Vitambulisho vya Taifa: Maoni ya Mchungaji

Vitambulisho vya Taifa: Maoni ya Mchungaji

Nchi ya mafisadi! ooh sorry, I'm proud of mother land "Tz"......mmmh calling myself TzPride!, probably I'm one of the fisadi"s
 
Wacha tungoje majibu ya barua yao maana ni haki yao ya msingi kuambiwa kwa nini wametupiliwa mbali ili wajue wapi wana makosa wajijenge kama kampuni .Lakini hizi smart cards tutazitumia kwenye machine ya ATM ama wapi ? Na wakati gani ?Kule kijiji kwetu zitatumika wapi ? Ili wanakijiji wamapate ? Kama ni National ID pekee mbona haya Passport imeshindikana kumpa kila mmoja ama ni ghali kuliko ID card ?
 
Lunyungu, hawa jamaa wanabebwa na watu wazito sana. Wameishasema kuwa kwa gharama yeyote LAZIMA waupate mradi huu. Tayari kuna taarifa kuwa wameisha muweka sawa Katibu Mkuu.
 
Kwa ufahamu wangu ni kuwa, Passport ni document kwa ajili ya kusafiria tu, hivyo utaitumia wakati wa safari tu, kama vile driving license, ni kwa wale wanaendesha magari tu.

Unajua Tanzania inapakana na nchi nane, kutokana matatizo ya kiusalama ktk nchi majirani hao,wote hutafuta nafasi ya kuingia na kuishi Tanzania. Kama haitoshi, wananchi toka Somalia na Sudan nao wanaingia Tanzania. Hao wote huendelea kufanya shughuli zao zisizo halali, na wengine kujihusishana uhalifu wa namna mbali mbali.

Inakuwa tabu kuwakamata wageni hao kwani hawatambuliki kirahisi kama wao ni wageni. Kwa sababu hiyo, hujiichanganya ktk mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupiga kura, kupata hati za kusafiria na kadhalika. Wengine huamua kwenda kuishi mikoani na hata vijijini ambako inakuwa vigumu kuwasaka.

Wakiwa vijijini hujichanganya na wenyeji ktk shughuli mbali mbali za maendeleo na kugombea nafasi mbali mbali ktk ngazi za uongozi.

Ni kitambulisho pekee ndio kitakachoweza kumtambua mgeni na raia.

Kwa kuwa miundombinu ya umeme haijaenea vizuri nchini, ni technology ya Smart card pekee ndio itakayoweza ku-operate ktk offline, yaani wahusika hawatahitaji kuwa na umeme kusoma data za mtu atakayetakiwa kuonesha kitambulisho. Lakini ili kuwe na security ya hali ya juu sana, tunahitaji Smart card kudhibiti "identity theft".

Sijui kama nimeweza kukupa taarifa ulikuwa unaitaka? Niulize tu, nitajitahidi kukuelewesha kile ninachokijua mimi kuhusu technology hii.
 
Nimeisoma barua ya Sagem iliyopo hapo juu. Nimeenda ktk mtandao, na kuwasiliana na jamaa zangu dunia nzima kutaka kujua hivi ni lini na wapi Sagem wame-implement mradi wa vitambulisho kwa teknologia ya smart card, SIJAPATA. Hivi hawa jamaa walidhani Tanzania ni sehemu ya kutupia teknologi zilizopitwa na wakati?

Sagem wameshitakiwa Nigeria, na hata Ghana kwa utapeli ktk miradi ya vitambulisho. Nashangaa kwanini wao hawalioni hilo kama ni kikwazo kikubwa kwao? au kwa sababu wanabebwa na "WAKUBWA" fulani pale wizara ya Mambo ya Ndani? Hivi hawajiulizi ni kwanini kila wanakoenda kuomba miradi ya vitambulisho wao ndio wanakuwa TATIZO? Hivi kwanini hao wanaowasaiia Sagem wasitafute kampuni zenye uwezo wa kufanya kazi hii, badala ya kuibeba kampuni ISIYOFAA? Hivi ni lini viongozi wetu watakuwa na uchungu na hela za watanzania masikini?
 
Nilivyoona ktk matangazo ya kumpa mzabuni, Serikali inataka smart card ambayo ni "multpurpose". Hii ina maana kuwa kitambulisho cha Taifa kitaweza kutumika ktk functions nyingine kama vile, Benki, Driving License, Passport details, Health Insurance details ambamo mtu ataweza kuweka aina ya damu yake na hivyo kurahisisha huduma hiyo pindi inapohitajika. Kumbuka kuwa kule Tanzania watu wengi sana wanakufa ktk ajali kutokana kucheleweshwa kuongezewa damu, na hii ni kwa sababu hawajui blood group ya majeruhi.

