Vitambulisho vya Taifa: Maoni ya Mchungaji




Ukichukua the thread yenyewe uchanganye na the above maelezo - yamejitosheleza kabisa.
 
mawazo mgando,hivi unajua maana ya database?
 
Naomba mfano Wa nchi iliyounganisha Hivi vyote ndio nitachangia hoja..,


Itakusaidia vipi kutoa mawazo yako ambayo yanatakiwa kuwa huru kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo vya nchi hii? Ama umegubikwa na ulimbukeni wa kufuata mzoga au huna upeo chanya wa kufanya hivyo.
 
Sasa kama hili wazo lako sio sahihi kwanini asitokee mtu akalipinga!!!? ...na kama ni sahihi ni kwa lisifikiriwe katika utekelezaji!? Je itakuwa sawa kukiri kuwa nchi sasa ina 'wafikiriaji (thinkers)' wasio na maamuzi au ina 'Waamuzi wasio fikiri'???
 
Naomba mfano Wa nchi iliyounganisha Hivi vyote ndio nitachangia hoja..,
haya mambo niyo maana yameletwa jamvini hapa kuangalia kama kweli na sisi kama Watanzania tuna la kuweza kufikifri wenyewe badala ya kuangalia yaliyofanyika kwingine. Angalia uhalisia wa mawazo!
 
ukiangalia pia kiasi cha fedha kinachokusudiwa kutumika na kutokana na uzoefu tulioupata, nadhani wengi tukisoma repoti ya bunge juu ya RICHMOND na jinsi wahusika walivyokuwa wakifuatilia usiku na mchana ungedhani kweli wana nia ya dhati kumaliza mgao wa umeme Tanzania, tuliona tulipoishia. Kuna haja ya kurejea huko!??
 
Wasomi tunajua kinachoendelea kwa hiyo inabidi tuwaelimishe wananchi tu.......
 

Weeee Mzalendo kweli? Mtoa hoja hajakataa vitambulisho ila jinsi ya kuvipata kwa kuwa kuna data base nyiingi na taasisi nyiingi ambazo hakuna hata moja inayofanya kazi zake kwa asilimia mia kila taasisi inagusagusa tu kwa hiyo akapendekeza iwe moja. Sasa wewe unataka watu wahame nchi unataka uishi peke yako?
 

hapo umezungumzia vitu vingi sana,ungejaribu kuweka bayana nia yako.wizi wa kura basiiiiiiiiii.
 
Kweli kabisa, naunga mkono, hizo pesa wamepewa hao wanunue vifaa kisha wapeleke kwao. kwa Mtanzania mpaka leo hawazi kutengeza kitambulisho? kama vipi wamkodi mtaalamu, kama Zanzibar wameomba msaada Israel, na wametumia Technology ya Israel kutengeneza vitambulisho ya Mzanzibari, nashangaa sisi bara kukabidhiwa walima minazi wa Malaysia, au kiji rangi tu kinachomata?
 
Mzalendo unatakiwa uwe kidogo makini unapochangia mada. Hakuna mtu aliyekataa kuwa vitambulisho sio muhimu, ila mchakato wake uende vipi ilhali kuna taasisi zingine zinafanya kazi kama hio, na ziko well equiped with personal information, and overall security ya watu binafsi.

'Heri akunyimae pesa, kuliko Akili'
 
Angalia

Ukitaka cheti cha kuzaliwa mlolong unaopitia

  • upite kwa balozi sijui wakili au mahakami.. .....ok umepita mlolongo huo umepata cheti cha kuzaliwa

Siku ukitaka passport hata kama una cheti za kuzaliwa vile vile

  • Unatakiwa uende mahakamani au upite kwa wakili, baalozi. Hata kama una kitambulisho cha mpiga kura ni kazi bure

Sasa ngoja ngoja mje msikie utaratibu wa kupata kitambulisho cha taifa..hata kama una passport utaambiwa anzia kwa balozi. au nenda kwa wakili. Hii vitu kama viko disjointed havina maana. na watu wanaposema ukritimba ndo mambo ama haya Ma system kibao lakini mtu unazungushwa.

