Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Mimi nazungumzia wale wanaosema mfumo wa Islamic Banking kwamba unakopeshwa bila riba,kama wewe unaenda benki kukopa pesa ufanye biashara wakakupatia mfano million 1 lakini wakataka ukirudisha urudishe million 1.1 na wale wa Islamic Banking wanakununulia bidhaa unayotaka kwa kiwango kile kile kisha wakakukopesha ila ukilipa ulipe na nyongeza kidogo ndio nikasema yote ni yale yale.


Ninahisi kuwa kuna tofauti na namna ulivyoelezea, mfumo wa "Islamic Finance" nilivyouelewa ni kuwa, tuseme unataka kukopa million kumi kwa ajili ya biashara.

Kwanza itabidi hiyo biashara itazamwe mwenendo wake, unaweza kuleta faida au hapana, upo kihalali na unafata sheria za nchi au hapana, ni biashara ambayo ipo tayari na unaongeza unataka kuongeza mtaji au ni mpya na vigezo vingine ambavyo wataalamu wa biashara watavitazama kiundani, kuna "proper study" au hapana ya hiyo biashara. Ukikidhi vigezo vyote basi "financiers" wanaingia ubia na wewe. Na pesa watakazotoa ni mtaji wao na wako, mtaji wao utakuwa unawaingizia faida kutokana na asilimia ya faida kama taji wao ulivyo, na wewe unaingiza faida kwa mtaji uliopatiwa. Katika faida yako utakuwa unarudisha mtaji uliopewa kidogo kidogo kwa kadiri mlivyokubaliana mpaka urudishe mtaji kama ulivyopewa, bila ya wewe kuongezea hata senti moja ya riba.

Utaona kuwa "financiers" wanapata faida kutokana na mtaji waliowekeza na hakuna riba waliopokea wala kutoa.

Halafu tofauti nyingine na "financiers" wa riba, ni muda wa mkopo unaotakiwa ulipe utapokwisha riba hupanda na kuendelea kupanda. Tofauti na "financiers" bila riba, huwa hakuna riba inayoongezeka.

Wenye ujuzi zaidi wanaweza kuweka sawa zaidi au kusahihisha tulipokosea.

Asante.
 
na je lazima uweke dhamana? maana ukipata hasara wao wana recover vipi hasara yao? Mfano nahitaji mtaji wa operation kwa miezi sita. Ina maana watawalia wafanya kazi wangu kwa miezi na kupilipa bili zote kwa miezi sita? Hao huu mkupo ni kwenye rawa materials tu wao kukununulia?

Underlying Conditions for Success in Islamic Finance

“In the Islamic financial system, money does not earn any return without being legally converted into actual capital in collaboration with effort. The proportionate returns for the investor, who provides part of the actual capital to undertake an investment project, and the bank which, on behalf of the depositors, provides the remainder, depends upon several factors such as the priority of the project in terms of value added or increase in employment, the degree of risk involved, social interests, and the like. We will say more about these issues later.

Source: Collateral in Islamic Finance - IslamicBanker.com
 
Umejaribu kueleza kwa urefu kadri ulivyoweza na mimi nashukuru kwa ufafanuzi wako,lakini kwangu mimi tafsiri ni moja tu kwamba unataka kuanzisha au kuendeleza biashara yako lakini unataka usaidizi sasa haijalishi unapewa pesa au bidhaa au kitendea kazi lakini ukirudisha kuwe na ziada kidogo ambayo mnaweza kuiita jina lolote iwe riba,faida au vyovyote kadiri mtakavyokubaliana lakini kikubwa na ukweli ulio dhahiri hicho ulichopewa(iwe pesa au bidhaa) umekopeshwa.


Nionavyo ni tofauti sana, kukopa kama mkopo na kuulipia riba upate faida upate hasara pasi na mwenzako kuufanyia kazi yoyote ni tofauti na kukopa kwa kutafuta mtaji na anaekupa mtaji anaingia ubia na wewe na faida na hasara mnagawana.


Ninakusihi isome article hii: Collateral in Islamic Finance - IslamicBanker.com
 
ivi Zainab Tamim kwa nini tusiiweke katika mfumo wa SACCOS?