Tanzania ina walipa kodi wasiopungua milioni kumi na nne, lakini cha kushangaza, ni walipa kodi wasiozidi laki tano tu ndio waliomo ktk data base ya TRA. Kenya wana wanalipa kodi milioni kumi na mbili, na hivyo kuifanya nchi hiyo kupunguza utegemezi ktk bajeti yake ya nchi.
 
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeiomba Serikali katika hatua za mwisho zilizobaki za kumpata mzabuni wa kutengeneza vitambulisho hivyo, kutumia vyombo vya usalama wa Taifa kumpata mzabuni wa kuendesha mradi huo.

Mamlaka hiyo imetaka kutotumiwa kwa utaratibu wa zabuni za uwazi ili kuepuka kufikishwa mahakamani, pindi baadhi ya wazabuni wanaposhindwa.

Badala yake imetaka wabunge na wananchi waiamini Serikali na kukabidhi kazi hiyo kwa vyombo vya usalama vya Taifa kwa ajili ya kusimamia kumpata mzabuni ili kuepukana na hatari ya kufikishwa mahakamani na wazabuni, kama ilivyotokea Kenya pindi wazabuni wengine wanaposhindwa.

Tangu kutangazwa kwa zabuni hiyo ya kutengeneza vitambulisho, wazabuni 104 walijitokeza, lakini 54 walitoweka, baada ya kuona ugumu wa kazi hiyo na sasa wamebaki watano ambapo Julai mwaka huu taratibu za zabuni zimepangwa kuendelea.

Akitoa mada juu ya maendeleo ya mradi huo kwa wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu, alisema "nawaomba tuiamini Serikali tusifanye zabuni ya wazi, wenzetu wa Uganda hawajafanya na Kenya walifanya kwa uwazi, matokeo yake wamefikishwa mahakamani, mimi nawaomba tuviachie vyombo vyetu vya usalama visimamie vitambulisho hivi".

Wabunge wengi walikubaliana na ombi hilo na kutaka kazi ya mwisho ya kumpata mzabuni ifanywe na Baraza la Usalama la Taifa ambalo limeonekana kuangalia zaidi maslahi ya Taifa.

Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM) alisema "naomba suala la vitambulisho lipelekwe kwenye Baraza la Usalama la Taifa, likiendelea kuwa katika zabuni ya wazi hatutafika popote, kutokana na umimi na maslahi binafsi. Watu wengine wakikosa zabuni wanakwenda kushitaki wakidai zabuni haikuwa ya wazi."

Alisema katika Baraza la Usalama la Taifa hakuna umimi bali maslahi ya Taifa pekee na kuongeza: "mbona vifaa vya Jeshi havitangazwi? Nawaomba suala la vitambulisho liondoke kwenye zabuni ya wazi. Sisi tuna maneno matamu mengi, utekelezaji shida.Tukiendelea na masuala ya siasa tutakuwa tukijihujumu wenyewe."

Mbunge wa Mtera, John Malecela (CCM), aliitaka Nida kulimaliza suala hilo la vitambulisho ndani ya Serikali na kuhadharisha kuwa baadhi ya wazabuni ndio wamiliki wa vyombo vya habari na hivyo wakishindwa, watavitumia vyombo vyao kuichafua Serikali.

Alitaka vitambulisho hivyo kutotengenezwa Korea Kusini na kusisitiza: "Nahadharisha vitambulisho kupelekwa Korea Kusini, kwa sababu ni matapeli wakubwa. Singapore ndio namba moja, wao wamekuwa na vitambulisho hivyo miaka mingi na wamefika mbali".

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF) aliitaka Mamlaka hiyo, kukusanya takwimu za kutosha kwa kutumia watu wenye taaluma hiyo, ili kuepuka dosari katika mpango wa utoaji wa vitambulisho vya Taifa.

Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa (Chadema) mbali na kukubali suala hilo kumalizwa serikalini kwa kusimamiwa na vyombo vya usalama, alitaka hatua zote za kuaminiana ziwepo na kusema Bunge kupitia kamati zake, lina haki ya kuingilia kama kutakuwa na matumizi mabaya.

Mbunge wa Rombo, Basil Mramba (CCM) alisema "Maimu nakushauri tumia sheria kwa kasi, kwani ipo siku utakuja kunyongwa".

