Cmfungua
JF-Expert Member
- Jul 14, 2021
- 381
- 1,083
Aisee kitabu kitam sana hichi naweza kukisoma kila wakatNitakitafuta aise. Shukrani kwa kukitaja. View attachment 1864954View attachment 1864955
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee kitabu kitam sana hichi naweza kukisoma kila wakatNitakitafuta aise. Shukrani kwa kukitaja. View attachment 1864954View attachment 1864955
Sio vyote mkuu, nitafutie the impossible is possible by john Masson nikushukuru mpk kesho.Tumia website ya Zlibrary...nenda Books. Vyote utavipata hapo.
Mkuu hongera sana kwaNitumie namba nikutumie hicho kitabu unachotaka hapo juu alafu mimi nimetafsiri vitabu vingi sina
Vipo kwenye mfumo wa hard copy na soft copy
Ok nitumie namba yako ila kuna garama kidogo kumshika mkono natafsiriMkuu hongera sana kwa
Kutafsiri vitabu.
Binafsi ningependa kusoma vitabu
Ulivyotafsiri. Kama hutajali waweza kunitumia?
The monk who sold his Ferrari.Ok nitumie namba yako ila kuna garama kidogo kumshika mkono natafsiri
Kipo bossThe monk who sold his Ferrari.
Kweli Asante Sana kwa wazo zuri kwanza nitapiga pesa kupitia YouTube channelHongera innocent kwa kutafsiri vitabu. Tafadhali jiunge na TedX Talks zinazorushwa YouTube ili utafsiri zile video zao kwa Kiswahili. Zitasaidia SANA wa tu.
Bei gani kwa softcopy ya kiswahili.Kipo boss
Naweza kupata soft copy yake?Simba wa Tunduru. By B.Z Mkirya.
Uchambuz mzr sana mkuu, ningekuwa mpenzi wa siasa siasa ningefaidi sana bt ndo hvyo tena mm na siasa mbali mbali, tuchambulie na vya kina Robert kiyosaki, robin sharma, etc.Paula Paul nilikuwa impressed na idea yako ya kureview walau kitabu kimoja nilichosoma na kukipenda katika mwezi. I'm doing it now!.
Mwezi huu, nimesoma vitabu vitatu, viwili sikuvimaliza nadhani nitavisoma kwa muda mrefu zaidi, ila kimoja ndio nimekimaliza, nilipoanza sikutaka kukiweka chini. Hii hapa nimejaribu kufanya mapitio ya kitabu hicho.
Kitabu kinaitwa SECURING DEMOCRACY; MY FIGHT FOR PRESS FREEDOM AND JUSTICE IN BOLSONARO'S BRAZIL. cha GLEN GREENWARD.
Kitabu hiki kimetoka mwezi wa nne mwaka huu, 2021. Ukiniuliza nawezaje kukielezea kitabu hiki kwa sentensi moja, jibu langu ni hili; Jinsi gani vyombo vya haki vinaweza tumika kutimiza malengo ya kisiasa.
View attachment 1875113
View attachment 1875114
Mwaka 2014, wakati Edward Snowden anapuliza kipyenga na kuibua jinsi gani vyombo vya usalama vya Marekani (National Security Agency) na Uingereza Government Communications Headquarters (GCHQ) vinavyotumika, kinyume na sheria, kuwapeleleza raia wake, raia na viongozi wa nchi mbalimbali duniani, kama Brazil. Snowden, alipotaka kutoa habari hizi, alimtafuta Glenn Greenwald, aliyekuwa ni correspondent wa gazeti la the Guardian la Uingereza, mwaka 2013. Pengine swali, kwanini Greenwald?
