Vitambulisho vya kitaifa vinavyotumika kama sehemu ya siasa na kampeni

Vitambulisho vya kitaifa vinavyotumika kama sehemu ya siasa na kampeni

markp

Senior Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
199
Reaction score
333
Ni aibu sana kwa Taifa la Tanzania kutumia vitambulisha vya taifa vinavyosimamiwa na nida kama sehemu ya siasa, watu wanaenda kujiandikisha wanaambiwa wakachukue number ya kitambulisho baada ya wiki 2, ukienda kuchukua number unapewa bila tatizo, tatizo linakuja kupata kitambulisho sasa, hata hao wanaotoa huduma hawajui ni lini watakupa kitambulisho chako kana kwamba kuna nchi nyingine tofauti na Tanzania ndio inatengeneza, yaani kupata kitambulisho imekuwa kama jambo la kumshukuru Mungu na ni bonge la bahati.

Kwanini nasema vinatumika kisiasa:
Mheshimiwa Magufuli alipokuwa kwenye safari ya kwenda Dodoma alipita Morogoro na alipofika Msamvu alisimamishwa na wananchi ili waongee nae wakamwambia kero yao ya vitambulisho palepale mzee wa masifa akampigia simu mkurugenzi wa NIDA kwanini mpaka sasa hajawapa wananchi wa Moro na wengine vitambulisho vyao na ni zaidi ya mwaka umepita? mkurugenzi akafanya kama anajiumauma akasema itafanyiwa kazi, KESHO YAKE WATU WANAPEWA VITAMBULISHO KUTOKA KWENYE MABOKSI.

HIVI KWELI KAMA VITAMBULISHO VILIKUWEPO KILIKUWA KINASUBIRIWA NINI KUGAWA TIU NI MPAKA RAIS ASEME? HIZI SIO SIASA? NA KAMA NI SIASA MBONA NI SIASA MBOVU ZAIDI ZA KUWATESA WANANCHI?

BAADA YA KUGAWA MORO NIKAFIKIRI NA MIKOA MINGINE WATAGAWA HA HA HA HA MPAKA WA LEO (kama kiswahili cha watu fulani) HAKUNA CHA KITAMBULISHO NI MWENDO WA NUMBER TU.

HAKUNA WA KUMUULIZA WALA KUMLALAMIKIA.
SASA SERIKALI ENDELEENI KUFANYA KAMPENI NA SIASA ZA KIJINGA MADHARA YAKE MTAYAONA , MNAWAFUNDISHA WANANCHI MAMBO AMBAYO WALIKUWA HAWAJUI NA YATAWASAIDIA MBELE YA SAFARI. UKATILI WENU NI KAMA SHAHADA YA KWANZA KWAO.
 
Sasa mkuu kama no. za ID unazo kwa nini uangaike na kitu ambacho unajua hakuna kiwanda cha kukitengeneza
 
Back
Top Bottom