly" lakini moja kwa moja kwenye hoja zako tatu ziloshiba.

Ila kama nilivyosema hii itabadili kabisa "New World Order" ambayo hata nchi za magharibi ndivyo zinavyodai kwamba ndio malengo halisi ya Putin.
 
Nafikiri
sote tunazungumzia kitu kimoja ila maneno tofauti tu mkuu.
Maslahi ndio yanayowasukuma wote hasa ya kiusalama.
 
Naam ni kweli kabisa mkuu, kuna mataifa yamechoshwa na mpangilio wa sasa wa Dunia ulianzishwa na kuratibiwa na Marekani. China ikiwa miongoni mwao.
Mkuu, umechambua "briefly" lakini moja kwa moja kwenye hoja zako tatu ziloshiba.

Ila kama nilivyosema hii itabadili kabisa "New World Order" ambayo hata nchi za magharibu ndivyo zinavyodai kwamba ndio malengo halisi ya Putin.
 
Mkuu, kama hutajali tueleze kidogo kuhusu huu mkataba
 
Mchambuzi uko bright Sana......

But kila mtu anayechambua lazima mizani iegemee kwa RUSSIA.....inawezekana Hawa jamaa ni hatari
Ni hatari sana sababu ndiyo wanaoongoza kwa kumiliki makombora mengi zaidi ya Nyuklia.
 
Kutoka Latvia mpaka Moscow ni umbali wa 954Km wakati kutoka Kyiv-Ukraine Hadi Moscow ni 865Km. Latvia ni Mwanachama wa NATO na Kuna Kambi ya Jeshi la Marekani pale,Latvia pia imepakana na Urusi. Kwahiyo sioni Kama sababu yako ya Urusi kukaa kimya wakati Latvia akijiunga NATO na Kuvamia Ukraine baada ya kuona inataka kujiunga NATO wakati Latvia na Ukraine zote zinapakana na Urusi Directly Haina mashiko. Njoo na sababu nyingine labda.
 
Unataka kusema tangu hiyo miaka hakuna nchi ambazo zilijiunga na NATO? Nchi Kama NORTH MACEDONIA imejiunga na NATO mwaka juzi tu 2020.
 
Nimekuelewa vyema mkuu
 
Unataka kusema tangu hiyo miaka hakuna nchi ambazo zilijiunga na NATO? Nchi Kama NORTH MACEDONIA imejiunga na NATO mwaka juzi tu 2020.
Hakuna mahali nimesema hakuna nchi ambazo zilijiunga NATO mkuu.
Kuweka rekodi sawa mwaka 1999 Poland, Hungary na Czech zilijiunga, zikafuata za Ulaya ya kati Slovakia, Slovenia, Bulgaria, Na zile za Baltic Estonia, Latvia na Lithuania. Shughuli haikuishia hapo 2009 Albania na Croatia wakajiunga. 2017 mambo yakaendelea Montenegro wakajiunga.
North Macedonia kama ulivyoainisha yenyewe ni ya 2020.

Nilichokua nasema ni kwamba hawa wote wamejiunga japo Urusi haikutaka hilo
Litokee hivyo waliishia kukemea kwa mdomo tu maana hawakua na namna ya kuzuia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…