Hiki si katika vitabu vyangu bora vya muda wote,ila nawashauri baadhi ya watu,hasa Atheists wakisome kwa kutafakari. Maana kuna kusoma na kusoma kwa kutafakari.
View attachment 1866948
Vifuatavyo ni katika vitabu vyangu vya muda wote (hapa nimekiondoa kile kitabu cha imani yangu sababu hiki ni maalum,kadhalika vitabu vilivyo kusanya maneno,vitendo vya Mtume wangu sababu hivi ni katika ufunuo kadhalika),nitakavyo vitaja hapa ni katika vile ambavyo kuna viumbe Mola wetu aliwapa elimu na uandishi, sababu wapo walio pewa elimu lakini hawakuwa waandishi,yaani hawakuandika.
1. Ibn Taymiyyah against Greek Logicians.
Hiki kitabu msingi wake kuwakosoa au kuikosoa logic (Mantiki) kama elimu pweke iliyo asisiwa na kina Aristoto na Plato. Kwa kujenga na ukosoaji hiki ni kitabu bora kwangu.
Kimenifunza ya kuwa si lazima uwe Mwanafalsafa au usome falsafa ndiyo uwe bingwa wa kuhoji au kuuliza maswali fikirishi.
Ukipata kitabu hiki kwa lugha yake ya asili yaani Kiarabu ni bora zaidi,kwa Kiarabu kinaitwa "Nasihat alhlul Imaan fi raddi al Mantiq al Yunaaniy"
2. Incoherence of the Philosophers
Muandishi wa kitabu hiki anaitwa Abul Hamiid al Ghazali,mtu huyu alikuwa mjuzi wa mijadala na kujenga hoja,zama zake aliifanya Falsafa ya Kiyunani ionekane kama elimu ya watu wajinga wasio kuwa na akili. Ilifikia kipindi zama zake ukitaka kutolea mfano juu ya ujinga au wajinga basi ni Wanafalsafa,hakika alifanya kazi kubwa sana.
Kimenifunza mengi sana kitabu hiki.
3. The Soul
Muandishi wa kitabu hiki anaitwa Ibn al Qayyim al Jawziyyah.
Kupitia kitabu hiki nimejifunza ya kuwa Roho haifi,bali Roho ni katika kiimbe chenye mwanzo ila hakina mwisho.
Kwa leo nakomea hapa.