Kawaida kila kinywaji kipya (masanga) kinakuja na kishindo chake. kwenye haya mambo yetu ni sawa tu na pale baa au club mpya inapofunguliwa, utadhani zingine hazifai.
Serengeti lite anapita tu, atapotea wakati ukifika. Castle lite ni chuma kile, hata kikijikongoja kwa sasa lakini kitabakia.
K Vant hauwezi mziki wa Nyagi. Konyagi ina wanywaji wake bwana. wanywaji wa kvant ni waigizaji tu, tena tunaweza sema ni waonjaji tu. Wanywaji wa ukweli wanaiheshimu na kuitukuza konyagi. Amini nawaambieni itafikia kipindi KVant atabaki historia.
Kwenye ulabu bwana mkongwe siku zote atabaki mkongwe na sifa yake itadumu. Balumi, japo si kongwe lakini huwezi kuilinganisha na Pilsner. Japo Pilsner ni ya kitambo lakini ni bia tofauti kabisa na balimi. ni sawa na kulinganisha bamia na kitunguu.
Angalia, kuna bia kama safari, Castle lager, Ndovu, nk ni za kitambo na bado zinatamba. zipo zitakozokuja na zitakazoondoka au kufifia, mkongwe anabaki na hashima yake milele.
Agggggh! wacha niwahi maeneo nikajipoze na safari+peck za nyagi (mambo ya bia na tera lake). Leo katikati ya wiki nitakuwa grocery tu ................... wadau wenzangu tunaopafahamu natangulia mie