Greenwald, ni Mmarekani, mwandishi wa Habari, ambaye kabla alikuwa na kampuni yake ya kisheria ambayo ilikuwa inajihusisha na mashtaka ambayo yamejikita kwenye haki zinazopatikana kutokana na mabadiliko ya kwanza ya katiba ya Marekani (First US Constitution Amendment, ya mwaka 1791, ambayo yaliweka masharti ambayo yanaikataza bunge la Marekani kutunga sheria ya kuanzisha dini maalumu ya taifa, au kutunga sheria itayozuia uhuru wa kuabudu, kuzuia uhuru wa maoni au habari; uhuru wa Wamerekani kukusanyika kwa amani). Baadae aliacha na kujikita kwenye uandishi wa habari ambao kimsingi ulikuwa ni zenye mlengo wa kupigania uhuru wa kisiasa, maoni na kuabudu. Kwa misingi hii, Snowden aliona huyu ni mtu sahihi, kumpa habari zake 'Snowden Files'. Mwaka 2014, alitoa kitabu kiitwacho No Place to Hide kuelezea mkasa mzima wa Snowden. Hapo ndipo nilipomfahamu na kuvutiwa sana na uandishi wake. Ambapo, kufuatia issue hii ya Snowden, ndipo ilipoanzishwa chombo cha Habari kiitwacho The Intercept, kikiwa na waandishi 'wa kweli' kama Jeremy Scahill, na Mehdi Hasan (kwa sasa hayupo), kikiwa na lengo la kufanya uandishi wa habari za Kichunguzi, bila kuwa na upande - Adversarial Journalism. Baada ya issue hii ya Snowden, Greenward alipata mtifuano mkubwa na serikali ya Uingereza na Marekani, na kuamua kusettle zaidi Brazil. Ambapo huko alianzisha tawi la intercept (Intercept Brazil). Na pia, alikutana na David Miranda na kufunga naye ndoa, in the course of life David, alikuja kuwa Diwani na hatimaye mbunge nchini Brazil.
Mwaka 2018, aliunganishwa na rafiki yake, Mbunge aitwaye Manuela, kuwa kuna mtu amehack mawasiliano ya mtandao wa Telegram (uliokuwa ukitumiwa na kuaminiwa na vigogo wa Brazil kuwa hauwezi kiwa hacked) ya mawaziri wa masuala ya katiba ya Brazil, Sergio Moro na Mwendesha Mashtaka Deltan Dellagnol. Katika Mawasiliano hayo ya zaidi ya miaka mitano, yanaonyesha ni jinsi gani, Moro na Dellagnol walivyokuwa wakiendesha operation kubwa katika historia ya Brazil, ya kupambana na rushwa iliyoitwa Operation Car wash. Uvujishaji huu, ni wa muhimu sana, sababu umetoa elimu na onyo kubwa sana kwenye jamii, juu ya tahadhari inapokuja suala la vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa masuala ya Rushwa au madawa ya kulevya n.k!
Brazili ni nchi ambayo kwa sababu za kihistoria (ukoloni), na baadae miaka ya 1960 , kuchangiwa na Marekani kufanya mapinduzi nchini humo na kuweka utawala wake, wa chama kimoja, wa kidikteta na kijeshi, ulifanyw tabaka la weupe ambao ni wachache kuwa ndio wamiliki wa kila kitu nchini humo, siasa, uchumi, biashara, vyombo vya habari, vyombo vya dola na mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya. Wasio weupe (non-whites) ambao ndio wengi ni tabaka tawaliwa kwa miaka mingi. Kutokana na misingi ya utawala wa kijeshi, udiktea, maisha ya Brazil katika nyanja zote yametawaliwa na ubabe na rushwa katika kila eneo. Hali hii ilipotamalaki, wabrazil walichoshwa na tabaka la watawala - elite establishment. Na yeyote ambaye alikuwa akihubiri na kupambana na tabaka hilo, wabrazil walimuhusudu na kumpa support mtu huyo.
Falsafa hii ya kisiasa, ndio iliwatawala wabrazil; 'Anyone who is hated by the political system that we despise and the elites who control it, and who promises to burn it and them down to the ground, is on our side.'
