Vitambulisho vya Taifa: Maoni ya Mchungaji

Vitambulisho vya Taifa: Maoni ya Mchungaji

Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, 1964. Haijalishi ziliunganaje cha muhimu ziliungana ikawa nchi moja full stop. Hatuwezi kila kizazi kingine kikija tunapangua taifa letu. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na Tanganyika ilikufa mwaka 1964 kwa utashi wa raia wa Tanganyika, wakati huo wakiwa karibu million 10 na Wazanzibari laki 3.

Kile walichofanya Zanzibar katika katiba yao waliyopitisha juzi ni uhaini na uhuni. Na inatakiwa wale waliosababisha wachukuliwe hatua za kisheria. Kumega sehemu ya Jamhuri ya muungano na kumpa mtu mwingine madaraka ya kugawanya mipaka ya sehemu hiyo nje ya yule aliyechaguliwa kidemodrasia kama Raisi mwenye mamlaka, walifanya kosa la uhaini. Kinachotutesa waTanzania ni kukosa uongozi thabiti wa kukemea na kuchukua hatua.

Down in 50 years most of us won't be there, tutakuwa taifa la namna gani lenye kugawika kila wakati watu wanapotaka kivyao. Tanzania ni nchi moja, wanachofanya wale walidiriki kufanya kule Zanzibar hakivumiliki hata kidogo. Ni upuuzi mkubwa kufikiria Zanzibar kuwa nchi, ni sawa na kusema Mtwara au Lindi au Mwanza iwe nchi.

Watanzania wengi ni kizazi kilichopatikana ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatujui Tanganyika, Ni miaka 47 imepita tangu Tanganyika na Zanzibar kama nchi pekee kufariki. Zilikufa, na hazitafufuka kamwe! Nimesema ni udhaifu wa viongozi wetu wa sasa ndio unaotuweka katika utata. Sifa mojawawapo ya kiongozi bora ni mtu mwenye maono (vision), viongozi tuliowapa dhamana ya kulinda nchi yetu hawajui wajibu wao. Jambo la ku-temper na mipaka ya nchi ni jambo serious sana, wale waliofanya hivyo Zanzibar walipaswa kuchukuliwa hatua. Ndiyo maana Rais aliyepita (Mkapa) alionya kile kiitwacho muafaka. Watu wachache wenye roho ya madaraka kule Zanzibar ndio walio influence insertion ya clauses za kuvunja nchi yetu. Halafu viongozi wetu wanacheka, wanasema katiba ya Zanzibar imeimarisha zaidi Muungano, ni jambo la kijinga sana hili! Watu wanafanya usanii kwenye mambo ya msingi.

Nyerere alikataa ushauri wa Karume wa kudisolve kabisa sovereignty ya nchi hizi na leo inatupa shida. It was possible to disolve Zanzibar and Tanganyika completely in fact Tanganyika ilishapotea kabisa. Kusita sita huku ndio kunawapa wahuni nafasi ya kudhoofisha nchi yetu. Badala ya ku-focus kujenga dola lenye nguvu sasa tunawaza kuvunja nchi, tutatumia muda mwingi kugombana tu.

Kinachotakiwa sasa hivi ni kukamilisha Muungano ambao Nyerere aliuchelewasha kuwa nchi moja na kuwa na raisi mmoja na taasisi zenye nguvu zitakazosimamia maendeleo ya Tanzania moja. Hii mambo ya kuwa na raisi wawili na makamu watatu kwenye nchi moja eti tu kuridhisha matakwa ya kakundi ka watu na hasa wataka uongozi ni jambo la kukemewa kabisa.

Tuna mifano mizuri tu ya kuimarisha muungano wetu, kwa mfano kuwa na majimbo yatayopewa madaraka ya ndani ikiongozwa na watu walichaguliwa. Hivyo Zanzibar, Unguja, Kusini (Lindi, Mtwara, Ruvuma), Kati (Dodoma, Singida etc), Pwani (Dar, Moro, Tanga ...), Ziwa au maziwa makuu (-----) na kadhalika yaweza kufaa au hata vinginevyo. Lakini hili la kuwa na raisi wawili ndani ya nchi moja halifai kabisa.