Katika maelezo yake kuhusu mradi huo, Maimu alisema katika kampuni tano zilizobaki, hakuna ya Korea Kusini na kusema mradi huo utagharimu Sh bilioni 200 na utakuwa wa miaka mitatu kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji iliyopitishwa na Serikali.

Alisema Serikali imepata mkopo kutoka Korea Kusini wa Sh bilioni 41 kwa ajili ya kujenga kituo cha kuhifadhi takwimu. Mkopo huo utalipwa kwa miaka 40 kwa riba ya asilimia 0.2.

Alisema vitambulisho hivyo vingekuwa vimeshaanza vingeokoa gharama za uandikishaji wapiga kura ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imetumia Sh bilioni 42.9 kusafisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, na kuongeza "hata Msajili alipotaka kuhakiki wanachama ingemsaidia, ingeongeza ukusanyaji mapato".

Alisema mradi huo utakapokamilika, utakuwa na kadi za aina tatu kwa mfumo wa smart card na zitatolewa kwa Watanzania, wageni na wakimbizi.

Katika taarifa zitakazojumuishwa za mtu ni pamoja na makazi yake, ndoa, umri na zitatumika pia katika upatikanaji wa leseni za kuendesha gari, mifuko ya hifadhi ya jamii na kuisaidia Serikali kufahamu mapato ya kampuni kama za simu za mkononi.

Source: Habari Leo
 
Alisema katika Baraza la Usalama la Taifa hakuna umimi bali maslahi ya Taifa pekee
Bongo bana!!!


Hivi wakati Richmond, EPA, Kagoda vinatokea hilo baraza la usalama wa taifa lilikuwa wapi? Na baada ya scandal hizo kujulikana baraza hili limefanya nini kuhakikisha the culprits are brough to book na wizi kama huo hautokei tena??????
 
Elimu ya Uraia sifuri:

Baraza la Usalama... ni watu wa chache, Rais, Waziri Mkuu, sijui Spika, Jaji mkuu, Katibu Mkuu kiongozi etc... this has nothing to do with TISS... please read carefully.
 
Mhh..full comedy..

Mwingine anasema eti dili wasipewe wakorea kwa sababu ni matapeli? Wangekuwa matapeli wangekuwa wana compete na wazungu kwene technolojia?

Halafu hilo Baraza la Usalama sounds to me kama ni kuwapa blanck cheque wateule wachache kuandika figure yeyote kwene cheque bila kuulizwa .HUU NI UPUUZI.
 
Alitaka vitambulisho hivyo kutotengenezwa Korea Kusini na kusisitiza: “Nahadharisha vitambulisho kupelekwa Korea Kusini, kwa sababu ni matapeli wakubwa. Singapore ndio namba moja, wao wamekuwa na vitambulisho hivyo miaka mingi na wamefika mbali”.

Jamaa naona ana share yake kwenye kampuni ya Singapore, nchi ya vituko hii!!!:frusty:
 
Nasikia kama harufu ya rushwa vile maana hii imekaa ki Meremeta Meremeta
 
Tutafika tu maana somethings will come to their sense one day. Dragging this issue all that long should be of beneficial to the country.I would be suprised kama watatengeneza TRL nyingine maana kwa jinsi tulivyo wala hatushindwi
 
Bongo bana!!!

Hivi wakati Richmond, EPA, Kagoda vinatokea hilo baraza la usalama wa taifa lilikuwa wapi? Na baada ya scandal hizo kujulikana baraza hili limefanya nini kuhakikisha the culprits are brough to book na wizi kama huo hautokei tena??????

Hao jamaa wanajua mambo mengi ila wanafanya kazi by remote mwenye nayo akiamua kuizima ina zima na akiamua kupotezea channel anapotezea tu, sasa what do u expect from Usalama wa Taifa

 
Duh bongo bana watu wanaogopa kuwajibika! Kila kitu kiamuliwe kwa vikao na kisirisiri!
 
Nasikia kama harufu ya rushwa vile maana hii imekaa ki Meremeta Meremeta

Spot on!

Ukiondoa transparency Africa maana yake unaweka ufisadi, I can bet my head that this is another scandal. Itafichwa kwenye jamvi la usalama wa taifa kama tulivyofichwa Meremeta, Mwananchi Gold, etc.

Kama tender process iko fair kwa nini tuogope kushitakiwa?? Je tunataka kuficha nini?
 
waacheni wafanye kazi hiyo pengine utakuwa mwanzo mzuri wa kuondokana ufisadi tz
 
Back
Top Bottom