IJUE SIASA, USHOGA NA NGENDEMBWE ZAKE!!
Na: Suphian Juma Nkuwi
Salaams!!
Nimekwepo kwenye siasa takribani muongo mmoja sasa. Nimefunza Siasa kwa kuitenda na naendelea kujifunza. Ni sahihi kusema Siasa ndio nguzo kuu iongozayo Nchi. Kila maamuzi ya Siasa humgusa kila mtu kwa kupenda ama kutokupenda, moja kwa moja ama 'indirectly'.
Changamoto kubwa ambayo naiona ni namna wafuasi wa wanasiasa wanavyoitafsiri Siasa. Wengi wana alama sikitishi katika somo la siasa. Hawaijui siasa kindakindaki nje ya kusoma machapisho mtandaoni ya Siasa na Wanasiasa na kuishi na majumuisho ya jumla jumla juu ya wanasiasa, na hata kubaki na makasiriko na chuki dhidi ya wanasiasa wasio katika upande wao ama hisia zao.
Mimi ni mhanga wa eneo hili. Wengi wa Marafiki, jamaa na ndugu zangu hupata tabu na hata wengine kufika pahala kunisihi niache siasa kisa taarifa potofu, matusi na vitisho dhidi yangu kwenye mijadala. Wasijue hata ukiacha siasa ukaenda kulima viazi vitamu Ikungi, viazi vataliwa na nguruwe pori, wezi wataiba na wadudu watayashambulia. Kiufupi kila kazi ina changamoto. Hakuna kukimbia changamoto.
Hivyo Leo naomba nitoe darasa fupi kuhusu Siasa na gharama zake. Nitaomba kusamehewa kama nitakuwa muwazi sana. Lengo ni kuepusha kiitwacho; uwongo usipodhibitiwa huweza kugeuka na kuaminiwa na kubebwa mioyoni kama ukweli.
Ipo hivi:
Unapokuwa Chama cha Upinzani, it's obvious Wapinzani wako ni Chama Tawala. Hivo hivyo Unapokuwa Chama Tawala Wapinzani wenu ni vyama vya Upinzani. Lengo lenu kuu ni moja; "kushika dola" (madaraka). Mtaji wenu mkuu ni wananchi. Hakuna pande itakayofurahi pande nyingine ipendwe na wananchi. Kila pande lazima iwe bize kuishinda imani ya wananchi, na kudhoofisha pande nyingine. Huu ndio uhalisia.
Sasa wafuasi wa kila pande lazima watetee pande zao. Ukiwa mbele (front) kutetea kama Suphian lazima udhoofishwe kwa namna yoyote ile ikiwemo kusingiziwa vitu hasi (negative)..Matusi na kuitwa kila majina ya fedheha lengo ni moja tu ni kukufanyia "political psychological assassination" yaani kukuathiri kisaikolojia ili urudi nyuma ukose uhalali (legitimacy) ya kutetea upande wako na hivyo upande wako ukose Sifa bora (credit) mbele ya umma.
Wanauliza; "Kwanini Suphian unasemwa sana pengine kuliko wanasiasa wengine?" Jibu ni rahisi; Kwasababu nipo mbele (front) sana kutetea upande wangu kwenye macho ya wengi (hususani mitandao ya kijamii). Formula ni rahisi mwanasiasa ukikaa kimya na Wapinzani wako nao wanakaa kimya dhidi yako. Uwiano (Rate) wa kuwapinga Wapinzani wako ndio uwiano (rate) huohuo au zaidi wa kupingwa na wa hao Wapinzani wako pia. That's simple mathematics.
Kwahiyo mimi Suphian nilipokwepo Upinzani ilikuwa kawaida upande wa Chama Tawala wanidhoofishe ndio maana Musiba alitunga uwongo wa kunichafua na hili suala la Ushoga kupitia gazeti lake la Tanzanite.. Na wakati huo Wapinzani wa Chama Tawala akiwemo Mange Kimambi, hao vijana wa CHADEMA akina Martin walimlaani sana kwa kunichafua, lakini cha kushangaza, leo hii hao hao Wapinzani na wafuasi wao wanatumia njia hiyohiyo ya kuniita shoga kunichafua. Kiufupi wanakula matapishi yao.
Maana hawana hoja zingine za maana za kunichafua mbele ya Uma. Na ikumbukwe sakata la Ushoga ndio limeshika kasi sasaivi kwahiyo wanajua ukimsema mtu Shoga atakosa maana kwa watu. Ndivyo propaganda za siasa zilivyo.
