Parasite
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 613
- 575
Share soft copy kama unayo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Share soft copy kama unayo
Kinavutia. 4.3 overall rating, it must be a good read.In God's name.....David Yallop
How they stole the game....David Yallop
Fist of God.....Fredrick Forsyth
Papilon.... Papilon
Round the world in eighty days.
Six against the rock........a must read
Mwisho wake huwa si mzuri nimesoma kadhaa.James Hadley Chase....ana vitabu vizuri sana dizaini ya Willy Gamba...
Inawezekana...tunaweza kumuongeza Sidney SheldonMwisho wake huwa si mzuri nimesoma kadhaa.
Nashukuru sana kwa uchambuzi huu mkuu. Mara nyingi mambo yanakuwa tofauti na yanavyoonekana. Nitajitahidi nipate muda nimelizie hicho kitabu.DHANA YA MALTHUS NA MLIPUKO WA KIJAMII KUTOKANA NA UWIANO USIO SAWA KATI YA IDADI YA WATU NA RASILIMALI.
Baada ya muda mrefu, hatimaye nimemaliza kusoma kitabu kiitwacho Collapse cha Jared Diamond. Katika kitabu hiki, Diamond anaelezea jamii mbalimbali zilizoshamiri na hatimaye kuanguka na baadhi zikisalimika. Anaposema kuanguka kwa jamii ni kushuka kwa kasi —na wakati mwingine kutoweka kabisa—kwa jamii kwa upande wa idadi ya watu, mifumo yake ya kiuchumi, kijamii na/au ya kisiasa. Zipo jamii za kale maarufu na kubwa zilizotoweka kama vile Maya, na zipo zilizoko kwenye hati hati ya kuanguka kama vile Haiti. Kwa ujumla wake Diamond anaelezea Sababu tano za jamii kuanguka [kwa kurejea historia]—au kwa maneno mengine huamua hatma ya jamii husika—ambazo ni matokeo ya shughuli za binadamu kwenye mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa, mahusiano na jamii jirani, madhara yatokanayo na uhasama wa jamii nyingine na muhimu ni nini jamii husika hufanya kupambana na matatizo yake.
Moja ya jamii iliyozungumziwa kwenye kitabu hiki Rwanda. Mwaka 1994, yafahamika kuwa Rwanda ilikumbwa na mauji makubwa, ikikisiwa watu Milioni Moja waliuwa. Na kwa kuwa mauji haya yalikuwa ni ya kimbari (racial killings), watusi wengi ndio waliouwa kwa kuwindwa na wahutu ikikisiwa watutsi 800,000 wakiuawa. Lakini pia wahutu takribani 200,000 waliuawa. Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa, ni mauji ya kimbari, basi watutsi waliuliwa na wahutu huku wahutu wakiuliwa na watutsi. Lakini, tafiti zinaonyesha kuwa wapo watutsi waliouawa wenyewe kwa wenyewe hali kadhalika wahutu wakiuawana wenyewe kwa wenyewe, mfano zipo jamii ambazo ni za wahutu pekee, lakini mauji yalikuwa 5% ya idadi ya watu. Kama ni mauji ya kikabila, mbona hapa hakukua na watutsi? . Ukisoma tafiti na takwimu, unaona kuwa licha ya kuwa ni kweli chuki za kimbari zilichochea na wanasiasa kuamua mauaji haya, lipo jambo jingine ambalo lilikuwa ni petrol kwenye moto huo wa chuki za kimbari—UHABA WA ARDHI.
Miaka ya 1700, mchumi wa kiingereza Thomas Malthus, alikuja na dhana inayoeleza kuwa, ukuaji wa idadi ya watu huwa na kasi kubwa (hujizidisha) kuliko ukuaji wa uzalishaji wa chakula (hujiongeza); hivyo kama hatua za makusudi —kama vile udhibiti wa uzalianaji—au za bila kutegemewa au bahati mbaya—kama majanga, vita au njaa— zisipotokea, basi itafika mahala kutatokea mlipuko mkubwa wa watu na hivyo kusababisha mnyukano mkubwa kwenye jamii husika. Mfano, kama ukuaji wa watu huongeza mara mbili kila baada ya miaka 30, hivyo, leo 2021 tutakuwa watanzania Mil 60, mwaka 2051 tutakuwa mil 120, 2081 tutakuwa Mil 240. Ukuaji mara mbili wa idadi ya watu, huchochea ukuaji la uzalishaji wa chakula kwa ongezeko, mfano leo wakati 2021 tuko Mil 60, na uzalishaji wa chakula ni Tani 50; 2051 tutakuwa mil 120 huku chakua kikiongezeka uzalishaji wa chakula kwa asilimia hivyo kuwa Tani Mil 75. Watu Mil 240, chakula itakuwa Mil 100. Na Sababu kuu ni kuwa ardhi haingezeki. Hivyo kwa mujibu wa dhana ya Malthus, jamii ikifika ongezeko la watu lisilowiana na ongezeko la uzalishaji wa chakula cha kutosheleza na hatimaye ardhi kuwa ndogo, kifuatacho ni mauji ya kugombea ardhi.
