Vita ya Urusi na Ukraine: Akili na malengo ya Putin nchini Ukraine

Siasa ya dunia haipo hivo, hakuna mtu yupo huru katika kila jambo, ukitaka kufahamu hilo angalia hata hapa bongo Zanzibar mambo yao mengi yanaamuliwa na sera za bara ingawa inajiona ni nchi kamili na hawaishi kulalamika kila siku.
Leo kuna nchi zinamiliki kila aina ya silaha lakini kuna baadhi zikijaribu kutaka kumiliki tu zinapigwa sanctions za kufa mtu na haohao wanaomiliki kama hizo.
HIvi nchi kama Libya ya Gadafi ilikuwa na tofauti gani na China au Russia katika siasa zake za ndani, lakini yeye kavamiwa ila hao wengine hakuna wa kuwagusa.
Mwendazake alikuwa na kamsemo "you have freedom but not to that extent"
 
Punguza mataputapu, Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, lakini Ukraine siyo sehemu ya Urusi.

Zanzibar haikutaka kujiunga na jumuiya ya kiarabu bali walitaka kujiunga na jumuiya ya nchi za kiislamu OIC.
 
Kwani mkuu Latvia alipokuwa anajiunga NATO ilikuwa mwaka gani? Hali ya Russia kiuchumi na kijeshi ilimruhusu kutunisha misuli mbele ya NATO?
Bila shaka mrusi alishindwa kumzuia Latvia kujiunga NATO kwakuwa wakati huo nguvu hazikumruhusu

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja nikuulize, hii hofu ya Nato kwa Russia inatoka wapi? Je Nato amewahi kusema kwamba siku moja anataka aichukue Russia halafu ili iweje.

Ebu angalia mataifa mawili wanachama wa Nato kama Estonia na Latvia je hawajapakana na Russia? Kwa nini basi Russia haijawavamia kama walivyoivamia Ukraine ambayo bado hata haijawa mwanachama.?

Huyu Russia yeye nani kampa haki au uhalali wa kuyaamulia mataifa mengine mambo yao?
 
Inachokiogopa kwa sasa hawa watu wanakwenda kuonana na Putin kwa lengo la maongezi na suluhu wasije mwekea sumu.
Kuwa na amani kabisa mkuu, hao wanaokwenda kumuona wana tahadhari kubwa wasiteleze kufanya hivyo maana madhara yake ni makubwa wakibainika.
 
Mkuu naomba niingilie swali hili.

Huhitaji kumsikia bwana Stoltenberg akisema kesho wanaivamia Urusi kuelewa Urusi iko hatarini ikiiacha NATO kuwajumuisha majirani zake ndani ya umoja wao. Suala la Jirani kuwa mwanachama wa umoja wa hasimu ni dalili tosha kuwa chochote kinawezekana. NATO wanatoa hakikisho kwa wanachama wake wote kuwa mmoja akishambuliwa ni sawa wameshambuliwa wote. Hii inatosha kuelewa kuwa Urusi akiruhusu kuwa na majirani wenye fikra hizi basi ‘any miscalculation’ yaweza fasiriwa kuwa ‘an act of aggression’ inaeleweka kuwa ‘to avoid war you need buffer zone between great powers’


Hizo nchi za ulizozitaja ni kweli zinapakana kabisa na Urusi, na Warusi si wajinga kuziacha. Waliziacha kwa sababu kuu mbili
1) Zilijiunga NATO wakati Urusi wana hali mbaya kiuchumi, hawakuwa na namna yoyote ya kuzuia.
2) Warusi wanajua ni vinchi vidogo vitagharimu muda mfupi tu kuvituliza wakati wa vita dhidi ya NATO (mungu atuepushe).

Kivipi?
Kimkakati nchi za Baltic zimejitenga na nchi nyingine za NATO na si rahisi NATO kuzilinda vita ikizuka. Japo ukitazama ramani utaona nchi wanachama wa NATO za Poland na Lithuania zinapakana lakini mpaka ule wanamikakati wanauita ‘sulwaki gap’ ( tangu miaka ya 2000 wameandika sana kuhusu hili gap) Wamagharibi wenyewe wanafahamu wazi kuwa Urusi wana Advantage kijiografia hivyo wenyewe wanatazamia kuwa eneo dhaifu kabisa kwao ni ‘gepu la sulwaki’. Kwakuwa Urusi wana hii advantage punde watakapodhibiti gap hili basi nchi za Baltic zitabaki bila usaidizi na itakua rahisi kuzitwaa. Ndio maana unaona Urusi hawashughuliki nao.

Hii ni tofauti kwa Ukraine, ile ni nchi kubwa kijiografia kuiacha ikaliwe na hasimu ni kosa kubwa sana, tujaalie Ukraine imekuwa NATO na vita ikazuka baina ya NATO na Urusi, kwa silaha zilizopo sasa Putin anakadiria itachukua dakika 7 tu kwa kombora toka Ukraine kupiga Moscow. Jambo ambalo halikubaliki vichwani mwa watunga sera wa Moscow.

