[font="]ndugu wanajamvi,
[/font]
[font="]
[/font]
[font="]kwa heshima kubwa napenda kuwasilisha hii hoja ili tuone inaweza kutusaidia vipi kupinga hii project ya vitambulisho vya taifa, msijali tuna nguvu kiasi gani maana saddam, mubarak, mobutu, n.k. Walionekana giants pia! Nadhani wanajamvi wengine wamesha post juu ya hili swala ila kutokana na umuhimu wake kwa taifa nakuja nalo tena.
[/font]
[font="]
fikiria haya yafuatayo:
mpaka sasa kuna vitambulisho vifutavyo kutoka serikalini/taasisi za serikali:[/font]
- [font="]tin certificate (inatolewa na tra)[/font][font="][/font]
- [font="]birth certificate (inatolewa na rita)[/font][font="][/font]
- [font="]passport (inatolewa na immigration/mambo ya ndani)[/font][font="][/font]
- [font="]voter registration card (inatolewa na tume ya uchaguzi)[/font][font="][/font]
- [font="]driving license (inatolewa na traffic police/mambo ya ndani)[/font][font="][/font]
- [font="]...nk[/font][font="][/font]
- [font="]...nk[/font][font="][/font]
[font="]mpaka sasa si tra au wizara ya mambo ya ndani ambayo database yake inahifadhi nusu ya watanzania, zote zina data kidogo sana na labda sizizo sahihi. Ukienda kuomba passport unatakiwa kutoa cheti cha kuzaliwa, tin unaombwa kitambulisho (sijui kipi!!) nk ila cha msingi hapa particulars la kila kitambulisho ni zile zile!
Kwa mfano, nimesoma habari inayohusu shirika la misaada la japan (jica) kutoa angalizo na maoni yake juu ya nini kinasababisha foleni jijini dar es salaam: Walioiona hiyo habari ni kuwa ziko taasisi karibia(zaidi) ya 15 zinazoshigulika na kitu kimoja - usafiri wa jiji!!! ...ambazo kutokana na maamuzi yao kutofautiana yameishia kuongeza ukubwa wa tatizo badala ya kupunguza. Wakashauri iwepo mamlaka moja tu yenye maamuzi.
kwa vile mradi huu wa vitambulisho unatiliwa mashaka na wengi, na kwa vile siku za nyuma mheshimiwa raisi wetu mpendwa sana dokta jakaya mrisho kikwete alishasema kuwa anajenga uwezo (capacity building) kwa kuelekeza nguvu kwenye kuimarisha taasisi, basi ni kwa nini hizo us $230m zinazotolewa kwa kazi hii zisiwekwe kwenye taasisi ambazo zipo tayari na zina mtandao mzuri badala ya kuanzisha mpya!!?
hii inaweza kulisaidia taifa kwenye mipango yake ya maendeleo na kuwa na 'a strong and reliable database' inayoweza kuondoa utata wa kuambiwa kuwa kuna wapiga kura milioni 22 lakini wakajitokeza milioni 7! Lakini kikubwa zaidi ni duplication of works and repetitions!
my take:
taasisi ya vizazi na vifo (registration, insolvency and trusteeship agency - rita) inaonekana ndiyo kiuhakika inahusika na kila mtanzania na ni ya kudumu (maana passport ni kwa wasafiri, leseni ni madereva, tin ni biashara, mpiga kura nk) ipewe hizo pesa ili waimarishe uwezo wao (database na administrative issues) badala ya kuzitupa "motoni"!?
(naomba kukosolewa)
nawasilisha[/font]