Vita ya ushuru ya Trump ni sawa na mwizi kupiga mayowe ya mwizi

Vita ya ushuru ya Trump ni sawa na mwizi kupiga mayowe ya mwizi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
1747031744745.png


Wakati dunia inaendelea kutafakari mantiki ya hatua zinazochukuliwa na serikali ya Marekani kuongeza ushuru wa bidhaa kutoka nje, kauli zinazotolewa na Rais Trump kuwa Marekani “imeibiwa, imeporwa na kudhulumiwa” na maadui na marafiki, inakumbusha historia iliyopitia Afrika ya kuibiwa, kuporwa na kudhulimiwa. Na Marekani yenyewe ikiwa ni nguzo iliyojenga mfumo ambao kwa muda mrefu umekuwa wa kiporaji na kandamizi kwa Afrika, inafurahisha kusikia Bw. Trump akilalamika.

Kama mwizi akijitokeza na kupiga mayowe ya mwizi, ni wazi kabisa kuwa mwizi anatafuta njia ya kujihama ili alichoiba kisiibiwe. Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu anajua vizuri kuwa Marekani ndio nchi tajiri na nchi yenye nguvu kiuchumi kuliko nchi yoyote duniani, na pia ndio nchi ambayo imejenga utaratibu wa sasa wa dunia, ambao unaitwa “utaratibu wa kufuata kanuni” (rule based order).

Tangu Donald Trump aingie madarakani Marekani imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kushambulia utaratibu ambao imeujenga, ikiutaja kuwa ni utaratibu ambao unaidhuru Marekani yenyewe. Swali la kujiuliza, ni kwanini Marekani ijenge utaratibu wa dunia ambao utaidhuru Marekani yenyewe? Ukweli ni kwamba Marekani haiwezi kujenga utaratibu wa kujidhuru yenyewe, kilichopo ni kwamba nchi mbalimbali duniani zimepata njia za kuweza kujitokeza licha ya kuwekwa katika mazingira magumu yaliyowekwa na Marekani.

Ukweli ni kwamba katika miaka 50 iliyopita dunia imepita kwenye mabadiliko mengi, kwa kiasi kikubwa dunia imekuwa na utulivu na nchi nyingi duniani zimepata maendeleo ya sayansi na teknolojia, na kuweza kujenga uchumi imara na wenye nguvu. Kinachoonekana ni kuwa kanuni za kufuatwa zilizowekwa na Marekani sasa inaonekana zinanufaisha nchi nyingine, hicho ndicho hasa ambacho Marekani haikitaki.

Kwa muda mrefu Marekani ilihimiza utaratibu unaoiwezesha kuuza bidhaa zake katika nchi mbalimbali duniani. Na nchi ambazo masoko yake yalifungwa kwa Marekani, Marekani ilifanya kila njia nchi hizo zionekana mbaya na adui kwa dunia. Lakini baada ya nchi mbalimbali kuanza kuuza bidhaa Marekani, Marekani sasa inaanza kuziona nchi hiyo ni adui na inaamua kuzitoza ushuru mkubwa, na kuzitaka nchi hizo zisiitoze ushuru Marekani. Wapenzi wa soka wanalinganisha hatua za Bw. Trump, sawa na kitendo cha kuhamisha magoli wakati timu pinzani inakaribia kufunga goli.

Kwa muda mrefu sasa Marekani imekuwa ni championi wa biashara huria, na nchi na makundi mbalimbali duniani yamefuata njia hiyo ambayo imekuwa ikipendekezwa na Marekani. Tukiangalia Umoja wa Ulaya, kimsingi ni Umoja ambao umeanzishwa kwa lengo la kuhimiza biashara kati ya nchi wanachama, na kuikaisi Marekani kiasi kwamba baadhi ya watu watumia jina la utani United States of Europe. Lakini hivi karibuni Bw. Trump alisikika akilaani Umoja huo akisema kuwa ulianzishwa kwa lengo la kuidhuru Marekani. Kwa maana nyingi Trump alipenda nchi za Ulaya ziendelee kuwa nchi vidogo vidogo ambavyo inaweza kuviburuza kirahisi, tofauti na ilivyo sasa kwa Umoja wa Ulaya.

Kimsingi Marekani ni nchi ambayo imeongoza mfumo ambao hadi sasa unaendelea kuinufaisha. Cha ajabu ni kwamba inalalamika kuwa mfumo huo unaifanya “iibiwe, iporwe na kudhulumiwa”. Tukiangalia kwa undani tunaweza kuona kuwa huenda Marekani haiwezi kuvumilia kuona nchi nyingine zinapiga hatua, na kupiga kwao hatua kunafanya maslahi yake yaliyodumu kwa miaka mingi yapungue. Hili ndio linafanya Bw. Trump atake maslahi zaidi kwa kuzirudisha nchi nyingine nyuma kwa ushuru.
 
Back
Top Bottom