Vitanda vya hoteli

Vitanda vya hoteli

Dodoma moja

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
307
Reaction score
182
Habari zenu wakuu, niliwahi kulala kwenye hoteli moja jijini mwanza ambayo ni miongoni mwa hoteli kubwa jijini mwanza kitu nilichovutiwa nacho ukiachilia mbali mambo mengine ni kitanda kwani hakikuwa vile vitanda nilivyozoea kuviona, nikianza kwenye kitanda chenyewe ni kirefu siyo ile futi 6 tuliyoizoea nadhani kitakuwa ni futi 7 au 8 lakini pia godoro lenyewe ni lile la kiwango sana ni laini kiasi kwamba ukilala staili yoyote na lenyewe linakupeleka hivyo hivyo kiufupi halichoshi unalala usingizi mzuri sana.

Kwa anaefahamu je ni wapi vinapatikana hivi vitanda pamoja na magodoro yake au watu wa mahotel wanaagiza nje?
 
kitanda

mafundi wapo wanakuchongeshea ukubwa na design unayotaka. ingia mtandaon uchague design unayotaka mpelekeee fundi akutolee kwa vipimo mtakavyokubaliana.

Godoro
Baada ya kitanda kukamilika, unaenda kiwandani unatoa order ya godoro kutokana na vipimo vya kitanda chako.

Kulala.
Viweke pamoja afu anza kuvilalia, vitapendeza zaidi ukiwa unavilalia na shemeji yetu.
 
Nilihudhuria maonesho ya nane nane kwenye mabanda ya jkt na magereza, nikakuta kabati na vitanda, aisee ni vzr sio mchezo.
Ila bei nayo si ya kitoto, ujipange kwelikweli.
 
Ilikuwa ni mkoa gani mkuu?
 
Habari zenu wakuu, niliwahi kulala kwenye hoteli moja jijini mwanza ambayo ni miongoni mwa hoteli kubwa jijini mwanza kitu nilichovutiwa nacho ukiachilia mbali mambo mengine ni kitanda kwani hakikuwa vile vitanda nilivyozoea kuviona, nikianza kwenye kitanda chenyewe ni kirefu siyo ile futi 6 tuliyoizoea nadhani kitakuwa ni futi 7 au 8 lakini pia godoro lenyewe ni lile la kiwango sana ni laini kiasi kwamba ukilala staili yoyote na lenyewe linakupeleka hivyo hivyo kiufupi halichoshi unalala usingizi mzuri sana.

Kwa anaefahamu je ni wapi vinapatikana hivi vitanda pamoja na magodoro yake au watu wa mahotel wanaagiza nje?
Magodoro ya spring yapo kila mji uliochangamka.
Lakini ukija mlimani city utapata hadi kitanda kwa bei ya kununulia kiwanja
 
Back
Top Bottom