Rwanda na Msongamano wa watu; Kihistoria toka miaka ya 1800, Rwanda ni nchi iliyokuwa na msongamano mkubwa wa watu uliosababishwa na mvua nzuri kwa kilimo na ardhi yenye miinuko hivyo kutoathiriwa na mbu na mbung'o. Kwa wastani, idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa 3% kwa mwaka. Hata miaka ya 1990 baada ya mauji, bado Rwanda ilikuwa na Msongamano wa watu 760/Sq Mile ikiizidi Uingereza yenye 610/Sq Mile na ikiikaribia Uholanzi yenye 950/ Sq Mile, lakini Uingereza na Uholanzi zilikuwa na kilimo cha zana za kisasa ni watu wachache waliolima kinyume na Rwanda ambayo kilimo ni jembe la mkono, uzalishaji duni hivyo takribani kila mtu ilimpasa alime ili apate chakula.
—Hadi kufikia kipindi cha baada ya uhuru, ardhi yote ya Rwanda, nje ya ardhi ya hifadhi ilikuwa inalimwa—wapo walitania kuwa Rwanda ni kama bustani. Vita za mwaka 1960 na 70, zilipelekea watutsi kufa na wengi kukimbia nchi, hivyo kuwapa fursa wahutu kupata ardhi. Kilimo kiliendelea kuwa cha mkono, na kisochozingatia maeneo ya kulima, mfano milimani mazao yalizolewa na udongo sababu ya mmomonyoko. Miaka ya 1980 walishuhudia upungufu wa chakula kutokana na ukame, mbinu za hovyo za kilimo, mabadiliko ya tabia nchi na ukataji holela wa miti.
—Wanazuoni wa kibelgiji, Catherine André na Jean-Philippe Platteau, walifanya utafiti wao kwenye mji wa Kanama uliopo kaskazini magharibi mwa Rwanda kati ya miaka ya 1980 na 1993. Katika tafiti yao, walihoji wanyarwanda katika meneo matatu; Idadi ya wanakaya, ukubwa wa ardhi inayomilikiwa na kaya na utegemezi wa wanakaya kwenye kilimo na nje ya kilimo.
—Kijiografia, Kanama ni mji wenye ardhi yenye rutuba ya kivolcano, hivyo inafaa sana kwa kilimo na kupelekea kuwa na Msongamano mkubwa wa watu. Mf, 1988 ilikuwa na watu 1,740/Sq Mile na kufikia 2,040/Sq Mile mwaka 1993 [Ongezeko la asilimia 85. Ambayo ni sawa na shamba [kwa kila kaya] lenye ekari 0.89 mwaka 1988 na kushuka kufikia ekari 0.73 mwaka 1993. Ili kupata maeneo ya kulima, kwa wastani kila mkulima [mwanakaya] alilima ekari 0.09 mwaka 1988 na eneo kupungua kufikia 0.07 mwaka 1993.
—Sababu hakukua na ardhi tena, vijana [20-25s years] hawakuwa na uwezo wa kujitegemea kimaisha i.e kuoa, kupata ardhi na kulima. Mf, mwaka 1988 wasichana walioishi majumbani kwao walikuwa ni 39% na wavulana 71%, mwaka 1993 wasichana iliongezeka kufikia 67% huku wavulana ikiongezeka kufikia 100%. Maana yake mwaka 1993 hakuna kijana aliyeweza kuondoka kwao na kujitemea kwa sababu ya kutokuwa na ardhi.
—Hii tafsiri yake ni kuwa, wasichana na wavulana walirudi makwao, na kuepelekea idadi ya wanakaya kuwa kubwa na hivyo wengi zaidi kulima kwenye eneo dogo. Mf, mwaka 1988 kila kaya ilikuwa na watu wanaolima wa wastani wa 4.9 iliongezeka kufikia 5.3 mwaka 1993. Hivyo kiuhalisia Mwaka 1988 kila mwanakaya alilima ⅕ ya ekari, na kupungua hadi ⅐ ya ekari mwaka 1993. Hii ilikuwa na madhara hadi kwenye kiwango cha virutubisho walivyopata, ni 77% tu ya Calories walizopata ndio zilitoka shambani, zingine ilibidi wanunue chakula kutokana na kazi kama za kapenta, ufyatuaji tofali n.k. Mf watu wenye njaa i.e wanaopata chini ya Calories 1,600 kwa siku, walikuwa 9% mwaka 1992, na kuongezeka kufikia 40% mwaka 1993.