Kama hili haliwezekani (yaani kuwa nchi moja chini ya rais mmoja) la kuwa na serikari tatu ndiyo haliwezekani kabisa wala Wazanzibari wasiwaelekeze huko wakidhani wabara watafurahi. Selikari tatu ni kizunguzungu kitakachokwamisha maendeleo yetu kwa miaka mingine 50 kama sio 100 ijayo. It will be sad, very sad but probably we will accept to part peacefully - Lakini nchi itaendelea kuitwa Tanzania na siyo Tanaganyika. Hivyo basi vitambulisho viendelee, Kama Wazanzibari wa sasa watang'ang'ana kutoka kwenye muungano basi sehemu itayobaki itaendelea kuitwa Tanzania.

Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote.

Viongozi bado mna nafasi ya kuikoa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chukueni hatua sahihi kwa wale wanaoleta fyokofyoko za kuvunja muungano. Kwenye kujenga umoja wa nchi yatakiwa muwe serious sana, Msivumilie watu wa namna hiyo hata kama ni marafiki zenu.

Rais Kikwete ametamani sana kuleta utengamano kule Zanzibar na kwa na namna fulani kwa muda mfupi ujao Zanzibar itatulia, lakini si sustainable. Raisi wetu ame trade off sana principles za kujenga strong future ya nchi hii kuleta tu amani ya muda mfupi kule Zanzibar. Ni risk kubwa sana hii. Yetu macho na masikio. The most sustainable system ni kuondoa sub autonomy section ya nchi moja. Kama Zanzibar haitakuwa na raisi watogombania nini? Sana sana itakuwa oh wenzetu wa bara wanapata hichi sisi hatupati.....
 
Nadhan mtoa hoja umeona mbali sana nakupongeza 2tapata hasara kubwa sana kwan uhai wa muungano unatia hofu 2kikurupuka itakua nikukosa akir kwan badae 2talazmika kuanza mchakato upya wakutengeneza vitambulisho vyatanganyika tutajifariji kama muungano utadum lakin nawahakikishia ha2na miaka miwili 2tajiita watanganyika tena kishujaa
 
Sioni sababu kwanini tuanze kushughulikia suala la vitambulisho vya taifa wakati mpaka sasa utaifa wetu hatuujui. Sisi tulidai uhuru na wala hatujawahi kutuma mtu yeyote kwenda kututafutia nchi ya kuungana nayo.
Ni afadhari huyo anedhani aliunganisha pande hizi angeruhusu mjadala na kuhusu huo muungano na mwisho mjadala ungehitimishwa kwa kupigiwa kura, na si kwa namna walivyofanya. Kwa kweli Mzee wetu pale alichemka kwa kutumia vibaya madaraka yake.
Hivyo sioni sababu ya kufanya jambo la gharama kubwa ambalo ni dhahiri kuwa litarudiwa tena, kwanza hao jamaa wa nyumba ya jirani si nao wapo kwenye mchakato kama huo huko kwao?
Tupige kwanza kura ya kuulizwa kama tunahitaji muungano au la, ili tutambue kwanza utaifa wetu ndipo zoezi hilo liendelee.
 
Tukumbuke kuwa huu ni mgogoro mwengine kwani Zanzibar wanavyo vitambulisho vyao(ZAN ID).Je sasa katika hivi nao wamo ama ni watanganyika peke yao ? kwanza lipatikane suluhisho la nchi...tusinunue punda kwa mlio.....
 
Mimi sioni tatizo la kuendelea na ili zoezi la vitambulisho; sana sana mambo yakiharibika kitakachotokea ni shirikisho la Tanganyika na Zanzibar, ambapo zitakuwepo serikali tatu na taifa moja la Tanzania.
 
Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, 1964. Haijalishi ziliunganaje cha muhimu ziliungana ikawa nchi moja full stop. Hatuwezi kila kizazi kingine kikija tunapangua taifa letu. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na Tanganyika ilikufa mwaka 1964 kwa utashi wa raia wa Tanganyika, wakati huo wakiwa karibu million 10 na Wazanzibari laki 3.

