Tokea vita kati ya Israel na Marekani Vs Iran vianze, bei ya mafuta imezidi kupanda, na kuzinufaisha nchi wazalishaji wa mafuta. Lakini mambo ni tofauti kabisa kwa Iran iliyo chini ya vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi yake na Marekani na mataifa rafiki.
Inaelezwa kuwa tangu vita vianze, uchumi wa Iran unapomoka kwa viwango ambavyo havijawahi kutokea mahali popote Duniani. Thamani ya sarafu ya Iran, Rial imepotomoka mpaka kufikia rial milioni 1.8 kubafilishwa kwa dollar 1 ya Marekani.
Bei za vyakula zimepanda kwa 115%, huku wastani wa mfumko wa bei kwa ujumla ukiwa umefikia 68.9%. Katika kukabiliana na hali hiyo, rushwa na ufisadi kwa watumishi wa setikali, vimeongezeka maradufu, na kuzidi kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi wa kawaida.
Wakati hayo yakiendelea, serikali ya Iran inasema kuwa mamilioni ya ajira zimepotea, huku serikali ikihangaika kurekebisha miundombinu na supply chain zilizoharibiwa na mashambulio ya kivita toka Israel na Marekani.
Kama hali ndivyo ilivyo, kwa nini Iran isikubaliane na uhalisia ili vita vikome moja kwa moja, na uhasama uishe ili wananchi wake, mataifa jirani na mahasimu wake, Israel waishi kwa amani, wahangaikie maendeleo kuliko kila siku ni vita tu?
Msimamo mkali wa Iran kuwa hakutakiwi kuwa na Taifa la Israel Duniani, na kwamba wayahudi wanatakiwa kuangamizwa, na kuwa ni agizo la Allah; ni kikwazo kikubwa sana kuumaliza uhasama kati ya Iran na Israel.
Kutokana na msimamo huo mkali wa Iran, unaifanya Israel kuona kila jitihada zinazofanywa na Iran kwenye masuala ya silaha (makombora ya masafa marefu na urutubishaji wa nuclear energy), uundwaji na uimarushaji wa makundi ya kigaidi, unalenga kutengeneza mazingira ya kuiangamiza Israel.
Lakini kwa upande mwingine, tamko la Ayatollah kuwa wasuni siyo waislam, na kwamba tawala zote za kisuni zinatakiwa kuondolewa, umejenga uhasama na mataifa ya kiarabu.
Kama Iran haitaweza kufuta falsafa zake hizo mbili: dhidi ya Israel na dhidi ya wasuni, Mashariki ya kati haitakuja kuwa na amani, na wairan wataendelea kuishi kwenye mateso yanayosababishwa na uchumi duni.
Iran’s economy is in a state of freefall, reeling from years of harsh sanctions, systemic corruption, and the severe impacts of the recent war.
The country is facing a historic economic crisis characterised by widespread infrastructure destruction, mass job losses, skyrocketing food prices, and a collapse of the national currency.
The Iranian rial has plummeted to historic lows, reaching up to 1.8 million to the U.S. dollar.
Overall inflation hovers around 68.9%, with food inflation soaring past 115%.