—Pia hali ya umiliki usio sawa wa mashamba—Shamba kubwa (zaidi ya ekari 2.5) na shamba dogo (chini ya ekari 0.6)— nao ulibadilika kadri miaka ilivyozidi kwenda. Mf mwaka 1988 mashamba madogo 7% hadi 40%. Maana yake ni kuwa, jamii za wakulima ziliongezeka matabaka, wachache wenye ardhi kubwa waliendelea, huku tabaka la kati likizidi kuwa na ardhi ndogo ndogo zaidi. Sababu kwa kaya masikini ardhi ilizidi kuwa ndogo, ililazimu kufanya kazi kwa wenye mashamba makubwa, hivyo masikini akizidi kuwa masikini na tajiri akizidi kuwa tajiri. Lakini, masikini waliuza sana ardhi zao ili kukidhi mahitaji kama afya, chakula, mashitaka, kupata fedha ya rushwa; huku tajiri huuza shamba ili kupata lenye faidia zaidi kama vile ukaribu.
—Kwa misingi hiyo, masikini walizidi kuwa masikini zaidi na frustrated, huku wachache wakiwa na utajiri zaidi huku wakiwa hawana frustration. Pia ilizaa tension ndani ya familia, mf binti anaposhindwa kuhudumiwa na mmewe, hurudi kwao hivyo kuongeza mzigo wa kulishwa, na pili wakaka huchukizwa pale anapokuwa na mtoto wa kiume—urithi. Hivyo, wajane, watoto wao iligeuka kuwa shida kuhudumiwa na familia zao. Pia ilileta tension kati ya mahusiano ya watoto na baba. Kimila baba akifariki, basi mtoto wake wa kwanza wa kiume hurithi. Kwa wasiwasi huu, baadhi ya wazee waligawa mali zao kwa watoto wote, ambayo nayo huzua migogoro mikubwa ya ndani ya familia. Na mauji yalipoanza yalitoa fursa kwa mauji ya familia.
Ukitazama wahanga wa mauji, mf eneo la Kanama, wanaangukia moja kati ya makundi haya sita.
i. Watutsi walioishi pekee yao au wajane. Sababu za kuuliwa yaweza kuwa ni ututsi, lakini ipo sababu nyingine. Mjane amerithi ardhi kubwa kutoka kwa mmewe, pia ameshiriki migogoro mingi ya ardhi, au pia mmewe alikuwa ni mhutu mwenye wake wengi.
ii. Kundi la pili ni wahutu wenye umiliki wa ardhi kubwa. Wengi wao hawa wana umri wa 50+. Hivyo ni kundi la kina baba. Watoto na wadogo zao walitaka ardhi.
iii. Pia wapo vijana waliomiliki ardhi kubwa mf kwa kurithi, hivyo waliwapa wivu vijana wenzao kuitaka ardhi yao.
iv. Kundi jingine ni wasumbufu wa migogoro ya ardhi. Hawa walikuwa ni wahutu walioshiriki migogoro mingi ya ardhi. Hivyo walikuwa kwenye chuki kubwa na makundi mengi.
v. Wahanga wengine ni wahutu ambao hawakuwa na ardhi. Hawa walijiunga na vikundi vya mauji kwa sababu ya kutokuwa na ardhi kabisa.
vi. Kundi la mwisho ni wahanga ambao walikuwa na hali ngumu za kimaisha sababu ya kutokuwa na chakula, pia walikuwa na ardhi ndogo au hawana kabisa kiasi cha kutokuwa na akiba ya chakula cha kuwawezesha kuhimili kipindi cha vita. Na wapo ambao hawakuwa na hela sababu ya kutokuwa na kazi kwa sababu walitegemea kufanya kazi za kuajiriwa nje ya mashamba.
“The 1994 events provided a unique opportunity to settle scores, or to reshuffle land properties, even among Hutu villagers . . . . It is not rare, even today, to hear Rwandans argue that a war is necessary to wipe out an excess of population and to bring numbers into line with the available land resources.” As Gérard Prunier, a French scholar of East Africa, puts it, “The decision to kill was of course made by politicians, for political reasons. But at least part of the reason why it was carried out so thoroughly by the ordinary rank-and-file peasants in their ingo [= family compound] was feeling that there were too many people on too little land, and that with a reduction in their numbers, there would be more for the survivors.”
Ukitazama tafiti hii, unaona suala la ardhi linavyochochea (kificho) ushiriki wa vijana kwenye vita au machafuko ya kisiasa. Turejee mfano wa Kenya mwaka 2007.
Cc: Red Giant Paula Paul Iceberg9 Kiranga
Kabisa. Kiasili jamii za wanadamu kwa wakati wote, hukumbwa na misukosuko inayotishia maanguko yao, kinachofanya jamii moja ipone na nyingine ianguke ni reaction ya jamii husika juu ya matukio hayo.Nashukuru sana kwa uchambuzi huu mkuu. Mara nyingi mambo yanakuwa tofauti na yanavyoonekana. Nitajitahidi nipate muda nimelizie hicho kitabu.
