Vitabu 50 Unavyopaswa Kuvisoma Kabla Mwaka Huu 2019 Haujaisha Kama Unataka Mafanikio Makubwa.

Vitabu 50 Unavyopaswa Kuvisoma Kabla Mwaka Huu 2019 Haujaisha Kama Unataka Mafanikio Makubwa.

huo muda unasoma vitabu 50 ukiutumia kufanya biashara kwa bidii au kazi kwa bidii utafika mbali sana. mwisho wa mwaka nitakuwa na hela nyingi wewe utakuwa na story nyingi kichwani
 
huo muda unasoma vitabu 50 ukiutumia kufanya biashara kwa bidii au kazi kwa bidii utafika mbali sana. mwisho wa mwaka nitakuwa na hela nyingi wewe utakuwa na story nyingi kichwani
Muda ule ule ambao mtu anaupoteza sasa kwenye mambo yasiyo ya msingi, kwa kuzurura kwenye mitandao ya kijamii na kufuatilia udaku, akiupeleka kwenye kusoma vitabu atapiga hatua zaidi.
Na wala huhitaji siku nzima ya kusoma, ni nusu saa tu mpaka saa moja kwa siku ya kujifunza na ukaondoka na maarifa yatakayokuwezesha kupiga hatua zaidi.
Karibu ujipatie vitabu na kuwa msomaji mzuri, utapiga hatua zaidi ya pale ulipo sasa.
 
Kitu ambacho hua najiuliza n Hawa wanaotuandikia ivi vitabu vya kutu motivate kwanini Misha yao hayaendani na wanavyoviongea Yana wakupamba kwa mafanikio makubwa ambayo wao hawana

Au ndio ule msemo wa mganga hajigangi
 
Kuna aina mbili za waandishi inapokuja kwenye uandishi wa mambo ya hamasa.
1. Kuna ambao wanajifunza na kuandika yale waliyojifunza, kama sehemu ya wao kupiga hatua na hata wengine kupiga hatua.
2. Kuna ambao wanaandika kutokana na uzoefu wao binafsi, kwa yale waliyopitia na jinsi walivyoweza kupiga hatua.
Hivyo inategemea umemwangalia mwandishi wa aina ipi.
Lakini kilicho muhimu zaidi ni kwamba kama maarifa ni sahihi na ukiyatumia yanafanya maisha yako kuwa bora zaidi basi yafaa kutumia.
 
waandishi wa vitabu wenyewe wanajikwamua na ugumu wa maisha, na vizur kusoma vitabu ila sio kupoteza muda mwingi wa kukesha badala ya kufanya kazi kwa bidii,maan theory sio kitu bila practical
 
Unawezaje Kuchambua Vitabu 50 vya hamasa za kibiashara na ukakosa Kitabu hata kimoja cha Robert Kiyosaki? Muwe serious bas, au huwa hamuelewi anacho andika?
 
waandishi wa vitabu wenyewe wanajikwamua na ugumu wa maisha, na vizur kusoma vitabu ila sio kupoteza muda mwingi wa kukesha badala ya kufanya kazi kwa bidii,maan theory sio kitu bila practical
Ni kweli kabisa, usomaji wa vitabu haupaswi kuwa mbadala wa kuchukua hatua.
Lazima ujifunze sana na lazima uchukue hatua kubwa katika yale uliyojifunza.
Kujifunza bila ya kuchukua hatua ni kujidanganya.
Karibu sana ujipatie vitabu.
 
Unawezaje Kuchambua Vitabu 50 vya hamasa za kibiashara na ukakosa Kitabu hata kimoja cha Robert Kiyosaki? Muwe serious bas, au huwa hamuelewi anacho andika?
Mkuu vitabu vinavyohusu hamasa na mafanikio ni vingi mno, waandishi ni wengi mno, na vitabu vya Kiyosaki na wengine nimevichambua kwenye mafunzo mengine ninayotoa.
Kwenye programu ya KISIMA CHA MAARIFA nimechambua kitabu kizima cha RICH DAD POOR DAD sura kwa sura na hatua za mtu kuchukua kupitia yale anayojifunza.
Kadhalika, vitabu 50 nilivyoshirikisha hapa siyo kwamba ndiyo vitabu pekee nimesoma. Tangu mwaka 2014 nimekuwa nasoma angalau vitabu 100 kila mwaka, hivyo kwa jumla ya vitabu nimesoma mpaka sasa vinazidi 500.
Tangu mwaka jana ndiyo nimeanza uchambuzi huu wa kina wa vitabu na baadaye kuuweka kwenye kitabu kimoja kama hivi.
Hivyo kama kuna vitabu zaidi na chambuzi zake unahitaji karibu utembelee www.amkamtanzania.com na www.kisimachamaarifa.co.tz na utaweza kujifunza zaidi.
Karibu sana.
 
