Vita ya Urusi na Ukraine: Putin aonya “Yeyote atakayeingilia atapata pigo la kihistoria”

Putin kichaa wa akili
 
Lakini hili biti liliwafanya waweweseke mwanzoni

Hata mimi niliweweseka maana siku zote nilijua Urusi ni supapawa wa kweli, nilijua ni nchi yenye uwezo mkubwa sana yaani picha niliyokua nayo akilini kuhusu Urusi aisei nilijua Ukraine watapigwa ndani ya wiki na hakuna atakayeingilia.

Supapawa akianza kupiga hauwezi kuingilia, angalia namna Marekani hufanya pale akianza kupiga, hutoa tamko moja la "aidha uko naye au uko upande wa adui"....
 
acha ushabiki wa kitoto, marekani ilitishia kumwondoa Maduro wa Venezuela; Russia ikatuma makomandoo bila hata mapigano USA ikaufyata, kule Syria USA ilitaka kumwondoa Bashar al asaad, Russia ikaingilia kati hadi leo Bashar al asad anadunda, Endorgan wa uturuki alipinduliwa na waasi kwa msaada wa USA, Russia ikamrejesha! RUSSIA NI ZAIDI YA SUPER POWER!
 
Milipuko ilisikika Mji Mkuu wa Ukraine, Kiev ambapo Putin akanukuliwa akisema: “Kwa yeyote atakayeingilia kutoka nje, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo katika historia.
Mzee ana mikwara kweli kweli........hao wanaopeleka silaha kwa Ukraine wamekutana na matokeo yapi mpaka Sasa ?
 
Atakaye ingilia mara ya ngapi ? Tayari wameingilia zaidi ya mwaka sasa. Alisema hivyohivyo kuwa Russia lazima icheze FIFA World Cup 2022 ama sivyo hakuna mashindano. Na game zikaendelea bila Urusi
 
kuna mkunya mmoja sijui kama atakuelewa, wengi hawa hawakuwepo wakati wa vita baridi
 

"Mwisho russia sababu anazo, nguvu anayo na uwezo anao ".
Hii kauli bado umeshikilia?
 
Mashabiki wa Putin farijikeni sasa. Marekani SI totalitarian state. Juzi Republicans wamekataa msaada wa Ukraine kuwa ndani ya bajeti ya mpito. Ukraine na washirika wa US wana huzuni sana.

Wapenzi wa Putin sasa ombeni Trump ashinde uchaguzi 2024 na kufuta misaada kwa Ukraine pamoja na kuiondolea Urusi vikwazo. Hapo Putin atashinda kimtelezo. Ombeni sana Trump ashinde na Republicans wapate viti vingi. Ndipo mtakapogundua kuichukia US kama nchi ni ujinga.

Hiyo ndiyo Marekani ya demokrasia. Wananchi ndio wanaoamua mwelekeo. Sio Urusi inayotawaliwa na mungu mtu Putin mliyeamua kumuabudu bila mantiki yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…