Nilikuwa najiuliza siku zote kwanini Rwanda ma Burundi zina watu wengi kupita kiasi. Leo nimepata jibu.
Hiki kitabu ni muhimu sana leo, hiyo trend ya vijana kuwa masikini, kutokuwa na mbele wala nyuma inatujia kwa kasi hapa Tz. Huko Naigeria imeshaanza kuleta shida kubwa. Huko South Africa EFF inapata nguvu kubwa sababu ya hilo, na inahubiri vurugu na kuchukua ardhi bila fidia. Leo SA wanafanya uchaguzi wa serikali za mitaa, bila shaka EFF itazidi kupata nguvu. Umesema kwamba njia nyingine ya kuamua hatima ya situation kama hiyo ni jinsi serikali inapambana nayo. Ni wakati wanasiasa wetu waafrika waamke, bara linazidi kuwa kame, teknolojia ya kilimo bado ni primitive huku watu tukiongezeka kwa kasi. Muda si mrefu nchi yetu itajikuta pabaya.
Shukurani kwa uchambuzi. Jared Diamond namfuatilia sana. Nimevisoma "Gun,Germs and Steel" na "Collapse" vilipotolewa. Diamond huwa namsoma karibu kila akitoa kitabu.DHANA YA MALTHUS NA MLIPUKO WA KIJAMII KUTOKANA NA UWIANO USIO SAWA KATI YA IDADI YA WATU NA RASILIMALI.
Baada ya muda mrefu, hatimaye nimemaliza kusoma kitabu kiitwacho Collapse cha Jared Diamond. Katika kitabu hiki, Diamond anaelezea jamii mbalimbali zilizoshamiri na hatimaye kuanguka na baadhi zikisalimika. Anaposema kuanguka kwa jamii anamaanisha kushuka kwa kasi —na wakati mwingine kutoweka kabisa—kwa jamii kwa upande wa idadi ya watu, mifumo yake ya kiuchumi, kijamii na/au ya kisiasa. Zipo jamii za kale maarufu na kubwa zilizotoweka kama vile Maya, na zipo zilizoko kwenye hati hati ya kuanguka kama vile Haiti. Kwa ujumla wake Diamond anaelezea Sababu tano za jamii kuanguka [kwa kurejea historia]—au kwa maneno mengine huamua hatma ya jamii husika—ambazo ni matokeo ya shughuli za binadamu kwenye mazingira, mabadiliko ya tabia nchi, mahusiano na jamii jirani, madhara yatokanayo na uhasama wa jamii nyingine na muhimu ni nini jamii husika hufanya kupambana na matatizo yake.
Moja ya jamii iliyozungumziwa kwenye kitabu hiki Rwanda. Mwaka 1994, yafahamika kuwa Rwanda ilikumbwa na mauji makubwa, ikikisiwa watu Milioni Moja waliuwa. Na kwa kuwa mauji haya yalikuwa ni ya kimbari (racial killings), watusi wengi ndio waliouwa kwa kuwindwa na wahutu ikikisiwa watutsi 800,000 wakiuawa. Lakini pia wahutu takribani 200,000 waliuawa. Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa, ni mauji ya kimbari, basi watutsi waliuliwa na wahutu huku wahutu wakiuliwa na watutsi. Lakini, tafiti zinaonyesha kuwa wapo watutsi waliouawa wenyewe kwa wenyewe hali kadhalika wahutu wakiuawana wenyewe kwa wenyewe, mfano zipo jamii ambazo ni za wahutu pekee, lakini mauji yalikuwa 5% ya idadi ya watu. Kama ni mauji ya kikabila, mbona hapa hakukua na watutsi? . Ukisoma tafiti na takwimu, unaona kuwa licha ya kuwa ni kweli chuki za kimbari zilichochea na wanasiasa kuamua mauaji haya, lipo jambo jingine ambalo lilikuwa ni petrol kwenye moto huo wa chuki za kimbari—UHABA WA ARDHI.