Down in 50 years most of us won't be there, tutakuwa taifa la namna gani lenye kugawika kila wakati watu wanapotaka kivyao. Tanzania ni nchi moja, wanachofanya wale walidiriki kufanya kule Zanzibar hakivumiliki hata kidogo. Ni upuuzi mkubwa kufikiria Zanzibar kuwa nchi, ni sawa na kusema Mtwara au Lindi au Mwanza iwe nchi.

Watanzania wengi ni kizazi kilichopatikana ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatujui Tanganyika, Ni miaka 47 imepita tangu Tanganyika na Zanzibar kama nchi pekee kufariki. Zilikufa, na hazitafufuka kamwe! Halafu viongozi wetu wanacheka, wanasema katiba ya Zanzibar imeimarisha zaidi Muungano, ni jambo la kijinga sana hili! Watu wanafanya usanii kwenye mambo ya msingi.

Nyerere alikataa ushauri wa Karume wa kudisolve kabisa sovereignty ya nchi hizi na leo inatupa shida. It was possible to disolve Zanzibar and Tanganyika completely in fact Tanganyika ilishapotea kabisa.

Kinachotakiwa sasa hivi ni kukamilisha Muungano ambao Nyerere aliuchelewasha kuwa nchi moja na kuwa na raisi mmoja na taasisi zenye nguvu zitakazosimamia maendeleo ya Tanzania moja. Hii mambo ya kuwa na raisi wawili na makamu watatu kwenye nchi moja eti tu kuridhisha matakwa ya kakundi ka watu na hasa wataka uongozi ni jambo la kukemewa kabisa.

Kama hili haliwezekani (yaani kuwa nchi moja chini ya rais mmoja) la kuwa na serikari tatu ndiyo haliwezekani kabisa wala Wazanzibari wasiwaelekeze huko wakidhani wabara watafurahi. Selikari tatu ni kizunguzungu kitakachokwamisha maendeleo yetu kwa miaka mingine 50 kama sio 100 ijayo. It will be sad, very sad but probably we will accept to part peacefully - Lakini nchi itaendelea kuitwa Tanzania na siyo Tanaganyika.
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote.

Viongozi bado mna nafasi ya kuikoa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chukueni hatua sahihi kwa wale wanaoleta fyokofyoko za kuvunja muungano. .....

Mkuu.
Hizi kelele ulizopiga hapa ni kwa sababu tu unataka Jamhuri ya Tanzania badala ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania)?

Mkuu. Unaikumbuka Soviet Union? Unaikumbuka Yugoslavia?....Na miungano hii pia ilikuwa ya nchi za kijamaa kama ilivyo kwa Tanzania.....Katiba inasema Tanzania ni nchi ya kijamaa.

Mkuu...mwanzoni mwa mchango wako unasema kwa kujiamini kuwa Tanzania ni nchi moja lakini mwishoni mwa mchango wako unasema "Kinachotakiwa sasa hivi ni kukamilisha Muungano ambao Nyerere aliuchelewasha kuwa nchi moja "..... Jee tukuelewe vipi?

Tanzania ni muungano wa nchi hizi:- Tanganyika na Zanzibar.

Lakini pitia hii michango mengine hapa pengine utaelewa kuwa Tanzania ni usanii na kama ulivyogusia katika mchango wako viongozi wanafanyaa usanii.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kn-mimi-nitabaki-mtanzania-3.html#post1896563

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/129687-kipindi-cha-mpito-kuelekea-hatma-ya-muungano-wa-tanganyika-na-zanzibar-3.html#post1899577

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/128366-jumuiya-ya-afrika-mashariki-na-zanzibar-2.html#post1884754

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/128366-jumuiya-ya-afrika-mashariki-na-zanzibar.html#post1878568

https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/58588-muungano-wa-tanganyika-na-zanzibar%3B-una-faida-gani-na-kwa-manufaa-ya-nani-26.html#post1868536

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wanawawakilisha-nani-bungeni.html#post1857826
 
Afadhali wadau mmeliona hili. Mie nawaaambia watu watafanya usanii katika hili. Kama zanzibar wana vitambulisho vyao vya kwetu(bara) vina tutambulishaje?
 
