Vitambulisho vya machinga ulikuwa mradi wa nani? Kwanini ile hela haikukusanywa na TRA?

Vitambulisho vya machinga ulikuwa mradi wa nani? Kwanini ile hela haikukusanywa na TRA?

Tanzania Ni Tajiri
Tuchelewa Sana Ndugu Zangu
Tumeliwa Sana Ndugu Zangu
Tumelaliwa Sana Ndugu Zangu
Tumehomolwa Sana Ndugu Zangu



Pesa Zipo Nchi Hii,Mambo Ya Michakato Sitaki Kwenye Serikali Ninayoiongoza. Wewe Waziri Wa Afya Sitaki Kusikia Mambo Ya Uzazi Wa Mpango



Watu Wazaane
 
Za asubuhi wadau,

Uongozi wa hayati ulikua na mambo mengi yenye ukakasi. Mojawapo ni hili la kuwauzia wamachinga kitambulisho kisicho na utambulisho wowote wa anaye kimiliki.

Manaake kitambulisho kingeweza kudondoka na kikaokotwa na kutumiwa na mtu mwingine.

La kushangaza zaidi malipo ya hivi kitambulisho hayakuwa na risiti na makusanyo hayakufanywa na TRA.

Kuna kipindi nguvu flani ilitumika kulazimisha machinga, mamantilie, waosha magari, washona viatu kuwa na hivi vitambulisho.

Kibaya zaidi haijulikani hi biashara ilianzishwa kwa madhumni gani. Je, ni biashara ilikua inafanywa na mtu pale state house. Ile hela ilienda kufanya nini, kuna taarifa ya mapato na matumizi.

Je, yale makusanyo yapo kwenye sheria ya kodi. Je, ulikuwa ni ufisadi unafanyika pale mahala patakaifu?
Machinga leo hawaamini wanachokiona
 
Back
Top Bottom