Miaka ya 1700, mchumi wa kiingereza Thomas Malthus, alikuja na dhana inayoeleza kuwa, ukuaji wa idadi ya watu huwa na kasi kubwa (hujizidisha) kuliko ukuaji wa uzalishaji wa chakula (hujiongeza); hivyo kama hatua za makusudi —kama vile udhibiti wa uzalianaji—au za bila kutegemewa au bahati mbaya—kama majanga, vita au njaa— zisipotokea, basi itafika mahala kutatokea mlipuko mkubwa wa watu na hivyo kusababisha mnyukano mkubwa kwenye jamii husika. Mfano, kama ukuaji wa watu huongeza mara mbili kila baada ya miaka 30, hivyo, leo 2021 tutakuwa watanzania Mil 60, mwaka 2051 tutakuwa mil 120, 2081 tutakuwa Mil 240. Ukuaji mara mbili wa idadi ya watu, huchochea ukuaji la uzalishaji wa chakula kwa ongezeko, mfano leo wakati 2021 tuko Mil 60, na uzalishaji wa chakula ni Tani 50; 2051 tutakuwa mil 120 huku chakua kikiongezeka uzalishaji wa chakula kwa asilimia hivyo kuwa Tani Mil 75. Watu Mil 240, chakula itakuwa Mil 100. Na Sababu kuu ni kuwa ardhi haingezeki. Hivyo kwa mujibu wa dhana ya Malthus, jamii ikifika ongezeko la watu lisilowiana na ongezeko la uzalishaji wa chakula cha kutosheleza na hatimaye ardhi kuwa ndogo, kifuatacho ni mauji ya kugombea ardhi.
Rwanda na Msongamano wa watu; Kihistoria toka miaka ya 1800, Rwanda ni nchi iliyokuwa na msongamano mkubwa wa watu uliosababishwa na mvua nzuri kwa kilimo na ardhi yenye miinuko hivyo kutoathiriwa na mbu na mbung'o. Kwa wastani, idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa 3% kwa mwaka. Hata miaka ya 1990 baada ya mauji, bado Rwanda ilikuwa na Msongamano wa watu 760/Sq Mile ikiizidi Uingereza yenye 610/Sq Mile na ikiikaribia Uholanzi yenye 950/ Sq Mile, lakini Uingereza na Uholanzi zilikuwa na kilimo cha zana za kisasa ni watu wachache waliolima kinyume na Rwanda ambayo kilimo ni jembe la mkono, uzalishaji duni hivyo takribani kila mtu ilimpasa alime ili apate chakula.
—Hadi kufikia kipindi cha baada ya uhuru, ardhi yote ya Rwanda, nje ya ardhi ya hifadhi ilikuwa inalimwa—wapo walitania kuwa Rwanda ni kama bustani. Vita za mwaka 1960 na 70, zilipelekea watutsi kufa na wengi kukimbia nchi, hivyo kuwapa fursa wahutu kupata ardhi. Kilimo kiliendelea kuwa cha mkono, na kisochozingatia maeneo ya kulima, mfano milimani mazao yalizolewa na udongo sababu ya mmomonyoko. Miaka ya 1980 walishuhudia upungufu wa chakula kutokana na ukame, mbinu za hovyo za kilimo, mabadiliko ya tabia nchi na ukataji holela wa miti.
—Wanazuoni wa kibelgiji, Catherine André na Jean-Philippe Platteau, walifanya utafiti wao kwenye mji wa Kanama uliopo kaskazini magharibi mwa Rwanda kati ya miaka ya 1980 na 1993. Katika tafiti yao, walihoji wanyarwanda katika meneo matatu; Idadi ya wanakaya, ukubwa wa ardhi inayomilikiwa na kaya na utegemezi wa wanakaya kwenye kilimo na nje ya kilimo.
—Kijiografia, Kanama ni mji wenye ardhi yenye rutuba ya kivolcano, hivyo inafaa sana kwa kilimo na kupelekea kuwa na Msongamano mkubwa wa watu. Mf, 1988 ilikuwa na watu 1,740/Sq Mile na kufikia 2,040/Sq Mile mwaka 1993 [Ongezeko la asilimia 85. Ambayo ni sawa na shamba [kwa kila kaya] lenye ekari 0.89 mwaka 1988 na kushuka kufikia ekari 0.73 mwaka 1993. Ili kupata maeneo ya kulima, kwa wastani kila mkulima [mwanakaya] alilima ekari 0.09 mwaka 1988 na eneo kupungua kufikia 0.07 mwaka 1993.
—Sababu hakukua na ardhi tena, vijana [20-25s years] hawakuwa na uwezo wa kujitegemea kimaisha i.e kuoa, kupata ardhi na kulima. Mf, mwaka 1988 wasichana walioishi majumbani kwao walikuwa ni 39% na wavulana 71%, mwaka 1993 wasichana iliongezeka kufikia 67% huku wavulana ikiongezeka kufikia 100%. Maana yake mwaka 1993 hakuna kijana aliyeweza kuondoka kwao na kujitemea kwa sababu ya kutokuwa na ardhi.