Mkuu.
Hizi kelele ulizopiga hapa ni kwa sababu tu unataka Jamhuri ya Tanzania badala ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania)?

Mkuu. Unaikumbuka Soviet Union? Unaikumbuka Yugoslavia?....Na miungano hii pia ilikuwa ya nchi za kijamaa kama ilivyo kwa Tanzania.....Katiba inasema Tanzania ni nchi ya kijamaa.

Mkuu...mwanzoni mwa mchango wako unasema kwa kujiamini kuwa Tanzania ni nchi moja lakini mwishoni mwa mchango wako unasema "Kinachotakiwa sasa hivi ni kukamilisha Muungano ambao Nyerere aliuchelewasha kuwa nchi moja "..... Jee tukuelewe vipi?

Tanzania ni muungano wa nchi hizi:- Tanganyika na Zanzibar.

Lakini pitia hii michango mengine hapa pengine utaelewa kuwa Tanzania ni usanii na kama ulivyogusia katika mchango wako viongozi wanafanyaa usanii.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kn-mimi-nitabaki-mtanzania-3.html#post1896563

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/129687-kipindi-cha-mpito-kuelekea-hatma-ya-muungano-wa-tanganyika-na-zanzibar-3.html#post1899577

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/128366-jumuiya-ya-afrika-mashariki-na-zanzibar-2.html#post1884754

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/128366-jumuiya-ya-afrika-mashariki-na-zanzibar.html#post1878568

https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/58588-muungano-wa-tanganyika-na-zanzibar%3B-una-faida-gani-na-kwa-manufaa-ya-nani-26.html#post1868536

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wanawawakilisha-nani-bungeni.html#post1857826

Nonda,

Ninachokisema ni hiki there is no way Tanganyika and Zanzibar can be separate sovereign states again. Mifano uliyoitoa ya soviet union na kadhalika ilfafanuliwa vizuri sana na mchangiaji wa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kn-mimi-nitabaki-mtanzania-3.html#post1896563 uliyoninukulia hapo juu kaisome vizuri. Pole kama nilikuchanganya, nilichosema ni kuelekea kuwa na Raisi mmoja tu na siyo wawili ama watatu kama wengine wanapendekeza.

Hakuna ufahari wowote kuwa na serikali tatu yani ya Tanganyika ya Zanzibar na kisha shirikisho. Havitatatua matitizo ya msingi tulio nayo, watu wanajidanganya kuwa kuitwa Mtanganyika kutaleta tofauti yoyote. Kuwa na Tanganyika hakutaondoa Ufisadi, hakutaondoa inefficiency kwa watendaji kwa ujumla hakutakuwa any positive change. Wengi waliokalia nafasi za kuleta mabadiriko ni watu wa bara lakini mambo hayaendi kila kukicha mara vijisenti, mara dowans, mara epa, mara rada, mara ndege ya raisi, mara dawasco, mara trl, mara madini, orodha ni ndefu sana. Wahusika wakuu ni watu wa bara ambao ukifufua (kama utakuwa na uwezo) ndio wataoshika hatamu (patamu).

Matatizo yote tuliyo nayo wala hayaletwi na wazanzibari. Watu walimlaumu Mzee Mwinyi oh kaleta uswahili, oh mzee ruksa oh na kadhalika. Haya kaondoka Mzee Mkapa kaingia na sasa Kikwete, yako wapi? Mbona bado tunalia. Kuna watu wanachukia wazanzibari utafikiri wao ndio source ya matatizo ya umaskini wa nchi yetu. Kuna Wazanzibari wachache wana fikra potofu, ndio maana nikasema kiongozi imara anaweza kusimamia na kuwashughulikia kikamilifu. Hatuwezi kuwa na taifa fluid ambamo raia wake hawana uhakika na nchi yao kila wakati. Nimesema wazi kabisa wale walio engineer draft ya katiba mpya ya Zanzibar walivunja sheria wanapaswa kuchukuliwa hatua. Kiongozi mkuu aliyeapa kulinda katiba alikaa kimya kwa sababu nilizozieleza hapo mwanzo. Tulimwambia akasema kitendo walichofanya kitaimarisha muungano zaidi!

