Vita ya Urusi na Ukraine: Putin aonya “Yeyote atakayeingilia atapata pigo la kihistoria”

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 

Hehehe mumehamia kwa Trump awaokoe, kipigo kiko pale pale...takbir
 
Hehehe mumehamia kwa Trump awaokoe, kipigo kiko pale pale...takbir
Soma vizuri chief. Huoni kuwa uwezekano wa ujio mpya wa Trump ndilo tumaini kuu la Putin?

In any case, hii vita si ya kushabikia kihivyo. The unnecessary human cost and wanton destruction is really saddening.
 
Soma vizuri chief. Huoni kuwa uwezekano wa ujio mpya wa Trump ndilo tumaini kuu la Putin?

In any case, hii vita si ya kushabikia kihivyo. The unnecessary human cost and wanton destruction is really saddening.

Trump hawezi akawasaidia kitu, Marekani huendeshwa na sera sio mtu.
Leo hii mnasema tusishabikie hii ni baada ya Ukraine kubadilisha kibao, hamkutumia ushauri wenu huo wakati mlikuwa mnashabikia msafara wa Urusi uliofyekwa na wabeba javelin.
 
Russia haiombi chochote marekani na hii vita atashinda ila kwenye vitabu vyenu vya kumbukumbu mtaandikaa ameshindwa kama vita na finland, japan, maana mtu kachukua maeneo yako bado unasema kashindwa kabla hajaandika huu utumbo sema counteroffensive imefikia wapi na mmeredisha maeneo mangapi
 
Trump hawezi akawasaidia kitu, Marekani huendeshwa na sera sio mtu.
Leo hii mnasema tusishabikie hii ni baada ya Ukraine kubadilisha kibao, hamkutumia ushauri wenu huo wakati mlikuwa mnashabikia msafara wa Urusi uliofyekwa na wabeba javelin.
Mmeredisha maeneo mangapi kwanza au ndyo kujifariji au counter offensive imeishia wapi mtoto wa kibera
 
Mmeredisha maeneo mangapi kwanza au ndyo kujifariji au counter offensive imeishia wapi mtoto wa kibera

ile kwamba huyo mtume wenu Putin alishindwa kuparamia hako kainchi ni ushindi tosha, halafu pia maeneo yanamtoka puani hata hivyo, na hiyo ni aibu sana pia.
 
Trump hawezi akawasaidia kitu, Marekani huendeshwa na sera sio mtu.
Leo hii mnasema tusishabikie hii ni baada ya Ukraine kubadilisha kibao, hamkutumia ushauri wenu huo wakati mlikuwa mnashabikia msafara wa Urusi uliofyekwa na wabeba javelin.
Mimi siko huko kabisa katika mjadala huu. Na tafadhali jaribu kuelewa muktadha wa nilichoandika. Ninaonyesha tu kile ambacho Putin na wafuasi wake wanachotumainia: a war of attrition until a “favourable administration” takes office in the US - kama kitatokea, sio nachofikiria mimi.

Wengi wanaoshambulia Marekani na NATO hapa hawaelewi dynamics za utawala wa Marekani na nchi za kidemokrasia (open systems) vs nchi za kiimla (closed systems). Hawajui kuwa ndani ya mfumo wa tawala za Marekani na Ulaya (NATO) kuna pande zinazopishana mitizamo kuhusu hii vita ya Urusi na Ukraine. Kwamba juzi tu wawakilishi toka Republicans kwa wingi wao ndani ya US Congress wameshinikiza msaada kwa Ukraine usiingizwe kwenye bajeti ya mpito.

Mfano mwingine, huko Slovakia (nchi ya EU na NATO) chama cha mgombea anayeunga mkono utawala wa Putin kashinda uchaguzi wa kidemokrasia. Tuone kiasi gani anaweza kubadili upepo na kuchelewesha msaada/support kwa Ukraine (not my wish but food for thought).