Karibuni mjipatie vitabu vya kuongeza maarifa na kuweza kupiga hatua zaidi kwenye chochote kile ambacho mtu unafanya.
 
Karibuni mjipatie vitabu vya kuongeza maarifa na kuweza kupiga hatua zaidi kwenye chochote kile ambacho mtu unafanya.
Sipingi swala la usomaji wa vitabu ila najiuliza kwa sauti kubwa! Ikiwa hao wandishi wa ivyo vitabu wana mbinu na njia mbali mbali ambazo mtu akizitumia anatoboa maisha! anapasua au tuseme anatusua , kwanini wanaviuza ivyo vitabu wanaviuza ili iweje ikiwa wao wanazijua njia zote za kufanya ili mtu atusue kwanini bado wanataka uyu mtu asiye na kitu apoteze tena ela yake kwa kununua icho kitabu chake?
 
Daktari, nilisoma kitabu cha Think and grow rich,tena nilikinunua kwa elfu 5(5,000) Ubungo mataa, kuna jamaa kapanga tu vitabu vizee chini katikati ya kingo zitenganishazo Barabara iendayo mjini na Morogoro 2012 ! Kwasababu ya kingereza nikapenda, just think and grow rich! Kwa dhati kimenibadili! Nikaamua ujasiriamali, nikawa mbishi kama usemavyo, nikakomaa! Nikajijengea imani, siyo kufuata dini kama usemavyo,kuwa bold na halafu Mungu anasaidia. Gharama ya kitabu chako?
 
Maarifa ni uwekezaji, maarifa ni gharama.
Napoleon Hill wakati anatafiti na kuandika moja ya vitabu bora kabisa vya mafanikio THINK AND GROW RICH, alifanya utafiti kwa muda wa miaka 25. Kwa miaka yote hiyo alikuwa akiwafuatilia wanaofanikiwa na wanaoshindwa na kisha kuchakata na kuja na kanuni za mafanikio.
Kutafuta na kuandaa maarifa haya kwa njia rahisi ya mtu kuelewa ni gharama, na ndiyo maana ili mtu ayapate lazima aingie gharama pia.
Kama watu wanavyolipa ada mashuleni na vyuoni, ni kwa sababu kuna watu wanatumia muda wao kuandaa na kuwafundisha. Hilo ndiyo linafanya maarifa yawe na gharama.
 
Daktari, nilisoma kitabu cha Think and grow rich,tena nilikinunua kwa elfu 5(5,000) Ubungo mataa, kuna jamaa kapanga tu vitabu vizee chini katikati ya kingo zitenganishazo Barabara iendayo mjini na Morogoro 2012 ! Kwasababu ya kingereza nikapenda, just think and grow rich! Kwa dhati kimenibadili! Nikaamua ujasiriamali, nikawa mbishi kama usemavyo, nikakomaa! Nikajijengea imani, siyo kufuata dini kama usemavyo,kuwa bold na halafu Mungu anasaidia. Gharama ya kitabu chako?
Hongera sana kwa kusoma kitabu hicho bora kabisa chenye kanuni zote muhimu za mafanikio.
Kuna vitu viwili vinachangia vitabu kuwa bei ghali ukilinganisha na vingine.
Moja ni ukubwa wa kitabu, kitabu cha TANO ZA JUMA ambacho kinauzwa tsh elfu 50, ni mara nne kwa ukubwa wa kitabu cha THINK AND GROW RICH, hapa ni kwa kurasa na ukubwa wa kitabu pia, hivyo uchapaji wake una gharama kubwa.
Mbili ni gharama za uchapaji, kwa hapa Tanzania, gharama za kuchapa vitabu zipo juu sana, hasa unapotaka kitabu ambacho ni cha ubora wa hali ya juu. Tofauti na nchi nyingine, hasa India ambapo naamini kitabu ulichosoma kimechapwa huko, gharama ziko chini mboni, ni zaidi ya nusu ya gharama utakazotumia hapa kuchapa kitabu.
Hizo ndiyo sababu zinapelekea gharama kutofautiana kwa kiasi kikubwa.
Karibu sana ujipatie vitabu ili uweze kupata maarifa sahihi ya kukuwezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
 
Back
Top Bottom