Ukweli mkubwa sana. Hao jamaa ndiyo wanatakiwa kuwa na hizi Datas zote na si wizara gani sijui.....
Wazo zuri sana sana na ninategemea Dr. Slaa, Tundu Lisu, Marando, Lipumba, na wadau wengine watalipinga hili na ikibidi kuandamana barabarani basi twendeni haraka.
Hicho chombo kiwezeshwe kwa kupewa hizo pesa na wanunue mitambo pamoja na Computer ambazo nyingine ziwe zimeunganishwa kwenye Internet na nyingine hazijaunganishwa.
Nafikiri KADI isiwe muhimu sana ila Data zilizowekwa kwenye computer maana hata mtu akikamatwa, inatosha tu kupiga simu HQ au kuangalia kwenye Internet na kupata uhakika kama kweli huyo ndiyo mwenye hiyo kadi.
Nafikiri hata nchi kama UK, watu huwa wanatembea bila kitambulisho. POLISI wakikukamata, wanakuuliza jina, sehemu unayokaa, tarehe ya kuzaliwa, jina la baba, mama nk na ole wako UDANGANYE. Wakishaandika, wanapiga simu kituoni na kupewa data kamili zako. Kuna wengine hudanganya, ila ni poa tu maana ikatokea kumbe nduguyo alikuwa anatafutwa, basi Watakubeba wewe. Hivyo watu huwa makini sana.
Nakumbuka zamani hapa Sikonge Hospital watu walikuwa wanapewa VIPANDE. Kipande kilikuwa ni kibati chenye namba yako ya FAILI na humo waliweka data zote. Watu walikuwa wakipoteza vipande na kila kitu kinapotea. Hizi kadi nazo zitakuwa zinapotea tu na watu vijijini ndiyo itakuwa kasheshe..... Dawa ni kuweka data na hizi kadi ziwe za kawaida sana na hii itapelekea bei yake iwe nafuu.
Hata wakizitengeneza vipi, watu mtaani watazifyatua tu. Wakishaenda China ndiyo kwanza watakuja na kadi nzuri kuzidi hata hizo za hao jamaa na pia kwenye mambo ya Datas, hawa Wa-Asia ukiacha Japan sijui kama ni wazuri sana kama walivyo German, Uk, nk nk..