Ama kwenye swali lako “Huyu Russia yeye nani kampa haki au uhalali wa kuyaamulia mataifa mengine mambo yao?”
Kiufupi kabisa ktk kujibu swali hili lazima tukubali ukweli kuwa siasa za kimataifa zimegubikwa na dhana survival of the fittest.
Ni ngumu kuelewa ikiwa mmoja anatazama mambo juu juu, ni rahisi sana kuelewa ikiwa mmoja atarudi kwenye maana ya msingi kutafuta maana ya ‘uhalali’ na nani aliibua hii dhana ya ‘uhalali’ kama tunavyoiona hii leo, ukioata majibu hapo utaelewa kuwa hizi ni dhana tu hazina nguvu kubwa kama tunavyozipa vichwani mwetu pia utakuja kuona haya mambo hayaamuliwi kihisia au kimaadili kama wengi tungependa mambo yawe, haya mambo hayaendi kwa ‘imaginations’ tulizonazo vichwani za usawa na haki na kuheshimiana.... kwa nchi yoyote lile kipaumbele nambari moja ni usalama wa nchi, kipaumbele hiki kitatimizwa bila kujali chochote kile. Kwenye huu mzozo Urusi anaihisi hatari kwa usalama wake kama nchi ndio maana kwa miaka zaidi ya 20 wamekuwa wakibembeleza NATO wasifanye hivi vitu lakini haikutosha, sasa wamechukua hatua ngumu kuhakikisha wanayotaka yanakuwa nani wa kuwalaumu? Ndio wanaharibu ‘haki’ za nchi nyingine lakini ndio uhalisia wa siasa za kimataifa ili ku-survive ni lazima uwe na jeshi imara kujilinda kinachowakuta Ukraine ni kushindwa kwao kutetea maslahi ya nchi yao na naweza sema bila kupepesa macho huo ndio mwisho wa nchi yoyote itakayoshindwa kujilinda.
 
Mimi sitaandika msaafu ila utakumbuka hili ninalolisema hapa; "Russia has triggered this heinous violence but she will not come out of it victorious and the history of Russia will be rewritten in the aftermath of this inept invasion".
 
Mimi sitaandika msaafu ila utakumbuka hili ninalolisema hapa; "Russia has triggered this heinous violence but she will not come out of it victorious and the history of Russia will be rewritten in the aftermath of this inept invasion".
Ningefurahia zaidi kama ungefafanua ili nifaidike na fikra zako mkuu
 
Mimi sitaandika msaafu ila utakumbuka hili ninalolisema hapa; "Russia has triggered this heinous violence but she will not come out of it victorious and the history of Russia will be rewritten in the aftermath of this inept invasion".
pole MKUU
 
Wanajeshi wake wanapigwa ambush za hapa na pale, wanauawa kinyama.
Ukraine amechafukwa kama noma iwe noma
Kuwa makini na vyanzo vyako vya habari, wakati wa vita Propaganda ni kila mahali.
Unakumbuka wakati wa vita ya Armenia na Azerbaijan mwaka 2020? Aibu kubwa kwa Armenia kwa uongo ule uliokithiri.
 
Kuwa makini na vyanzo vyako vya habari, wakati wa vita Propaganda ni kila mahali.
Unakumbuka wakati wa vita ya Armenia na Azerbaijan mwaka 2020? Aibu kubwa kwa Armenia kwa uongo ule uliokithiri.
Kwa hiyo ulitegemea Russia apokelewe Ukraine kwa nderemo na vifijo. Kumbuka Ukraine ni nchi kamili ina jeshi kama ilivyo Tanzania so usidhani kwamba hii vita ni rahisi kihivyo
 
Kwa hiyo ulitegemea Russia apokelewe Ukraine kwa nderemo na vifijo. Kumbuka Ukraine ni nchi kamili ina jeshi kama ilivyo Tanzania so usidhani kwamba hii vita ni rahisi kihivyo
Mkuu sikatai wanashambuliwa hapa na pale hofu yangu ni kuwa taarifa za wao kupigwa zatiwa chumvi nyingi... ndio
Maana nakutahadharisha. Ila kama unaona haina maana sawa tuendelee na vyanzo hivyo hivyo tu.
 
Nchi 6 zinazopakana na Russia tayari ziko NATO, Hizo ni Norway, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland na Uturuki.

Urusi akiweza kuikalia Ukraine kimabavu atakutana na nchi nyingine 5 za NATO

Sweden na Finland baada ya kuona uvamizi wa Ukraine na Georgia sasa zinafikiria kujiunga na NATO, kwa sababu ni wazi kama Ukraine isingechelewa kujiunga na NATO leo hii isengevamiwa.

Katika mazingira yote hayo hiyo buffer zone anayoitaka Russia iko wapi? Atavamia nchi zote zinazomzunguka na kuweka serikali ya kidekteta kama ya Belarus ili aweze kuipata hiyo buffer zone?
 
Point of correction; Uturuki haipakani na Urusi.

Katika malengo ya Urusi kuikalia Ukraine si miongoni mwao kwa sababu za wazi kabisa kuwa kwa kufanya hivyo lengo lao la kupata Buffer zone halitawezekana na pia kiasi cha rasilimali watu walichokigenga kwaajili ya hii vita hakitoshi kusimamia ukaliaji wa Ukraine.

Yes, Ukraine wangejiunga NATO wakati Urusi ni dhaifu wasingevamiwa ktk kipindi hiki. Labda wakati wa Vita ya tatu ya dunia (Mungu atuepushe)

Buffer zone aitakayo Urusi ni pale Ukraine tu huko kwingine ashachelewa. Umuhimu wa Ukraine nmeeleza kidogo kwenye comment yangu uliyo-reply.
 
Uturuki imepakana na Urusi kwenye Black Sea.

Kama Russia haitaki kuikali Ukraine lengo la mwisho la uvamizi wao ni nini?

Mwisho wa uvamizi wao ili uhasibike umefanikiwa wanataka watimize nini ndio waondoe majeshi yao Ukraine?
 
Uturuki inapakana na Urusi Black Sea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…