Bottom line Zanzibar kama nchi na Tanganyika kama nchi vilikufa 26/4/1967 anayefikiri Zanzibar au Tanganyika vinaweza kufufuka na kuwa nchi peke yake kikamilifu tena anajidanganya na kamwe haitatokea. Wazanzibari wasahau kuwa sovereign state tena na wale wanaoota Utanganyika don't even think about it.
 
Ndo maana nasema viongozi wakuu wa zanzibar wanayoyasema majukwaani ni tofauti na yaliyoko mioyoni mwao. Waeleze hadharani mpango wao
 
Nonda,

Ninachokisema ni hiki there is no way Tanganyika and Zanzibar can be separate sovereign states again. Mifano uliyoitoa ya soviet union na kadhalika ilfafanuliwa vizuri sana na mchangiaji wa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kn-mimi-nitabaki-mtanzania-3.html#post1896563 uliyoninukulia hapo juu kaisome vizuri. Pole kama nilikuchanganya, nilichosema ni kuelekea kuwa na Raisi mmoja tu na siyo wawili ama watatu kama wengine wanapendekeza.

Hakuna ufahari wowote kuwa na serikali tatu yani ya Tanganyika ya Zanzibar na kisha shirikisho. Havitatatua matitizo ya msingi tulio nayo, watu wanajidanganya kuwa kuitwa Mtanganyika kutaleta tofauti yoyote. Bottom line Zanzibar kama nchi na Tanganyika kama nchi vilikufa 26/4/1967 anayefikiri Zanzibar au Tanganyika vinaweza kufufuka na kuwa nchi peke yake kikamilifu tena anajidanganya na kamwe haitatokea. Wazanzibari wasahau kuwa sovereign state tena na wale wanaoota Utanganyika don't even think about it.
Salisalum,
Maelezo yako matamu kama asali. Hata hivyo mkuu, niruhusu nikukumbushe maneno ya mwalimu katika hali tuliyonayo leo ya kufufuliwa kwa EAC na hatua ambayo itapelekea EA Federation.

Mwalimu leo angeridhia kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Alisema hivi:-
"Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili."

Baadaya Azimio la EA federation bado tunaona umuhimu wa kung'ang'ania Tanzania?
Soma ukurasa wa 10 mpaka 12. Kwa kuifufua EAC na azimio la kuanzisha EA federation ni wazi basi muungano wa Tanganyika na Zanzibar umepoteza maana na mantiki ya kuendelea kuwepo. Au tunayapinga maneno ya "baba wa taifa"?

Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
 
Wazanzibari mnasemaje kwa hili? Mambo yaendelee hamna tatizo?

Sisi Wazanzibari tunavyo vya kwetu na hatuna haja ya vya Tanzania kama tusivyo na haja ya huu unaoitwa "muungano"

Hata hivyo huko kwetu vinatumika vibaya mpaka kupewa wageni kupiga kura (ni masharti ya kuandikishwa katika daftari la kudumu la kupiga kura.)

Hivyo huo mchezo hata huko kwenu unaweza kutumika, ni tahadhari tu:

msumbiji1.jpg

zanid1.jpg

Huyu ni raia wa Msumbiji ambae alipewa kitambulisho cha Mzanzibari ili aweze kupiga kura ingawa huko kwao pia ameshapiga kura.

Hivi ndivyo CCM yenu inavyoshinda Uchaguzi.

Hivi ndivyo CCM inavyoimarisha "muungano"

Pamoja na kuleta majeshi ya uvamizi Zanzibar na kutuadhibu ndani ya nchi yetu wenyewe:

View attachment 29317

View attachment 29318

Sasa tutaukubali vipi "muungano" wenu huu?
 