Najaribu kuwaza tu!


Ni wazo jema sana na mpaka sasa tunahisi itakuwa ni saccos itoayo mikopo bila riba.

Mjadala mpana unahitajika kwa njia sahihi na zisizovunja sheria na kanuni unahitajika ili tufikie huko.

Tunakaribisha maoni, ushauri, maswali ili tufanikiwe.
 
Tatizo Watalaamu wa Masuala Ya Fedha Hawaonekani,,,Labda Ndo Kasumba Yetu Watz Kutotoa Madini Tuliyonayo Kisa Atafaidika Fulani?
Tuacheni Jaman Fikra Hizo,,, Huu Ni Muda Wa Kujenga Taifa Lenye Umoja Na Mshikamano Na Ndio Tutafikia Malengo Makubwa.

Wazee Wa Zamani Walisema UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU,,, tukisaidiana wote kwa pamoja itafika muda kila mmoja wetu ana uwezo wa kusurvive,
Ni ushaur tu lakin msichukie!
 
Hapana labda unifafanulie kidogo?

Kuna hii ya zamani, nimeiona:

Mimi nilikuwa afisa ushirika nimekuwa kiongozi na mwanzilishi wa saccos kwa miaka 20. Sasa hivi natoa ushauri wa biashara NGO na SACCOS. SACCOS kirefu chake ni Savings and credit cooperative society. Kiswahili ni chama cha ushirika cha akiba na mikopo. naomba nikupe habari kamili katika taarifa hii hapa chini ili ujue nini unachotafuta kwenye SACCOS na historia yake. Kwa kifupi unataka kuanzisha asasi ya kifedha endelea kusoma mchakato unaohitajika

Watu wengi wanafikiri kufanya biashara ya fedha au kuanzisha taasisi za kifedha ni kazi ngumu. Hali siyo hivyo katika dunia ya sasa. Mfumo wa kifedha ninaozungumzia hapa siyo benki kubwakubwa za biashara. Ninazungmzia benki ndogondogo za wananchi, vikundi au vyama vya ushirika vinavyoendesha asasi za kifedha. Asasi hizi zinaitwa SACCOS au SACCA, SACCOS ni vyama vya ushirika vya akiba na mikopo na SACCA ni NGO zinazotoa huduma za kifedha. Kati ya asasi hizi SACCOS ndiyo ambayo ni rahisi kuanzisha. Historia ya vyama vya ushirika vya akiba na mkopo inanzia kipindi cha mapinduzi ya viiwanda huko Ulaya kutokana na ugumu wa maisha na ugumu wa upatikanaji wa mikopo toka benki kwa wanyonge, watu hawa wafanyakazi na wakulima wadogowadogo waliamua kuungana na kuchangisha fedha kidogokidogo na kisha kuanza kukopeshana. Hali hii hata hapa kwetu Tanzania iko hivyo. Wale wanyonge, wakulima na wafanyakazi siyo rahisi kupata mikopo benki. Hawawezi kukopa toka Benki kutokana na masharti magumu wanayowekewa na Benki. Suluhisho la Kujikwamua kiuchumi kwa wanyonge ni kuanzisha SACCOS. Mfumo huu wa SACCOS unaweza kuanziswa sehemu ambapo kuna mkusanyiko wa watu wanaofahamiana na wanafanya shughuli zinazofanana, kwa mfano wafanyaazi wa kampuni au ushirika fulani, wafanyabiashara wa sehemu fulani, wakulima wa vijiji fulani au waumini wa dhehebu au dini fulani wakiwa na nia hiyo wataitisha mkutano ambao utasimamiwa na Afisa Ushirika na kupitisha azimio la kuanzisha SACCOS. Watatuma maombi ya kusajili SACCOS na kuanza kuchangishana. Baada ya kupata usajili, kutoa mikopo kutahitaji subira kidogo ili mikopo itolewe baada ya chama kuwa na akiba ya kutosha baada ya kukusanya akiba ikianzia miezi mitatu hadi sita.