—Hii tafsiri yake ni kuwa, wasichana na wavulana walirudi makwao, na kuepelekea idadi ya wanakaya kuwa kubwa na hivyo wengi zaidi kulima kwenye eneo dogo. Mf, mwaka 1988 kila kaya ilikuwa na watu wanaolima wa wastani wa 4.9 iliongezeka kufikia 5.3 mwaka 1993. Hivyo kiuhalisia Mwaka 1988 kila mwanakaya alilima ⅕ ya ekari, na kupungua hadi ⅐ ya ekari mwaka 1993. Hii ilikuwa na madhara hadi kwenye kiwango cha virutubisho walivyopata, ni 77% tu ya Calories walizopata ndio zilitoka shambani, zingine ilibidi wanunue chakula kutokana na kazi kama za kapenta, ufyatuaji tofali n.k. Mf watu wenye njaa i.e wanaopata chini ya Calories 1,600 kwa siku, walikuwa 9% mwaka 1992, na kuongezeka kufikia 40% mwaka 1993.
—Pia hali ya umiliki usio sawa wa mashamba—Shamba kubwa (zaidi ya ekari 2.5) na shamba dogo (chini ya ekari 0.6)— nao ulibadilika kadri miaka ilivyozidi kwenda. Mf mwaka 1988 mashamba madogo 7% hadi 40%. Maana yake ni kuwa, jamii za wakulima ziliongezeka matabaka, wachache wenye ardhi kubwa waliendelea, huku tabaka la kati likizidi kuwa na ardhi ndogo ndogo zaidi. Sababu kwa kaya masikini ardhi ilizidi kuwa ndogo, ililazimu kufanya kazi kwa wenye mashamba makubwa, hivyo masikini akizidi kuwa masikini na tajiri akizidi kuwa tajiri. Lakini, masikini waliuza sana ardhi zao ili kukidhi mahitaji kama afya, chakula, mashitaka, kupata fedha ya rushwa; huku tajiri huuza shamba ili kupata lenye faidia zaidi kama vile ukaribu.
—Kwa misingi hiyo, masikini walizidi kuwa masikini zaidi na frustrated, huku wachache wakiwa na utajiri zaidi huku wakiwa hawana frustration. Pia ilizaa tension ndani ya familia, mf binti anaposhindwa kuhudumiwa na mmewe, hurudi kwao hivyo kuongeza mzigo wa kulishwa, na pili wakaka huchukizwa pale anapokuwa na mtoto wa kiume—urithi. Hivyo, wajane, watoto wao iligeuka kuwa shida kuhudumiwa na familia zao. Pia ilileta tension kati ya mahusiano ya watoto na baba. Kimila baba akifariki, basi mtoto wake wa kwanza wa kiume hurithi. Kwa wasiwasi huu, baadhi ya wazee waligawa mali zao kwa watoto wote, ambayo nayo huzua migogoro mikubwa ya ndani ya familia. Na mauji yalipoanza yalitoa fursa kwa mauji ya familia.
Ukitazama wahanga wa mauji, mf eneo la Kanama, wanaangukia moja kati ya makundi haya sita.
i. Watutsi walioishi pekee yao au wajane. Sababu za kuuliwa yaweza kuwa ni ututsi, lakini ipo sababu nyingine. Mjane amerithi ardhi kubwa kutoka kwa mmewe, pia ameshiriki migogoro mingi ya ardhi, au pia mmewe alikuwa ni mhutu mwenye wake wengi.
ii. Kundi la pili ni wahutu wenye umiliki wa ardhi kubwa. Wengi wao hawa wana umri wa 50+. Hivyo ni kundi la kina baba. Watoto na wadogo zao walitaka ardhi.
iii. Pia wapo vijana waliomiliki ardhi kubwa mf kwa kurithi, hivyo waliwapa wivu vijana wenzao kuitaka ardhi yao.
iv. Kundi jingine ni wasumbufu wa migogoro ya ardhi. Hawa walikuwa ni wahutu walioshiriki migogoro mingi ya ardhi. Hivyo walikuwa kwenye chuki kubwa na makundi mengi.
v. Wahanga wengine ni wahutu ambao hawakuwa na ardhi. Hawa walijiunga na vikundi vya mauji kwa sababu ya kutokuwa na ardhi kabisa.
vi. Kundi la mwisho ni wahanga ambao walikuwa na hali ngumu za kimaisha sababu ya kutokuwa na chakula, pia walikuwa na ardhi ndogo au hawana kabisa kiasi cha kutokuwa na akiba ya chakula cha kuwawezesha kuhimili kipindi cha vita. Na wapo ambao hawakuwa na hela sababu ya kutokuwa na kazi kwa sababu walitegemea kufanya kazi za kuajiriwa nje ya mashamba.
“The 1994 events provided a unique opportunity to settle scores, or to reshuffle land properties, even among Hutu villagers . . . . It is not rare, even today, to hear Rwandans argue that a war is necessary to wipe out an excess of population and to bring numbers into line with the available land resources.” As Gérard Prunier, a French scholar of East Africa, puts it, “The decision to kill was of course made by politicians, for political reasons. But at least part of the reason why it was carried out so thoroughly by the ordinary rank-and-file peasants in their ingo [= family compound] was feeling that there were too many people on too little land, and that with a reduction in their numbers, there would be more for the survivors.”
