Vitambulisho vya machinga ulikuwa mradi wa nani? Kwanini ile hela haikukusanywa na TRA?

Vitambulisho vya machinga ulikuwa mradi wa nani? Kwanini ile hela haikukusanywa na TRA?

kagoshima

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
2,887
Reaction score
5,687
Za asubuhi wadau,

Uongozi wa hayati ulikua na mambo mengi yenye ukakasi. Mojawapo ni hili la kuwauzia wamachinga kitambulisho kisicho na utambulisho wowote wa anaye kimiliki.

Manaake kitambulisho kingeweza kudondoka na kikaokotwa na kutumiwa na mtu mwingine.

La kushangaza zaidi malipo ya hivi kitambulisho hayakuwa na risiti na makusanyo hayakufanywa na TRA.

Kuna kipindi nguvu flani ilitumika kulazimisha machinga, mamantilie, waosha magari, washona viatu kuwa na hivi vitambulisho.

Kibaya zaidi haijulikani hi biashara ilianzishwa kwa madhumni gani. Je, ni biashara ilikua inafanywa na mtu pale state house. Ile hela ilienda kufanya nini, kuna taarifa ya mapato na matumizi.

Je, yale makusanyo yapo kwenye sheria ya kodi. Je, ulikuwa ni ufisadi unafanyika pale mahala patakaifu?
 
"Hii nchi imechezewa sana ndugu zangu, wapinzani wametuchelewesha sana jamani.

Machinga wanyonge wasibugudhiwe-natoa vibali mtu asiwasumbuae."

Baada ya muda "nimekusanya milioni 800 kutokana na mradi wa vitambulisho vya machinga-mawaziri wangu muwe wabunifu pesa ipo-nchi hii ni tajiri sana".

MAENDELEO HAYANA VYAMA-CCM HOYEEEEEEE
 
TRA walipewa hiyo kazi tangia 2016 mpaka 2018 hawakuwa wamefanya lolote kila siku wako kwenye Tathimini ikabidi Mh Rais kwa kipindi icho aibuke na wazo lake akatoka kitambulisho cha mjasiliamali na kikapokelewa vyema tu!

Kwakuwa nchi ina mapato yanayokana na kodi na yasiyotokana na Kodi basi Fedha iliyopatika kwa vitambulisho vya Machinga ilikuwa na Mapato tasiyotokana na Kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwa mchango kama ilivyo michango mingine isiyokuwa na sheria yoyote ya kiundeshaji; mara nyingi michango ya aina hii ni miradi ya Chama kama ule wa kukimbiza "mwenge wa uhuru" sidhani kama inakatiwaga risiti. Wanufaika ni Chama na magenge yake!
Ndiyo maana CCM inazidi kuwa na mikwanja mingi kisa hivi visera vyao
 
TRA walipewa hiyo kazi tangia 2016 mpaka 2018 hawakuwa wamefanya lolote kila siku wako kwenye Tathimini ikabidi Mh Rais kwa kipindi icho aibuke na wazo lake akatoka kitambulisho cha mjasiliamali na kikapokelewa vyema tu.! Kwakuwa nchi ina mapato yanayokana na kodi na yasiyotokana na Kodi basi Fedha iliyopatika kwa vitambulisho vya Machinga ilikuwa na Mapato tasiyotokana na Kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kilipokelewa vizuri? Are you serious on this point?

Hebu eleza tukuelewe unamaanisha nini.
 
Back
Top Bottom