ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,424
- 4,954
Katika vitengo vinavyoongoza kwa Rushwa katika ofisi nyingi za TANESCO ni katika mtiririko hapa chini kulingana na ukubwa wa TATIZO, na pia utaweza kufahamu mikoa ya KITANESCO inayoongoza kwa Rushwa
1. Kitengo Cha Kuungia wateja umeme kwamaana ya wenye nguzo na wasio na Nguzo: hichi ndo kitengo kinachoongoza kwa Rushwa katika Ofisi za TANESCO, kwani wafanyakazi wa hichi kitengo wanajikusanyia feza nyingi sana zisizo halali kutoka kwa wateja, wengi wanalazimika kutoa Rushwa Ili wapate huduma haraka, hii inatokana na shirika kuwa na uwezo mdogo wa kuhudumu kundi kubwa la wateja wanaotaka huduma, sasa bajeti ndogo inayopangwa inawapa nguvu watendaji wa Tanesco kuchagua wa kumuhudumia kulingana na fedha anayotoa mteja, mathalani wanaohitaji umeme ni watu 3000, unapewa bajeti ya watu 500, Sasa hapo ukitoa pesa unahudumiwa bila kuwa na utaratibu wa FIFO, feza zinazotolewa ni kubwa lakini mgao unapita kwa wengi kuanzia wa ofisini hadi kibarua anayejenga
2. Kitengo Cha Upimaji/survey: Hawa wananuka Rushwa, kitengo hiki cha tanesco hakina tofauti na trafki, wanakula Rushwa kana kwamba hawalipwi mshahara, hii inatokana na mazoea, upungufu wa wafanyakazi, magari kwa hiyo ataenda kuhudumia kwanza anapoweza kupewa pesa ya ziada wengine wanakodiwa Hadi teksi.
3. Suala la kukatika katika umeme kwa Tanesco ni dili, na hapa ndo kinakuja kitengo Cha dharura/emergency hii katika katika umeme huwa inawapanikisha wateja hasa wa biashara mfano samaki, sasa kuliko samaki aoze bora atoe Rushwa, kwakuwa umeme unakatika kwa watu wengi kwa wakati mmoja na watendaji ni wachache emergency wanachagua wa kumuhudumia japo Kuna utaratibu wa kazi ipi ipewe kipaumbele.
4. Kitengo Cha mita: kwa vile Watanzania wengi wanapenda kitonga, kitengo hiki kimewekwa kutafuta wezi wa umeme, sasa mafundi wasio waaminifu wakikamata mwizi wa umeme wanamalizana nae huko huko, hiki ni kitengo chenye Rushwa kubwa Sana Mana viwanda vingi huwa vinaiba sana umeme, mikoa yenye viwanda TANESCO wanapiga sana hela kupitia kitengo hiki.
Hapo juu matendo hayo maovu ya Rushwa yanaongoza katika mikoa inayoitwa mikoa mikubwa KITANESCO yaani mikoa daraja la juu, ambapo Ina wateja wengi sana na mapato yao ni makubwa mno na ni mikoa yenye watu wenye feza, mikoa inayoongoza kwa Rushwa bila kufuatilia mpangilio wa utajaji ni DODOMA, MWANZA, KILIMANJARO, ARUSHA, DAR (TEMEKE, ILALA, KINONDONI S/N), MBEYA, PWANI.
Na mikoa ambayo Rushwa haipo sana na hii ni kutokana na udogo wa mkoa kwa kuwa na wateja wachache hivyo mahitaji ni machache na Ni rahisi kuhudumu ni RUKWA, KATAVI, RUVUMA, MANYARA
NB: Hapa imeongelewa Rushwa ya wateja tu, kuna rushwa za juu za Mambo ya manunuzi wanaelewa wenyewe, Makamba nakushauri weka watu wako katika Ofisi hizi watakuletea riport kamili, shirika limekuwa kama la wafanyakazi, huduma mpaka utoe Rushwa.