Ukitazama tafiti hii, unaona suala la ardhi linavyochochea (kificho) ushiriki wa vijana kwenye vita au machafuko ya kisiasa. Turejee mfano wa Kenya mwaka 2007.
Cc: Red Giant Paula Paul Iceberg9 Kiranga
Mostly for beginners I think. They are easy to follow. Mimi nimesoma almost vitabu 50 vya James Hadley ChaseMwisho wake huwa si mzuri nimesoma kadhaa.
Msaada mwenye PDF ya hiki kitabu The race for Timbuktu search for the city of gold. Kimeandikwa na Frank .k. kyrzaSio vyote mkuu, nitafutie the impossible is possible by john Masson nikushukuru mpk kesho.
Cheki pdf drive huwezi kukikosa.Msaada mwenye PDF ya hiki kitabu The race for Timbuktu search for the city of gold. Kimeandikwa na Frank .k. kyrza
Aisee!!umekipa sifa hadi zimekinaisha.Nimesoma vitabu vingi ila 'Green eggs and ham' ya dr. Seuss Ni mwisho wa reli.
Yaani jamaa is very eloquent Na uandishi wake wakuu ...the best book ever..I mean the best FULLSTOP
Reading it is like walking in a reader's paradise....
It's pages are So smooth and wooly like royal sheets of old.
Perusing it's chapters is so pleasant like swimming in silver and gold.
Reading it's parts with conflict is very jaw dropping, like experiencing the chaos of a tornado brought by a million butterflies flapping their wings...
Reading Its resolutions is like massaging your eyes with soft buttery honey, whilst relaxing your train of thoughts in a garden swing where kids nearby with sweet lullabies sing..
It's characters are so mesmerizing, marvelous and Prodigious.
It's plot is so unique, so groundbreaking the most epic your eyes have ever seen,ears have ever heard and brains have ever grasped.
In short it is not the best book of this generation,century,era or even millennium.
It is the best book to ever exist and that will ever exist it is the best book of all eternity
Shukrani sana.View attachment 2009239View attachment 2009239
Hiki ni kitabu cha nne kukisoma kutoka kwa Jared Diamond [Guns, Germs and Steel —kitabu changu bora cha wakati wote—, Collapse, na Why Sex is Fun]. Katika vitabu vyake vyote, mambo matatu yanafanya vitabu vyake viwe bora katika Nonfiction authors; Moja vyanzo vyake vya taarifa viko wazi, pili mtiririko mzuri wa hoja zake na tatu umahiri wa kueleza mambo magumu katika namna nyepesi.
Tofauti na vitabu vyake vya awali, unaweza sema kitabu hiki ni uzoefu wake binafsi Diamond katika maeneo mbalimbali aliyotembelea na kufanya kazi mf New Guinea na Nchi za ulaya. Hivyo, mengi yaliyomo humu ni masimulizi binafsi (anecdotes) yakichagizwa na facts kutoka vyanzo mbalimbali.
Kitabu hiki kinasema nini. Katika kitabu hiki, Diamond anafanya ulinganisho wa nyanja mbalimbali za kimaisha—dini, siasa, uongozi, migogoro, familia, malezi ya wazee n.k—kati ya jamii ndogo ndogo/za asili na zile ambazo zimeendelea. Anaposema jamii za asili ni nini anamaanisha? Ukitazama historia ya Maendeleo ya dunia, maisha haya tuliyonayo leo sisi watu wa mjini, kwa kiasi kikubwa yameanza karne ya 19. Ni maisha yaliyoratibiwa na kupangwa. Mf, Chakula kiko sokoni, maji yanapatikana Dawasco, Matibabu yanapatikana Hospital, Migogoro inatatuliwa mahakamani, mawasiliano unapiga simu, Dawa zinapatikana duka la kuuza Dawa, Shule usafiri kijana anapanda school bus, ukipata ajali kuna bima, ukitaka taarifa kuna TV na simu. Haya ndio maisha ya jamii za kisasa. Lakini, kabla ya maisha haya (na baadhi ya sehemu hadi sasa) kulikuwa na maisha ya asili; Chakula ulihitaji kwenda Porini au lazima ulime, mawasiliano ulihitaji utembee au sasa hivi maeneo mengine utumie baiskeli au upande basi kwenda kupeleka taarifa, Dawa unahitaji uingie shambani ukachimbe mzizi, habari lazima uzungumze na jirani, migogoro ni mapigano au usuluhishi wa kijiji, maji unahitaji uende kisimani au mtoni ama ziwani. Maisha haya ndio mwanadamu ameyaishi hadi karne chache zilizopita (jana), lakini bado maisha haya jamii nyingi zinayaishi. Mf New Guinea kwa watu wa Fore alipoeleza Diamond. Lakini hata kwetu Tanzania, vijijini bado maisha haya yapo. Hakuna umeme, hakuna Dawsco, wakati mwingine mtandao wa simu hakuna, Zahanati iko moja nayo mganga wakati mwingine hayupo.