Swali ni: Ni sahihi kwa Putin kutegemea mabadiliko ya kidemokrasia ya tawala za US na nchi za NATO ili apate angalau ahueni ya mapambano au ushindi kabisa katika vita aliyoianzisha?

Binafsi siamini kama US na nchi za NATO kwa ujumla wanaweza kuitelekeza Ukraine moja kwa moja. Wao wanatoa pesa na silaha tu. Lakini Ukraine inatoa gharama kubwa sana ya damu (human cost) isiyomithilika kupambana na adui yao wote. Si kitu wanachoweza kukipuuza kirahisi. Afghanistan hakukuwa na wenye nchi waliokuwa tayari kupambana dhidi ya adui. Yote NATO waliyofanya kwa miaka 20 yakaanguka ndani ya “masaa 24”. Lakini kuna dalili za nyufa kwenye demokrasia. Can it be trusted to stay the moral course for Ukraine?

Pamoja na kwamba hii mada ni ya kishabiki zaidi, ningependa kuona wadau pia wakiitambua mikanganyiko (complexities) iliyomo na kujadili mambo yanayofikirisha zaidi. Vita sio jambo la kushabikia tu. The terrible human cost is real.
 

Kiana hujaonyesha chembe za ushabiki kama wavaa makobazi wanaoshabikia Putin kisa wameaminishwa chuki dhidi ya Marekani, hivyo nitathubutu kutumia muda wangu kukujibu, ila kwa wale huwa nawapuuza na kuwatupia mipasho kwenye insha zao.

Kwenye vita vyovyote kuna wale ambao hupinga na hata kuwa upande wa pili tena openly, hususan war of attrition. Pia kuna wanasiasa wa upinzani hutafuta mwanya wa kuponda utawala uliopo almradi waweze kushambulia. Hivyo hayo matamko ya Republican hayashangazi na watafanya mengi tu ikiwemo hata kuleta hoja bungeni za kutaka kusitisha misaada kwa Ukraine.

Hivi vita ni tofauti, Marekani na washirika wake wamekua wakitafuta namna ya kuilezama Urusi kwa miaka mingi sana, kiaina hakuna aliyekua anajua uwezo wa Urusi kijeshi na waliogopwa sana, nakumbuka hata wakati vita vinaanza hao hao Magharibi walimuomba Zelensky aikimbie nchi na walikua tayari kumpa hifadhi, ila akagoma na kukomaa humo ndani kwa ndani hadi akafaulu kufyatua shambulizi lote na kugeuza kibao.

Leo hii Urusi imelemezwa hadi inaomba msaada wa Korea Kaskazini na Iran na kote, hali tete na imekua vigumu wao kushambulia, wamekua defensive huku wakipoteza maeneo ambayo waliyanyakua kwa damu na gharama kubwa sana. Kwa hivyo kadiri Magharibi wanazidi kuwekeza ndivyo wanaizika Urusi, na wameaanza maandalizi ya bajeti ya miaka mitano ijayo.

Hao Ukraine kwa upande wao hii ndio fursa imejitokeza ya kujikomboa na hawawezi kuiachia, kumbuka kuna miaka walimiliki silaha za nyuklia ila wakashawishiwa na Urusi kuziachia kwa ahadi kwamba Urusi haitokuja hata siku moja iwashambulie, kitu ambacho ilikiuka na kumega Crimea na juzi walithubutu kuparamia Ukraine yote, hivyo kwa jamii ya watu wa Ukraine, hapa wako tayari kufa hata milioni ila wajikomboe na kwa ajili ya vizazi vya kesho.

Mrusi ndiye anapoteza maana mpaka hapo Warusi wenyewe hawajui wanakwenda kufia nini Ukraine, kama ni ardhi wanayo ya kumwaga, madini yapo yote, raslimali za kila aina, hawaelewi tija ya hivi vita dhidi ya haka kainchi ambapo kenyewe ni saizi ya mkoa wao moja.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…