salisalum
JF-Expert Member
- Oct 27, 2010
- 423
- 140
Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, 1964. Haijalishi ziliunganaje cha muhimu ziliungana ikawa nchi moja full stop. Hatuwezi kila kizazi kingine kikija tunapangua taifa letu. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na Tanganyika ilikufa mwaka 1964 kwa utashi wa raia wa Tanganyika, wakati huo wakiwa karibu million 10 na Wazanzibari laki 3.
Kile walichofanya Zanzibar katika katiba yao waliyopitisha juzi ni uhaini na uhuni. Na inatakiwa wale waliosababisha wachukuliwe hatua za kisheria. Kumega sehemu ya Jamhuri ya muungano na kumpa mtu mwingine madaraka ya kugawanya mipaka ya sehemu hiyo nje ya yule aliyechaguliwa kidemodrasia kama Raisi mwenye mamlaka, walifanya kosa la uhaini. Kinachotutesa waTanzania ni kukosa uongozi thabiti wa kukemea na kuchukua hatua.
Down in 50 years most of us won't be there, tutakuwa taifa la namna gani lenye kugawika kila wakati watu wanapotaka kivyao. Tanzania ni nchi moja, wanachofanya wale walidiriki kufanya kule Zanzibar hakivumiliki hata kidogo. Ni upuuzi mkubwa kufikiria Zanzibar kuwa nchi, ni sawa na kusema Mtwara au Lindi au Mwanza iwe nchi.
Watanzania wengi ni kizazi kilichopatikana ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatujui Tanganyika, Ni miaka 47 imepita tangu Tanganyika na Zanzibar kama nchi pekee kufariki. Zilikufa, na hazitafufuka kamwe! Nimesema ni udhaifu wa viongozi wetu wa sasa ndio unaotuweka katika utata. Sifa mojawawapo ya kiongozi bora ni mtu mwenye maono (vision), viongozi tuliowapa dhamana ya kulinda nchi yetu hawajui wajibu wao. Jambo la ku-temper na mipaka ya nchi ni jambo serious sana, wale waliofanya hivyo Zanzibar walipaswa kuchukuliwa hatua. Ndiyo maana Rais aliyepita (Mkapa) alionya kile kiitwacho muafaka. Watu wachache wenye roho ya madaraka kule Zanzibar ndio walio influence insertion ya clauses za kuvunja nchi yetu. Halafu viongozi wetu wanacheka, wanasema katiba ya Zanzibar imeimarisha zaidi Muungano, ni jambo la kijinga sana hili! Watu wanafanya usanii kwenye mambo ya msingi.
Nyerere alikataa ushauri wa Karume wa kudisolve kabisa sovereignty ya nchi hizi na leo inatupa shida. It was possible to disolve Zanzibar and Tanganyika completely in fact Tanganyika ilishapotea kabisa. Kusita sita huku ndio kunawapa wahuni nafasi ya kudhoofisha nchi yetu. Badala ya ku-focus kujenga dola lenye nguvu sasa tunawaza kuvunja nchi, tutatumia muda mwingi kugombana tu.
Kinachotakiwa sasa hivi ni kukamilisha Muungano ambao Nyerere aliuchelewasha kuwa nchi moja na kuwa na raisi mmoja na taasisi zenye nguvu zitakazosimamia maendeleo ya Tanzania moja. Hii mambo ya kuwa na raisi wawili na makamu watatu kwenye nchi moja eti tu kuridhisha matakwa ya kakundi ka watu na hasa wataka uongozi ni jambo la kukemewa kabisa.
Tuna mifano mizuri tu ya kuimarisha muungano wetu, kwa mfano kuwa na majimbo yatayopewa madaraka ya ndani ikiongozwa na watu walichaguliwa. Hivyo Zanzibar, Unguja, Kusini (Lindi, Mtwara, Ruvuma), Kati (Dodoma, Singida etc), Pwani (Dar, Moro, Tanga ...), Ziwa au maziwa makuu (-----) na kadhalika yaweza kufaa au hata vinginevyo. Lakini hili la kuwa na raisi wawili ndani ya nchi moja halifai kabisa.
Kama hili haliwezekani (yaani kuwa nchi moja chini ya rais mmoja) la kuwa na serikari tatu ndiyo haliwezekani kabisa wala Wazanzibari wasiwaelekeze huko wakidhani wabara watafurahi. Selikari tatu ni kizunguzungu kitakachokwamisha maendeleo yetu kwa miaka mingine 50 kama sio 100 ijayo. It will be sad, very sad but probably we will accept to part peacefully - Lakini nchi itaendelea kuitwa Tanzania na siyo Tanaganyika. Hivyo basi vitambulisho viendelee, Kama Wazanzibari wa sasa watang'ang'ana kutoka kwenye muungano basi sehemu itayobaki itaendelea kuitwa Tanzania.
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote.
Viongozi bado mna nafasi ya kuikoa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chukueni hatua sahihi kwa wale wanaoleta fyokofyoko za kuvunja muungano. Kwenye kujenga umoja wa nchi yatakiwa muwe serious sana, Msivumilie watu wa namna hiyo hata kama ni marafiki zenu.
Rais Kikwete ametamani sana kuleta utengamano kule Zanzibar na kwa na namna fulani kwa muda mfupi ujao Zanzibar itatulia, lakini si sustainable. Raisi wetu ame trade off sana principles za kujenga strong future ya nchi hii kuleta tu amani ya muda mfupi kule Zanzibar. Ni risk kubwa sana hii. Yetu macho na masikio. The most sustainable system ni kuondoa sub autonomy section ya nchi moja. Kama Zanzibar haitakuwa na raisi watogombania nini? Sana sana itakuwa oh wenzetu wa bara wanapata hichi sisi hatupati.....