Msishangae sasa wanatembea na narrative kwamba kila mfuasi wa Rais ama Chama Tawala akinyenyua mdomo tu anaambiwa anatafuta uteuzi mara sijui anajipendekeza, tujiulize toka lini uteuzi umekuwa kitu kibaya? Si njia tu kama njia zingine za kutumikia umma? Kujipendeza? How? Which? Who? Mimi kusimama na upande wangu najipendekeza? Yaani ntupo kijiweni tukakunywa kahawa nimsifie mke wangu ni mrembo na ana maadili, uniambie najipendekeza? Sawa najipendekeza, jipendekeze na wewe kwa wako au upande wako. ACHA WIVU.
Mbona wao kutwa wanatetea na kusambaza kazi za vyama vyao na viongozi wao hatuwaambii wanajipendekeza? Mbona wanateuliwa kwenye vyama vyao hatuwanangi?
Ndugu wasomaji ndio muelewe hizi zinaitwa "propaganda tactics" za kudhoofisha pande pinzani zikose uhalali kwa Umma.
Sasa nipo CCM tangu Desemba 31, 2020, naitetea na kuisema vizuri CCM na kuhabarisha na kuzitetea Juhudi za maendeleo zisizomithilika za Rais na Mwenyekiti wa Chama chetu cha Mapinduzi CCM Daktari Samia Suluhu Hassan. Mnatarajia nipongezwe na Wapinzani wake? Wapinzani wa CCM wanipongeze? HAPANA.
Ni lazima nitukanwe na watu/pande zote pinzani kwa Rais na CCM na ndio maana Mange na wenzake wananitukana baada ya kuwakemea walipomtukana na kuutweza utu wake Rais wetu kwenye sakata la Bandari ambalo kiuhalisia linaenda kuleta Mapinduzi ya kihistoria katika kunufaika na uwekezaji bandarini kinyume na propaganda zinazoenezwa kwamba bandari inauzwa.
Aidha ndugu wasomaji ifahamike kutukanwa huchaguliwi tusi wala huwezi kutuma maombi ya namna ya kuchafuliwa.. Sasa imagine..Mange Kimambi kaweka picha yangu nimefuga kucha ambayo nilipiga wakati nipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) miaka 10 huko na nikiwa nimefuga dred, na wakati huo nilikuwa Mtangazaji wa Mlima TV kipindi cha wasanii (Muziki na Maisha)...So ilikuwa kawaida kuwa na mwonekano huo kuakisi kipindi hicho na pia nilikuwa najihusisha na mambo ya mtindo.
Picha nyingine ni ile nimejifunika shuka la kimasai ameizoom kama vile nimesuka rasta.. Uwongo Sijawahi kusuka rasta maishani. Ni kawaida sana hata wewe ukitembelea kwenye gallery za wamasai Arusha unaweza kuvaa hizo shuka ukapiga picha.
Kupitia Makala hii pia naomba niwahakikishieni (kwa wale wenye mashaka).. Naaapa kwa Mungu wetu; Sijawahi na namwomba Mungu sana isije ikatokea niwe Shoga. Na hata kuzungumzia tu Ushoga huwa napata kichefuchefu. Na naumia sana nikiona wanaume wanafanya wanafanya ujinga huo. Nipo vizuri kimwili, nina mchumba wangu na Mungu akipenda nitafunga nae ndoa karibuni. Inshallah!!
Hivyo ni vizuri sote huku tukaelewa mambo haya. Katika mambo mabaya watu wanapenda kujizungumzia jinsi walivyo kwa kutumia nafsi ya mtu mwingine.
Ni vizuri sasa tutambue Mheshimiwa Rais ameturejeshea na kuimarisha uhuru wa Kujieleza kuliko wakati wowote ule tangu tupate uhuru. Hamuoni yeyote anafungwa, kutekwa ama kuuawa kisa amemkosoa ama kumtukana Rais na Serikali yake. Kiongozi wa namna hii nisipende? Ndio maana rafiki yangu mmoja juzi ananiambia: Suphian huna ushabiki na Rais Samia, una mahaba na Rais Samia akidai Siambiki unapokuja mjadala wa kumsema vibaya. Yes she deserves it.
Uungwana huu wa Rais Samia nawaomba tuutumie vema. Ifahamike Dictators are also made from innocent leaders via abusive critics. Viongozi wema huweza kutengenezwa kuwa madikteta kupitia midomo michafu. Hivyo Tukosoe kwa staha, tusifie kwa staha, tujenge Nchi yetu pamoja.
Otherwise NAWAPENDA nyote ndugu zangu Watanzania.
Mungu ibariki Tanzania.
Ahsanteni.
Suphian Juma Nkuwi,
Kada-CCM,
Singida,
Juni 14, 2023
Namba: 0717027973
View attachment 2657239