Vithibitisho vya uwepo wa Mungu.
Ni matendo yake jinsi anavyojidhihirisha kwenye maisha ya wanadamu.
Je, unaelewa Mungu ni wa namba gani?
Hachunguziki, Bali kila Mwanadamu anaouwezo wa kuelezea ukuu wa Mungu kadri jinsi Mungu alivyojifunua kwa Mwanadamu kupitia Matendo yake Makuu ambayo ni nje ya uwezo wa Mwanadamu.
Uthibitisho wa Uwepo wa Mungu upo kwenye jamii yetu inayotuzunguka, Ukuu wake unaonekana.
Watu kila siku wanashuhudia jinsi walivyokombolewa ,Jinsi Mungu alivyowasaidia kutoka kwenye Kifungo cha Nguvu za Giza.
Je, huna Imani na jamii inayokuzunguka?
Rehema na kweli zisifarakane nawe.
Hujathibitisha Mungu yupo unafanya circular argument.
Nakuambia thibitisha Mungu yupo.
Unaniambia Mungu yupo kwa sababu tunaona matendo yake.
Unahakikishaje hayo matendo ni ya Mungu tu na si vinginevyo?
Unasema Mungu hachunguziki.
Sasa kama Mungu hachunguziki wewe umejuaje hachunguziki?
Kama Mungu hachunguziki, umejuaje haya ni matendo ya Mungu?
Na unajuaje hiyo habari kwamba Mungu hachunguziki si ya kutungwa na watu tu kukupoza ukubali Mungu yupo bila uthibitisho wa uchunguzi?
Unasema kila mwanadamu anaelezea ukuu wa Mungu, mimi na atgeists wengi hatukubali uwepo wa Nungu hapo huna hoja, unalqzinisha mambo tu.
Kusema watu wengi kumshuhudia Mungu yupo ndiyo uthibitisho Mungu yupo ni logical fallacy, argument from popularity. Watu wengi kushuhudia kitu hakufanyi kitu kiwe kweli. Kitu cha kweli kinaweza kisikubalike na wengi, halafu cha uongo kikakubalika na wengi.
Ukweli hautegemei jura za watu, utasimama palepale ukikubaliwa na watu wengi au wachache.
Hujathibitisha Mungu yupo.
Umeandika circular logic na logical fallacies mwanzo mpaka mwisho.
Hujathibitisha Mungu yupo.