Attachments

  • msumbiji2.jpg
    msumbiji2.jpg
    105.6 KB · Views: 9
hoja nzuri yenye muono wa mbele. naiafiki kwa 100%. kama tumeishi miaka yote hii bila hivyo vitambulisho, hatuna haraka navyo mpaka mustabali wa nchi uwe wazi
 
hoja nzuri yenye muono wa mbele. naiafiki kwa 100%. kama tumeishi miaka yote hii bila hivyo vitambulisho, hatuna haraka navyo mpaka mustabali wa nchi uwe wazi

Safi sana kiongozi. Roho yangu inaniambia kuwa utakuwa uzushi kama ilivyokwenye noti mpya
 
Ukiona wanaharakisha suala la vitambulisho lazima patakuwa na uwalakini,Serikali nnajua mnapita humu tafadhali kalifanyieni kazi kwa umakini
 
Kama kawaida ya Great Thinkers wetu, mtu anatoa hoja moja zinazuka hoja kumi na moja. Sipingi hilo kwani yote yameungana na yasipopatiwa ufumbuzi, watu watakula pesa baadaye tuambiwe "vitambulisho vile havifai na itabidi tchapishe vipya". Suala la msingi hapa ni "mchakato wa vitambulisho" na harufu ya rushwa inayonukia katika utengenezaji wake.

Lakini katika kujadili suala la vitambulisho pamezuka suala mwiba la muda mrefu la "Mustakabali wa Muungano wetu". Na kwa kuwa tunajadili hili pia, nitaliweka upande suala la vitambulisho na kutoa maoni yangu kama Mzanzibari, kama Mtanzania kuhusu Muungano. Nasema kama Mzanzibari kwa sababu kule ndiko nilikozaliwa, kama ambavyo atatoa maoni Mtanga, Mmwanza, Muarusha n.k. nikimaanisha kuwa sote tunajitambua kuwa ni Watanzania kutoka sehemu gani. Hapa watakaosoma ndani ya misitari wataelewa nimekusudia nini.

Tatizo si Muungano kama suala la msingi, bali utata na uwingu uliomo katika muundo wa Muungano wenyewe. Tukubali kuwa waasisi wa Muungano, pamoja na nia yao nzuri, hawakuwa wawazi tangu mwanzo katika Muundo wa Muungano. Kwa maneno mengine, muungano wetu ulikuwa wa kiitikadi (kijamaa) zaidi (dhidi ya itikadi ya kibepari au ya kimagharibi) kuliko matakwa ya watu wetu; na ndio maana, kama alivyogusia mmoja hapo juu, miungano iliyowekwa kiitikadi yote imekufa (Urusi na Yugoslovakia).

Kwa wale wanaoona ubaya wa serikali 3, wamejiuliza katika Umoja wa Ulaya kuna serikali ngapi? Ninavyokumbuka kwa sasa ni 27 na bado nchi zinaendelea kuungana na mpaka leo katika nchi za EU kila nchi ina ID zake na Passport zake, kila nchi ina serikali yake na shughuli zake. Kwa hiyo, sioni ubaya wa Tanzania kuungana kwa muundo huo, na bado ikabaki kama Tanzania, huku Watanganyika na Wazanzibari wakawa na utambulisho wao, bila ya kuathiri uwepo wa Tanzania. Faida nyengine ya kuwa na serikali 3, itaondosha hii mnayoiita fyokofyoko na longolongo la nani anamkandamiza nani, nani anammeza nani.

Labda neno la mwisho na ambalo ninaimani nitawekwa msalabani lakini siogopi wala kulionea haya kulisema, ni kwa Wazanzibari wenzangu. Umefika wakati wa kuacha kuwalaumu Watanganyika kuwa wamekuwa ndio sababu kubwa ya kikwazo cha Maendeleo ya Zanzibar. Pengine kuna mambo ambayo ki-nje nje yataonekana kama vilevSerikali ya Muungano ina mkono wake, lakini kuilaumu Tanganyika kwa kukosa kwetu maendeleo ni sawa na wale wanaoendelea kuwalaumu wakoloni kwa sababu hiyo hiyo.

