Nimefuatilia nyuzi zako kwa makini sana Mr's Abdul ningependa nikupongeze kwa juhudi zako na binafsi wewe ni mmoja kati ya watu ninao wakubali Sana katika jukwaa hili.
Pia nikupe pongezi kwa saccos yenu,itanufaisha wengi.
Binafsi Kama mjasiriamali siwezi kukopa kwa mtu bila kumrudishia na pesa ya nyongeza (riba) naona Kama namrudisha nyuma ki uchumi ....Naomba unisaidie Kama mfanya biashara Je upande wenu hamnufaiki na chochote?(faida) Na Kama hamnufaiki na chochote mnaweza vipi kuendesha saccos yenu?
Kwanza kabisa, asante sana kwa kauli zako njema.
Sisi tunafaidika sana, baadhi ya faida tunazonufaika nazo:
1) Sisi pekee tusingeweza kumudu miradi tunayoifanya nje ya saccos bila kushirikisha wawekezaji wengine ambao kila mwenye mtaji mdogo ambae alikubali wazo letu tumeingia nae ubia wa muda mfupi, ubia wa mradi kwa mradi.
Tunashukuru kwa muitikio na tukaweza kuanza mradi mdogo wa kwanza kwa kuwekeza kwa ubia kwa mtu kuwekeza kuanzia Shillingi 500,000.
Tukafanya vizuri kwa muda mfupi tukaendelea na mradi wa pili, nao tukafanya vizuri na kuweza kuongeza mradi mwengine wa uwekezaji wa kati. Kima cha chini kikawa million tano kwa mwekezaji. Nao ukafanya vizuri kwa muda mfupi sana.
Tukawa na miradi mitatu inayoenda sambamba. Wawekezaji wanafaidika na sisi tunafaidika kwa kuisimamia miradi na mtaji wetu mdogo unazaa sambamba na wengine.
Sasa tupo mradi wa nne, wa kwanza ulikamilika, wa pili, wa tatu na wa nne inakwenda sambamba na wa pili na wa nne tunatarajia itakamilika October. Wa tatu utaisha mwakani mwezi April.
Sasa tunaanza wa tano ndani ya miezi miwili ijayo. Huu utajumuisha wawekezaji wa kuanzia Shillingi million moja hadi million 30 kwa kila mwekezaji. Unakaribishwa.
2) Faida ya pili ni kuanzisha saccos rasmi ambayo itajumuisha wawekezaji wa kila mtaji, mdogo na mkubwa, na kuwekeza kwenye miradi mikubwa na midogo ambayo itajumuisha watendaji wa miradi (wana saccos wataokopa), wawekezaji ambao mitaji yao itatumika kukopesha.
Tunakopesha kwenye miradi ya maendeleo ambayo na sisi wenyewe tunakuwa wabia, faida tunagawana baina ya mkopaji na mkopeshaji.
3) faida kubwa zaidi ni kuwa na mtandao mkubwa ambao unajumuisha aina tofauti za utaalamu na miradi.
Natumai nimeeleweka.