Mikopo inayotolewa itatozwa riba ya silimia 2.5 na inaweza kuwa ni ya dharura kwa ajili ya biashara, ujenzi, ufugaji na kilimo na kadhalika. Vyama hivi vimewasaidia sana wanachama wake kujikwamua kiuchumi. Faida ya kuvianzisha ni kwamba SACCOS inaweza kukopa toka Benki kama imesajiliwa na kutoa mikopo kwa wanachama wake. SACCOS ina wafundisha wanachama wake kuwa na tabia ya kuweka akiba. Zikiendeshwa kwa makini na uaminifu mkubwa SACCOS zinaweza kugeuka na kuwa Benki kamili na kumiliki vitega uchumi kama majego na magari na pia kutoa ajira. Matatizo ya biashara hii ni kukosekana kwa uaminifu kwa wanachama na viongozi katika masuala ya uendeshaji na utoaji mikopo, hivyo kufanya vyama hivi kutokuwa na maendeleo. Ufumbuzi wa matatizo ya SACCOS ni kutoa elimu ya ushirika ili kuwe na mwamko wa wanachama katika kusimamia uendeshaji wa vyama hivi.

Kwa ushauri zaidi nipigie 0755394701
 
Mimi nazungumzia wale wanaosema mfumo wa Islamic Banking kwamba unakopeshwa bila riba,kama wewe unaenda benki kukopa pesa ufanye biashara wakakupatia mfano million 1 lakini wakataka ukirudisha urudishe million 1.1 na wale wa Islamic Banking wanakununulia bidhaa unayotaka kwa kiwango kile kile kisha wakakukopesha ila ukilipa ulipe na nyongeza kidogo ndio nikasema yote ni yale yale.
Kuna tofauti mkuu, riba haiangalii hasara, upate hasara au upate faida ni lazima ulipe riba na inachajiwa kila mwaka, na pia lazima ulipe kile ulichokopa.
Mfumo wa Islamic Finance ni tofauti, wao ni kama wanatumia mfumo wa hisa katika biashara kwa muda maalumu mtakaokubaliana kisha baada ya hapo unaachiwa biashara inakuwa yako peke yako. Mfumo huu wa kiislamu hasara ikipatikana wewe uliokopeshwa hutadaiwa kwasababu hiyo ni biashara yenu wote kwa muda maalum. Mnachogawana ni faida ya biashara husika mpaka yule aliyekukopesha atakaporudisha pesa yake na faida kidogo kisha anakuachia biashara inakuwa yako peke yako kama mlivokubaliana. Mfano ni wa kuwapa vijana bodaboda kwa mikataba, huu mfumo ni kama kumkopesha kijana bila riba yeye anapata kitu kwa biashara ile kila siku na wewe unapata na baada ya muda maalumu mliokubaliana kijana anabaki na pikipiki yake. Jee hii ni riba?? Hii si riba bali ni faida ya biashara. Kuna tofauti ndogo kati ya faida na riba, usipokuwa makini utachanganya hivi vitu viwili.
 
Ndio Yale yale
Sio yaleyale mkuu hiyo si kweli. .mfanya biashara hununua bidhaa kwa bei fulani na kuuza kwa bei ya juu kidogo, unataka kusema hiyo ni riba?? Laa, hiyo si riba bali hiyo ni faida ya biashara. Ndivyo mfumo wa islamic financing ufanyavyo kazi. Taasisi inakupatia bidhaa fulani kwa faida fulani ambayo wao wanapata. Ni kama vile wamekuuzia kwa mkopo. Na kama tujuavyo ukinunua kitu kwa mkopo bei inakuwa juu kidogo tofauti na ukinunua kwa cash. Tufahamu kuwa unapokopa kwa riba, ukishindwa kulipa katika muda uliowekwa deni lako linaendelea kuongezeka kila mwezi na kila mwaka, Suala hili kwenye Islamic finance halipo kabisa. Ukifungua uelewa wako utaelewa tofauti hizi japo ni ndogo lkn umuhimu wake ni mkubwa sana katika ulimwengu wa biashara na mikopo. Na usipoamua kuelewa, hutaelewa kwakuwa umeamua iwe hivyo.
 
Back
Top Bottom