Nitatoa mifano michache inayonigusa sana. Zanzibar walianzisha chuo kikuu chao mwaka 2002/2003, miaka 9 sasa. Wakati ule wakapewa eneo la Tunguu kujenga chuo chao pale, wakapata misaada na mikopo ya ujenzi. Wamefikia wapi hadi leo? Bado wanaendelea kupiga kwata na Kitivo kimoja cha "Undergraduates" na wameshindwa kutoa shahada za uzamili hadi leo. Ukilinganisha na Dodoma ambao kulianzishwa chuo miaka minne baadaye, angalieni sasa wako wapi ki kiwango cha elimu na miundo mbinu. Hivi tuseme Watanganyika ndio walio/wanaoizuwia Zanzibar isiendelee kwa hili? Ni wasomi wangapi wa Zanzibar wanakimbia kusomesha na kufanyakazi Zanzibar? Ni Watanganyika ndio wanaowaambia hameni kwenu? Naomba anayejua ukweli kuhusu hili atupe maelezo. Vile vile Wazanzibar tunalalamika uwepo wa vyuo vikuu vya wakristo Tanzania bara; hivi hakuna matajiri wa kizanzibari, wa ndani na nje ya nchi ambao wanauwezo wa kuanzisha vyuo vikuu lakini hawafanyi, kwa nini? Watawalaumu Watanganyika kwa kuwakosesha vibali wakati hakuna hata aliyejaribu. Hivi Watanganyika ndio wanaosababisha mpaka leo Zanzibar isiwe na umeme wa uhakika, huku tunajisifu kuwa ZNZ ulianza kuwaka umeme kabla ya London? Ni Watanganyika wanaoifanya Zanzibar isiwe na barabara za viwango wakati Zanzibar nzima ni ndogo kuliko mkoa mmoja tu wa Tanganyika? Watanganyikka ndio wanaoifanya TVZ iwe haina viwango mbali na kujisifu tu kuwa "ZNZ ni nchi ya mwanzo Afrika ya Mashariki kuwa na TV ya rangi, lakini bado inafungua saa 4 asubuhi na kufunga saa 6 usiku? Tuwache kulalamika bila kuangalia chanzo hasa cha tatizo.

Juzi kuna Mzanzibari mwenzangu ameniambia eti "Wabara wamefanyafanya mpaka Benki ya Watu wa Zanzibar wameichukua kwao", baada ya kuona kuwa PBZ wamefungua tawi Dar. Mawazo kama haya ya watu wa vijiweni, wanaolishwa kasumba katika akili zao mtindio, ndiyo yanayowafanya watu bila kujua wananungúnika "kihiyohiyo".

Kwa ufupi, mimi ni Mzanzibari na ninayeipenda Zanzibar (na Tanzania bila ya shaka), lakini ninawaomba Wazanzibari wenzangu wanaouchimbachimba Muungano wafikirie tena na tena wakati hata sembe, mchele, maharage, umeme...na msululu wa mahitaji tunayapata kutoka Tanganyika. Ninawasilisha na ninasubiri kusulubiwa.
 
Haya ndiyo maajabu mengine....hivi kuna wazanziba ambao wanafikiri vizuri ku-neutralise mawazo yao kwa kiwango hiki? Amini nawaambieni, kama tungekuwa na watu 10 tu wa aina hii ndani ya Zanzibar leo hii hata kama hawana nafasi za uongozi, yaani wawepo tu mitaani, Zanzibar na Tanzania tungekuwa mbali sana na kusingekuwa na kelele za muungano na Tanzania ingekuwa na jambo la kujivunia.
Ninaongea hivyo kwasababu wazanzibar wanachoamini ni kuwa waliumbwa na kuzaliwa ili waje dunianai kupingana, kuwatusi na kubishana na Tanganyika, wameaminishana na kurithishana hivyo, ukiona mtu hususani viongozi wa zenji wapo kimya ujue kuna maslahi wanayapata yakikata nao wanaanza kuunanga muungano na kutukana Tanganyika. Ndiyo maana hata sasa hakuna mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi wa vyombo na idara za serikali zenji na wale wa . Hili lipo wazi.
Hongera sana Mammamia kwa kuwa na ka-vision
 
Back
Top Bottom