Yaani system za serikali zenyewe haziaminiani. Kuna haja gani ya kutumia gharama kubwa kuwa na haya mambo. kama hayarahisishi utendaji. Kitambulisho cha taifa ni kizuri ilaaaa...................

Mfano mwingine ndio maan Kutoa mizigo bandari ya Dar inachukua siku mbili zaidi ya kutoa mzigo huo huo Mombasa. Sijui TRA sijui TICS. Ndo mambo haya haya. Kila bosi anataka aweke singature
 

Hata kama humkubali Jk ila tambua kuwa he is entitled to be called Dr kwa kupewa Honorary DOctorate na vyuo mbalimbali.
Kama umebahatika kupitia chuo utakuwa wajua hili na nimeona nikuambie tu japo si sehemu ya mjadalia.
unaposema vitatumika hadi bank ina maana kadi za bank hazitatumika tena au? una uhakika na hili?
Nijuavyo mie ni kwamba vitambulisho vya taifa ni vya msingi sana na lazima viwe na ubora zaidi ya vitambulisho vya mpiga kura.
 
Great thinkers tumekuwa tukiambiwa kuwa tunapenda kulaumu kwa kiasi kikubwa pale tatizo linapotokea lakini kwa kiasi kidogo hutahadharisha pale tunapoona tatizo linaweza kutokea. Ingawaje ukisoma threads zote utaona maonyo mengi tu ambayo hutolewa kwenye jukwaa hili, ila kwa kuwa kazi yetu ni kusema, wahusika wanaona hatuwezi kuwafanya lolote.

Sasa mimi kama mmoja wa great thinkers ninaanza kutoa tahadhari mapema kabisa.

Tanzania yetu kwa sasa ina utata hasa katika muundo wa serikali yake ya Muungano. Wenzetu wa Zanzibar wameweka bayana kupitia njia mbalimbali kuwa hawakubaliani na muundo wa muungano ulivyo. Wanapendekeza Kuwa iwepo serikali ya Zanziba , ya Tanganyika na ya Muungano. Kwa hali hii wanataka Zanzibar itambulike kama nchi inayojitegemea yaani Taifa huru.

Wakati huohuo nchi iko fasta inataka kutengeneza vitambulisho vya utaifa kwa billioni nyingi zaidi ya 220. Je vitambulisho hivyo ni vya watu wa namna gani? Watanzania wa Zanzibar wanaodai kuwa na nchi huru si watataka kuwa na vya kwao. Je kwenye bajeti ya sasa ya hivyo vitambulisho si na wao wapo? Je muundo wa vitambulisho umekaaje na vinawatambulishaje watu wa bara na wa Visiwani.

Wasiwasi wangu ni kwamba tutaingia hasara kutengeneza vitambulisho vingi ambavyo bila kufikia muafaka utambulisho tutakao kuwa nao utakuwa umebadilika na kuifanya serikali itengeneze vipya. Hivyo Muafaka juu ya suala la muungano ufikiwe mapema kama vitengenezwe vya Tanganyika tuu, ili wenzetu nao watengeneze vya Taifa la Zanzibar. La sivyo utakuwa mwanya wa mafisadi kuchanganya hesabu kwa kusema kuwa vitambulisho vimekosewa. Waulizeni wanaoulalamikia muungano wanataka vitambulisho viwatambue kwa utaifa upi? Watanzania, Wazanzibari au Watanganyika?

Kwa mwenye fikra za karibu ataona hii haina tatizo ila Watanzania wenzangu fuatilieni ili muone watu wanalichukuliaje. Tahadhari tumetoa mapema. Tatizo litakalotokea sababu ya uzembe wa haya tutaendelea kukosoa na kulaumu maana tumeeleza mapema.

Mungu ibariki Tanzania
 
Watu wameshapiga hesabu zao. Vitengenezwe alafu ionekane havikidhi wananchi wote wa Muungano , mfarakano utokeee, watu wale tender mara mbilimbili. Hatukubali.
 
Kwanza tunataka tanganyika ndipo tuhitaji vitambulisho vya nchi yetu.
Mimi siijui tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…