✳️SANAA NA WASANII NDIO KITOVU CHA KUPOROMOKA KWA MAADILI NCHINI TANZANIA
👉(UHAMASISHAJI WA USHOGA NA USAGAJI )
🌐Na:Shujaa©️®️Ⓜ️
Ni muhimu kufahamu kutokana na nguvu kubwa ya sanaa na wasanii katika jamii,kumekuwepo na agenda nyingi kubwa nyuma yake zenye lengo la kupenyeza tamaduni za kigeni na kuhamasisha na kuchochea vitendo viovu kama Ushoga na Usagaji, Uzinzi & Uasherati, Talaka (Divorce), Movie za mazombi n.k ili vionekane ni vitu vya kawaida katika jamii
Mpango au Agenda iliyopo ulimwenguni sasa ili kupenyeza vitendo hivyo, ni kutumia sanaa na wasanii wenye mvuto na wanaokubalika katika jamii husika, na kupitishia kwao aidha kwa kuigiza au kwa kuimba n.k .Na hapa ndipo wasanii wengine kwa kujua kabisa wanachokifanya ni uhamasishaji wa kazi walizotumwa kuzifanya na wengine kwa kutokujua ila kwa kuiga tu tamaduni za kigeni zenye uchafu nyuma yake
Moja ya mambo makubwa yanayochangia kuporomoka kwa maadili yetu ya Kiafrika na kitanzania ni ukosefu wa udhibiti wa kazi za sanaaa nchini na ndio umechangia kuongezeka tabia mbovu kwa kuiga tamaduni ambazo sio asili yetu wala desturi zetu na kuziingiza nchini.
Ni kweli kabisa, kazi ya sanaa na wasanii imetumika sana kuelimisha, kuburudisha na hata kufundisha jamii mambo mengi mazuri, pia tukumbuke kazi ya sanaa sio tu kuelimisha na kufundisha lakini pia inatumika sana kuhamasisha na kuchochea watu kupenda maisha ya wasanii wanayoyaonyesha katika sanaa zao na tabia zao .Na jamii yetu inaharibika pale wanapoona wasanii kama kioo cha jamii wakifanya vitendo fulani kinyume na maadili yetu, wadau wao hupenda kuiga kuvaa kama wao,kunyoa kama wao,kuishi kama wao n.k
🕹️Kwa mfano katika Tasnia ya sanaa ya mziki,leo hii utawaona wasanii wakiume kama akina Diamond, Ali kiba , Harmonize wakiimba jukwaani wakiwa wamevaa sketi za kike, wengine wamesuka nywele,kuvaa mikufu na heleni kama wanawake mpaka unajiuliza wanavyovaa vinauhusiano gani na kazi ya sanaa?.Pia katika show zao au video zao zina wanenguaji na wahusika wengine wamevaa nusu uchi wakiwa wanafanya mapenzi katika nyimbo hizo, na je hayo huo muonekano wa tu unahusiano gani na sanaa? .Na mbaya zaidi maneno wanayoimba mengine ni matusi na ya kuhamasisha mapenzi mfano nyimbo ya Nyege nyegezi, Nyimbo ya peleka moto, mpelekee moto zinafundisha nini zaidi ya kuharibu vijana na watoto . Lakini ukiuliza ndio utaambiwa ni kazi ya sanaa imekua…. Utakuja kugundua kuna watu wanatumia sanaa vibaya kupitishia agenda zao, Kwani maudhui na vitendo vinavyofanyika havihusiani kabisa na kazi ya sanaa
📹Na katika Tasnia ya sanaa ya Uigizaji,ndio imehusika kwa sehemu kubwa kuharibu vijana na jamii kubwa.Mfano leo hii tunamuona Joti na comedian wengine wanaigiza ki-kike kike na kuvaa uhusika wa mwanamke ilihali wao ni wanaume, wengine tunaona ni kitu cha kawaida na kuita ndio sanaa yenyewe ila wala havina uhusiano wowote na sanaa ,hatujui nyuma yake vimebeba hamasa kubwa na vichocheo vikubwa kama Uhamasishaji wa ushoga, Uhamasisha wa kuzoelea ushetani, uhamasishaji wa kufanya mapenzi n.k
Kwa mfano, ebu jiulize swali hili mwenyewe, Je! Ikiwa wewe ni mwanaume msanii na unafanya hicho unachoitwa sanaa,Je unaweza kuigiza wewe ni mwanamke malaya ambaye katika kuigiza kwenu tunaona wanaume wenzio wanakushika shika makalio kama sehemu ya igizo wakikuchezea⁉️.Jibu ni jepesi kama kweli wewe sio shoga, hutaweza kukubali kufanya sanaa ya namna hiyo maana inadhalilisha hata utu wako lakini pia inahamasisha vitendo vingine vya uchafu
Ili kulinda jamii yetu dhidi ya huu mmong'onyoko wa maadili ,Serikali inapaswa kuweka mipaka ya kipi kinafaa na kipi hakifai kulingana na tamaduni zetu zilizo katika maadili mema ya nchi zetu za kiafrika sio kuruhusu Wasanii kuiga kila kitu katika tamaduni za ughaibuni na sio kuruhusu kila kazi ya sanaa kufanyika katika nchi yetu bila kuangalia maudhui yake ikiwa haitaweza kuathiri jamii yetu au bila kuangalia kama inaendana na utamaduni wetu.
Lakini pia huwezi kufundisha watu wasifanye ushoga kwa kuigiza ushoga ukoje kwa hicho unachokiita ni sanaa. Sio kila sanaa inayoweza kuelimisha na kufundisha jamii,tunaweza tukairuhusu kufanyika katika nchi yetu hata kama nia ya sanaa hiyo ni njema kabisa, ni ili kuonya jamii isifanye kwa mfano huo unaoigizwa, ila ikiwa ndani yake inaonyesha viashiria kama vya ushoga na usagaji au vinaonyesha tabia ambazo zipo kinyume na maadili yetu,bado sanaa hiyo Serikali inapaswa kuipiga marufuku haraka
Ikiwa Serikali yetu ya Tanzania haitaweka udhibiti wa kutosha na limitation katika sanaa zetu na kuruhusu chochote kufanyika kwa madai eti ni kazi ya sanaa basi tutazidi kukiharibu kizazi chetu cha sasa na kijacho.Hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwepo na hatari za kuingia kwa ushoga na usagaji nchini, ndio serikali inapaswa zaidi kuweka sheria na adhabu kali kwa wasanii wote watakaohusika kuonyesha viashiria vyovyote vibovu katika sanaa zao kinyume na tamaduni zetu ikiwa ni pamoja na kuwafungulia kesi, kuwafutia usajili wao wa kazi za sanaa
🌐Na: Shujaa©️®️Ⓜ️
stmwaisembac@gmail.com
0712054498