Pritty wa joseph
JF-Expert Member
- Jul 17, 2014
- 2,379
- 2,047
Hapo ndo nimemaliza mkuuTafadhali tufafanunulie huo mpango wako ili tuuelewe zaidi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo ndo nimemaliza mkuuTafadhali tufafanunulie huo mpango wako ili tuuelewe zaidi.
0714547830Tusamehe sana kwa usemi wetu "hakuna", ni kutokuelewa kwetu. Tunafuta usemi huo.
Tunaomba sana tuwasiliane aidha hapa au kwenye whatsapp ili tuone namna tunavyoweza kushirikiana na kubadilishana uzoefu.
Mimi nazungumzia wale wanaosema mfumo wa Islamic Banking kwamba unakopeshwa bila riba,kama wewe unaenda benki kukopa pesa ufanye biashara wakakupatia mfano million 1 lakini wakataka ukirudisha urudishe million 1.1 na wale wa Islamic Banking wanakununulia bidhaa unayotaka kwa kiwango kile kile kisha wakakukopesha ila ukilipa ulipe na nyongeza kidogo ndio nikasema yote ni yale yale.
Hapo ndo nimemaliza mkuu
na je lazima uweke dhamana? maana ukipata hasara wao wana recover vipi hasara yao? Mfano nahitaji mtaji wa operation kwa miezi sita. Ina maana watawalia wafanya kazi wangu kwa miezi na kupilipa bili zote kwa miezi sita? Hao huu mkupo ni kwenye rawa materials tu wao kukununulia?
good idea,,,
Naomba nami niwemo ndani niweze kujifunza practically,
Mkuu Zainab Tamim kwa hili tuko pamoja
PLEASE NAOMBA USINISAHAU.
Umejaribu kueleza kwa urefu kadri ulivyoweza na mimi nashukuru kwa ufafanuzi wako,lakini kwangu mimi tafsiri ni moja tu kwamba unataka kuanzisha au kuendeleza biashara yako lakini unataka usaidizi sasa haijalishi unapewa pesa au bidhaa au kitendea kazi lakini ukirudisha kuwe na ziada kidogo ambayo mnaweza kuiita jina lolote iwe riba,faida au vyovyote kadiri mtakavyokubaliana lakini kikubwa na ukweli ulio dhahiri hicho ulichopewa(iwe pesa au bidhaa) umekopeshwa.
Patamu hapa!Kwa sisi wazee wa fursa mambo haya huwa haturuhusu yatupte.
Ikiwa vp naomba nami niwepo tagadhar
Nadhani Hii Ndo Itakuwa Njia BoraZaidiNi wazo jema sana na mpaka sasa tunahisi itakuwa ni saccos itoayo mikopo bila riba.
Mjadala mpana unahitajika kwa njia sahihi na zisizovunja sheria na kanuni unahitajika ili tufikie huko.
Tunakaribisha maoni, ushauri, maswali ili tufanikiwe.
Nadhani Hii Ndo Itakuwa Njia BoraZaidi
Hapana labda unifafanulie kidogo?Asante, wacha tuendelee kujadili na tuone mawazo mengine kuna mtu nilikuwa ninaongea nae kwa simu ameongelea kuhusu SACCA, una uelewa wowote kuhusu SACCA?
Hapana labda unifafanulie kidogo?
Hapana labda unifafanulie kidogo?
