Ngoja nikuulize, hii hofu ya Nato kwa Russia inatoka wapi? Je Nato amewahi kusema kwamba siku moja anataka aichukue Russia halafu ili iweje.
Ebu angalia mataifa mawili wanachama wa Nato kama Estonia na Latvia je hawajapakana na Russia? Kwa nini basi Russia haijawavamia kama walivyoivamia Ukraine ambayo bado hata haijawa mwanachama.?
Huyu Russia yeye nani kampa haki au uhalali wa kuyaamulia mataifa mengine mambo yao?
Mkuu naomba niingilie swali hili.
Huhitaji kumsikia bwana Stoltenberg akisema kesho wanaivamia Urusi kuelewa Urusi iko hatarini ikiiacha NATO kuwajumuisha majirani zake ndani ya umoja wao. Suala la Jirani kuwa mwanachama wa umoja wa hasimu ni dalili tosha kuwa chochote kinawezekana. NATO wanatoa hakikisho kwa wanachama wake wote kuwa mmoja akishambuliwa ni sawa wameshambuliwa wote. Hii inatosha kuelewa kuwa Urusi akiruhusu kuwa na majirani wenye fikra hizi basi ‘any miscalculation’ yaweza fasiriwa kuwa ‘an act of aggression’ inaeleweka kuwa ‘to avoid war you need buffer zone between great powers’
Hizo nchi za ulizozitaja ni kweli zinapakana kabisa na Urusi, na Warusi si wajinga kuziacha. Waliziacha kwa sababu kuu mbili
1) Zilijiunga NATO wakati Urusi wana hali mbaya kiuchumi, hawakuwa na namna yoyote ya kuzuia.
2) Warusi wanajua ni vinchi vidogo vitagharimu muda mfupi tu kuvituliza wakati wa vita dhidi ya NATO (mungu atuepushe).
Kivipi?
Kimkakati nchi za Baltic zimejitenga na nchi nyingine za NATO na si rahisi NATO kuzilinda vita ikizuka. Japo ukitazama ramani utaona nchi wanachama wa NATO za Poland na Lithuania zinapakana lakini mpaka ule wanamikakati wanauita
‘sulwaki gap’ ( tangu miaka ya 2000 wameandika sana kuhusu hili gap) Wamagharibi wenyewe wanafahamu wazi kuwa Urusi wana
Advantage kijiografia hivyo wenyewe wanatazamia kuwa eneo dhaifu kabisa kwao ni ‘gepu la sulwaki’. Kwakuwa Urusi wana hii
advantage punde watakapodhibiti
gap hili basi nchi za Baltic zitabaki bila usaidizi na itakua rahisi kuzitwaa. Ndio maana unaona Urusi hawashughuliki nao.
Hii ni tofauti kwa Ukraine, ile ni nchi kubwa kijiografia kuiacha ikaliwe na hasimu ni kosa kubwa sana, tujaalie Ukraine imekuwa NATO na vita ikazuka baina ya NATO na Urusi, kwa silaha zilizopo sasa Putin anakadiria itachukua dakika 7 tu kwa kombora toka Ukraine kupiga Moscow. Jambo ambalo halikubaliki vichwani mwa watunga sera wa Moscow.
Ama kwenye swali lako “Huyu Russia yeye nani kampa haki au uhalali wa kuyaamulia mataifa mengine mambo yao?”
Kiufupi kabisa ktk kujibu swali hili lazima tukubali ukweli kuwa siasa za kimataifa zimegubikwa na dhana survival of the fittest.
Ni ngumu kuelewa ikiwa mmoja anatazama mambo juu juu, ni rahisi sana kuelewa ikiwa mmoja atarudi kwenye maana ya msingi kutafuta maana ya ‘uhalali’ na nani aliibua hii dhana ya ‘uhalali’ kama tunavyoiona hii leo, ukioata majibu hapo utaelewa kuwa hizi ni dhana tu hazina nguvu kubwa kama tunavyozipa vichwani mwetu pia utakuja kuona haya mambo hayaamuliwi kihisia au kimaadili kama wengi tungependa mambo yawe, haya mambo hayaendi kwa ‘imaginations’ tulizonazo vichwani za usawa na haki na kuheshimiana.... kwa nchi yoyote lile kipaumbele nambari moja ni usalama wa nchi, kipaumbele hiki kitatimizwa bila kujali chochote kile. Kwenye huu mzozo Urusi anaihisi hatari kwa usalama wake kama nchi ndio maana kwa miaka zaidi ya 20 wamekuwa wakibembeleza NATO wasifanye hivi vitu lakini haikutosha, sasa wamechukua hatua ngumu kuhakikisha wanayotaka yanakuwa nani wa kuwalaumu? Ndio wanaharibu ‘haki’ za nchi nyingine lakini ndio uhalisia wa siasa za kimataifa ili ku-survive ni lazima uwe na jeshi imara kujilinda kinachowakuta Ukraine ni kushindwa kwao kutetea maslahi ya nchi yao na naweza sema bila kupepesa macho huo ndio mwisho wa nchi yoyote itakayoshindwa kujilinda.