Ndipo ilipotokea mwaka 2014, ilipoanzishwa Operesheni ya kupambana na wala rushwa, wakwepa kodi na watakatishaji fedha. Chini ya aliyekuwa Jaji katika mji wa Curitiba, Sergio Moro, (Jaji wa mahakama hii, unaweza mfananisha na Hakimu katika mahakama ya Kisutu hapa nchini kwetu kutokana na unyeti wa kesi zinazopelekwa pale). Kiongozi wa Operesheni hii alikuwa ni Mwendesha Mashtaka Deltan Dellagnol, na iliitwa Operation Car wash [emoji3]. Mamia ya watu walikamatwa, Mamilioni ya dola zililipwa mfano wakuu wa Shirika la mafuta Brazil, Petrobas walilipa takribani $ Mil 700, vigogo walifungwa, na hatimaye kigogo mkubwa zaidi alifungwa, Luiz Inácio Lula da Silva. Huyu alikuwa Rais wa Brazil mwaka 2003 hadi mwaka 2010. Wananchi waliiunga mkono Operesheni hii sababu 'maadui zao'-wala rushwa walikuwa wanaburuzwa mahakamani na Jaji Moro alikuwa ni shujaa wa taifa na 'Mungu Mtu'-kwa lugha yetu, tungesema aliupiga Mwingi.
Kwa sura ya nje, Operesheni hii, ilikuwa ni jambo la kitakatifu. Lakini, ambacho wabrazil hawakujua ni kuwa, hii ilikuwa ni harakati ya kisiasa, ya kumzuia Rais Mstaafu Lula, asiweze gombea uchaguzi wa 2018-ambaye ndiye alikuwa na 'uhakika' wa kushina na chama chake cha Mrengo wa kushoto cha Workers Party. Kufungwa kwake, kulimpa nafasi Jairo Bolsonaro, ambaye chama chake hakikuwa na nguvu, ambaye kihulka ni dikteta mwenye siasa kali za mrengo wa kulia. It went right, Bolsonaro mwaka 2019 alishinda Urais wa Brazil.
View attachment 1875118
Alipoingia Madarakani Bolsonaro, mwaka 2019, alimpa Moro nafasi ya waziri wa katiba na Usalama wa Taifa. Huyu ndiye alikuwa waziri, pengine, mtu mwenye mamlaka na wa kutisha zaidi brazil, sababu ya vyombo vilivyokuwa chini yake. Investigation, law enforcement, policing, domestic intelligence, financial monitoring, and electronic surveillance.
View attachment 1875125
Wakati nasoma kitabu hiki, nilipata mawazo pia, kama nia ilikuwa ni ya kisiasa, haiathiri ukweli kuwa walifanya makosa ya rushwa, seems I was too quick to conclude. Faili alizozitoa mdukuzi huyu kwa Greenwald, ziliibua mambo yafuatayo;
1. Dallagnol alikamata 'vidagaa' ambao walishinikizwa kutoa ushahidi dhidi ya Vigogo, ambao hatimaye walitiwa hatiani. Mfano, Vigogo wa Shirika la Petrobas.
2. Mwendesha Mashtaka (MM) na Jaji walishirikiana kuandaa Ushahidi dhidi ya washatakiwa ambao waliwalenga, na hatimaye jaji mwenyewe kuwafunga.
3. Tatu, walighushi nyaraka ambazo ziliwasilishwa kama ushahidi wa mashtaka.
4. MM na jaji walitengeneza jumbe za kughushi kwa lengo la kumchafua Rais Lula.
5. MM aliharibu ushahidi ambao ungetumiwa na washtakiwa kwenye utetezi wao.
6. MM na jaji walikuwa na mawasiliano wakati wote juu mwendendo wa kesi ambao ni kinyume na Sheria na maadili ya majaji.
Kimsingi, Jaji Moro hakuwa tu anashirikiana na Mwendesha Mashtaka, bali yeye ndiye alikuwa kiongozi, Bosi na Mchora mipango mkuu, wa kuwatia hatiani vigogo ambao mwishoni watamtia hatiani Lula; walifanikiwa. Na hatimaye Lula alifungwa miaka 9. Maana yake hakuweza shiriki uchaguzi, na lengo kuu la kisiasa lilifanikiwa- Bolsonaro alishinda Urais.
Ukipause hapa ukavuta kumbukumbu na kutafakari, unaweza kuona ni jinsi gani hata hapa nchini mwetu, yapo mashataka au Operesheni ambazo licha ya kuonekana zinafanya jambo sahihi lakini zimekuwa na malengo ya kisiasa nyuma yake-hii kwa nchini mwetu iko hasa ndani ya Chama Tawala, si kwa sababu wapinzani ni 'Malaika', bali hawana resources za kufanikisha.
