Vitenge na kanga vyasambazwa nchi nzima kuelekea siku ya wanawake Duniani, kete nzuri kuelekea 2025

Vitenge na kanga vyasambazwa nchi nzima kuelekea siku ya wanawake Duniani, kete nzuri kuelekea 2025

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Wanawake wa Tanzania wamepewa kanga zakutosha na vitenge kuelekea siku ya wanawake Duniani.

Wanawake wengi wamejipanga Kuvaa vitenge kusherekea siku ya wanawake Duniani.

Wanawake wengi watabeba mabango yaliyobeba ujumbe wa kisiasa kuhusu mwanamke mwanasiasa.

Wanawake wengi watalipwa kushiriki maadhimisho kutoka serikalini Hadi vyama vya siasa.

Hoja yangu, ni lini wanawake watavaa kanga na mabango yanayozungumzia matatizo yao na watoto wao? Lini wataacha kumsifia mwajiri wakati kwenye korido wanalalamika Hali ngumu? Nani atathubutu kubeba Bango lenye ujumbe sahihi kuhusu Kero za wanawake?

Uhuru wa fikra, shibe ya muda mfupi na unafiki viwe dira kumsaidia mtawala kujua ukweli kuhusu watawaliwa.
 
Sidhani kama hizo khanga na vitenge watapewa bure kwani niliko kuna hamasa kubwa ya kuhamasisha akina mama watoe 20000 kwa ajili ya kununua hivyo vitenge
 
Watu na mipango yao, Mungu na mipango yake
 
Back
Top Bottom