Mimi nilikuwa afisa ushirika nimekuwa kiongozi na mwanzilishi wa saccos kwa miaka 20. Sasa hivi natoa ushauri wa biashara NGO na SACCOS. SACCOS kirefu chake ni Savings and credit cooperative society. Kiswahili ni chama cha ushirika cha akiba na mikopo. naomba nikupe habari kamili katika taarifa hii hapa chini ili ujue nini unachotafuta kwenye SACCOS na historia yake. Kwa kifupi unataka kuanzisha asasi ya kifedha endelea kusoma mchakato unaohitajika
Watu wengi wanafikiri kufanya biashara ya fedha au kuanzisha taasisi za kifedha ni kazi ngumu. Hali siyo hivyo katika dunia ya sasa. Mfumo wa kifedha ninaozungumzia hapa siyo benki kubwakubwa za biashara. Ninazungmzia benki ndogondogo za wananchi, vikundi au vyama vya ushirika vinavyoendesha asasi za kifedha. Asasi hizi zinaitwa SACCOS au SACCA, SACCOS ni vyama vya ushirika vya akiba na mikopo na SACCA ni NGO zinazotoa huduma za kifedha. Kati ya asasi hizi SACCOS ndiyo ambayo ni rahisi kuanzisha. Historia ya vyama vya ushirika vya akiba na mkopo inanzia kipindi cha mapinduzi ya viiwanda huko Ulaya kutokana na ugumu wa maisha na ugumu wa upatikanaji wa mikopo toka benki kwa wanyonge, watu hawa wafanyakazi na wakulima wadogowadogo waliamua kuungana na kuchangisha fedha kidogokidogo na kisha kuanza kukopeshana. Hali hii hata hapa kwetu Tanzania iko hivyo. Wale wanyonge, wakulima na wafanyakazi siyo rahisi kupata mikopo benki. Hawawezi kukopa toka Benki kutokana na masharti magumu wanayowekewa na Benki. Suluhisho la Kujikwamua kiuchumi kwa wanyonge ni kuanzisha SACCOS. Mfumo huu wa SACCOS unaweza kuanziswa sehemu ambapo kuna mkusanyiko wa watu wanaofahamiana na wanafanya shughuli zinazofanana, kwa mfano wafanyaazi wa kampuni au ushirika fulani, wafanyabiashara wa sehemu fulani, wakulima wa vijiji fulani au waumini wa dhehebu au dini fulani wakiwa na nia hiyo wataitisha mkutano ambao utasimamiwa na Afisa Ushirika na kupitisha azimio la kuanzisha SACCOS. Watatuma maombi ya kusajili SACCOS na kuanza kuchangishana. Baada ya kupata usajili, kutoa mikopo kutahitaji subira kidogo ili mikopo itolewe baada ya chama kuwa na akiba ya kutosha baada ya kukusanya akiba ikianzia miezi mitatu hadi sita.
Mikopo inayotolewa itatozwa riba ya silimia 2.5 na inaweza kuwa ni ya dharura kwa ajili ya biashara, ujenzi, ufugaji na kilimo na kadhalika. Vyama hivi vimewasaidia sana wanachama wake kujikwamua kiuchumi. Faida ya kuvianzisha ni kwamba SACCOS inaweza kukopa toka Benki kama imesajiliwa na kutoa mikopo kwa wanachama wake. SACCOS ina wafundisha wanachama wake kuwa na tabia ya kuweka akiba. Zikiendeshwa kwa makini na uaminifu mkubwa SACCOS zinaweza kugeuka na kuwa Benki kamili na kumiliki vitega uchumi kama majego na magari na pia kutoa ajira. Matatizo ya biashara hii ni kukosekana kwa uaminifu kwa wanachama na viongozi katika masuala ya uendeshaji na utoaji mikopo, hivyo kufanya vyama hivi kutokuwa na maendeleo. Ufumbuzi wa matatizo ya SACCOS ni kutoa elimu ya ushirika ili kuwe na mwamko wa wanachama katika kusimamia uendeshaji wa vyama hivi.
Kwa ushauri zaidi nipigie 0755394701
Kuna tofauti mkuu, riba haiangalii hasara, upate hasara au upate faida ni lazima ulipe riba na inachajiwa kila mwaka, na pia lazima ulipe kile ulichokopa.Mimi nazungumzia wale wanaosema mfumo wa Islamic Banking kwamba unakopeshwa bila riba,kama wewe unaenda benki kukopa pesa ufanye biashara wakakupatia mfano million 1 lakini wakataka ukirudisha urudishe million 1.1 na wale wa Islamic Banking wanakununulia bidhaa unayotaka kwa kiwango kile kile kisha wakakukopesha ila ukilipa ulipe na nyongeza kidogo ndio nikasema yote ni yale yale.
Sio yaleyale mkuu hiyo si kweli. .mfanya biashara hununua bidhaa kwa bei fulani na kuuza kwa bei ya juu kidogo, unataka kusema hiyo ni riba?? Laa, hiyo si riba bali hiyo ni faida ya biashara. Ndivyo mfumo wa islamic financing ufanyavyo kazi. Taasisi inakupatia bidhaa fulani kwa faida fulani ambayo wao wanapata. Ni kama vile wamekuuzia kwa mkopo. Na kama tujuavyo ukinunua kitu kwa mkopo bei inakuwa juu kidogo tofauti na ukinunua kwa cash. Tufahamu kuwa unapokopa kwa riba, ukishindwa kulipa katika muda uliowekwa deni lako linaendelea kuongezeka kila mwezi na kila mwaka, Suala hili kwenye Islamic finance halipo kabisa. Ukifungua uelewa wako utaelewa tofauti hizi japo ni ndogo lkn umuhimu wake ni mkubwa sana katika ulimwengu wa biashara na mikopo. Na usipoamua kuelewa, hutaelewa kwakuwa umeamua iwe hivyo.Ndio Yale yale