Kisheria, jaji anapaswa awe huru na asiwe na upande wowote (When the judge loses impartiality, he ceases to be a judge.). Pili, Mashtaka yanapaswa yasaidiwe na ushahidi ambao haupaswi kuwa wa kughushi, udanganyifu au umepatikana kwa shurti. Haya yote ukiyaweka kwenye Muktadha unaona kuwa Operesheni hii, ilikuwa ni batili na waliofungea hawakufungwa kihalali. Na ilipaswa punde baada ya taarifa hii kutika, Moro kama waziri alipaswa kuwa amejiuzuru na kushtakiwa. Lakini kwa Brazil ni tofauti, a mafia state. Greenwald alipata mashambulizi ya kila namna, kutoka kwenye Serikali ya Rais Bolsonaro, Bolsonaro mwenyewe, wanaye ambao ni viongozi wakubwa wa kisiasa na propagandists wake, Waziri moro mwenyewe na vyombo vyake anavyo viongoza. Ilichukua zaidi ya mwaka, ndipo Moro alipojiuzuru (kutokana kuibuka hali ya kutiaminiana kisiasa kati yake na Rais Bolsonaro) na na Dellagnol (akitoa sababu ya afya ya familia yake).
Kwenye kitabu hiki, kuna mafunzo mawili makubwa, ambayo yote mawili ni tadhali/angalizo.
1. Operesheni zinazofanywa na vyombo vya dola, zinapswa sana kuwa na mazingira ya kuweza kumulikwa, ili kuhakikisha utii wa sheria.
2. Jamii, inapokuwa ina kiu kubwa ya mabadiliko, inahitaji iwe makini, sababu kuna uwezekano mkubwa wa harakati za kisiasa kutumia fursa hiyo kutimiza azma za kisiasa-madaraka.
Haki huchelewa, lakini baadae hupatikana, Rais Lula alitumia mwaka mmoja na nusu gerezani, na baadae mahakama kumuachia huru.
Nakusihi kisome kitabu hiki katika sura zake zote 9, kina mafunzo makubwa kuhusu mazingira ya uhuru wa vyombo vya habari duniani hasa nchi za Uingereza, Marekani na Brazil, Historia ya Brazil kisiasa-hada jinsi gani Marekani alivyosaidia kuwekwa misingi ya udikteta, ukatili, kutokuheshimu sheria (Sura ya 2), hali ya sasa ya kisiasa na kijamii ya Brazil chini ya Rais Bolsonaro na kumfahamu yeye mwenyewe binafsi (sura ya 5). Ila kama una 75% ya muda wako, basi soma Sura ya Tatu, ya nne, ya sita na ya saba (ambazo ndio hasa zimeelezea kuhusu Ubakaji huu wa misingi ya haki). Kama Una 50% ya muda wako, basi soma sura ya tatu ja ya sita. Kama una muda mchache zaidi, na unataka kupata picha ya jumla, lakini inayojitosheleza, basi soma sehemu ya Utangulizi (Preface), ametoa summary ambayo imeelezea maudhui na story yote kwenye sakata hili. Ila kwa ujumla, ni kitabu chepesi kusoma, kina kurasa 280 tu, na kilivyoandikwa, ni kama unatazama filamu ya kusisimua ya kipelelezi kuhusu siasa.
Red Giant I hope you will this too!
Shukrani mkuu. It's an irony, unaitwa Vladimir Lenin na hupendi siasa[emoji3]Uchambuz mzr sana mkuu, ningekuwa mpenzi wa siasa siasa ningefaidi sana bt ndo hvyo tena mm na siasa mbali mbali, tuchambulie na vya kina Robert kiyosaki, robin sharma, etc.
[emoji2] [emoji2] najikuta namkubali tu hyu mwamba, plus kim jong, siasa ya tanzania imenifanya niichukie siasa kwa ujumla wake.Shukrani mkuu. It's an irony, unaitwa Vladimir Lenin na hupendi siasa[emoji3]
Sasa,have you pursued any of those?Things fall apart
The river between
Mine boy
No longer at ease......
Nakumbuka nilikuwa napenda sana Literature. Siku moja nikamfuata mwalimu kumuuliza 'What career should I pursue?' akanijibu nakuona kuwa mkalimani au mkutubi. Dah!