Hivyo, licha ya kuwa ni maisha tunayasema ya zamani [kwa baadhi yetu], lakini uhalisia ni kuwa ukitoka nje ya mijini au ukaondolewa mifumo hii, ni maisha ambayo unakutana nayo, hivyo ni muhimu sana kuyajua—ndio umuhimu wa kitabu hiki.
Ni kweli hatuwezi acha maisha haya ya kisasa na tuyarejee maisha ya asili. Lakini, yapo mambo mengi ambayo tunaweza jifunza kutoka kwenye jamii za asili na kisha kuyajumuisha kwenye maisha yetu ya usasa as a supplement kutokana na faida zake.
Kwa uchache haya ni mambo ambayo binafsi nimeyapenda kutoka kwenye jamii za asili [of course, yanaweza yakawa si mageni kwako, na mengine ninayaishi binafsi pia].
a. Mfumo wa Utatuzi wa migogoro. Jamii za asili ni jamii ambazo watu huishi kwa kufahamiana sana. Huyu anamjua yule au anamjua baba yake, au anajua kijiji anachotoka au ana imani kuna siku watakutana aidha kwenye biashara au mambo mengine. Hivyo hata migogoro inapotokea husuluishwa kwa muktadha wa kulinda mahusiano hayo. Mfano, maeneo mengi ya vijijini (mf New Guinea alipotolea mfano], anapoua mtu bila kukusudia na ikathibitika na kijiji, basi muhusika hulipa fidia kama njia ya kuonyesha maumivu yake kwa wahanga. Kwenye mifumo yetu ya kisasa mauji ya bila kukusudia, muhusika hufungwa. Na kesi nazo huchukua miaka mingi na gharama kubwa. Hivyo, bila shaka mfumo huu wa asili unaweza uchukua kama mtu binafsi katika kutatua migogoro binafsi na jamii zetu kwa ujumla.
b. Ulaji na Afya. Watu wa jamii za asili hula vyakula ambavyo havina sukari hatarishi, havina mafuta hatarishi. Hii huwaepusha na magonjwa kama ya kisukari na magonjwa ya moyo. Lakini pia mitindo yao ya maisha huwalinda pia—wanatembea sana, huendesha baiskeli, hulima kwa mkono n.k. Hii huwafanya wawe na miili imara, mikakamavu na yenye misuli. Kinyume kabisa na sisi watu wa jamii za kisasa.
Nina kijana mmoja ambaye amekuwa akiniletea maziwa nyumbani. kwa takribani miaka mitatu, amekua akitumia usafiri wa baiskel kuuza maziwa, akiendesha takribani Km 30 kila siku kuzunguka kusambaza maziwa. Mwaka huu mwezi April, alianza kutumia pikipiki kusambaza maziwa. Kimuonekano kwa sasa ameanza kutoka kitambi. Hivyo, a mere shift kutoka maisha ya 'asili' kwenda ya 'kisasa', huleta mabadiliko ya afya zetu wanadamu.
Kama nilivyosema hatuwezi acha maisha ya usasa na kurudi ya asili, lakini ni muhimu kuchukua ulaji wa asili ulio na faida zaidi kiafya na kufanya kazi za kutoa jasho/mazoezi/kuepuka magari isipolazimu ili kujiepusha zaiid na magonjwa.
c. Ujuzi wa lugha nyingi. Watoto wengi vijijini ni wajuzi wa lugha zaidi ya moja. faida yake kuu ni kuwa na wigo mpana wa mawasiliano na watu. Ni kweli tunaweza kuwa hatuhitaji kisukuma, kinyakyusa au kichaga leo kama ilivyokuwa kwa wazazi wetu. Lakini, umuhimu bado upo, tunahitaji kujua Kiarabu, kichina, kifaransa. Hivyo, kama wazazi ni muhimu kuwalea watoto wetu katika namna ambayo wanajifunza lugha nyingi kadri iwezekanavyo.
d. Mtazamo wenye uhalisia kuhusu dini. Ukizitazama jamii za asili hadi tulipo leo, dini zimekuwa zikibadilika kila muda na mazingira yalivyo badilika. Dini iliitikia mahitaji ya jamii Mfano, zipo jamii zilikuwa na Mungu wa mvua kwa sababu ya mahitaji yao ya ukulima . Hivyo kwa mtu ambaye anapata wakati mgumu kuhusiana na dini, ni vyema atambue na kuitazama dini kwa uhalisia zaidi.
Hayo ni machache kati ya mengi niliyoyachukua kwenye kitabu hiki. Nakusihi kisome.