SoC04 Vitengo vya masoko vya mashirika ya umma na binafsi visimamiwe na wasomi kutoka jamii za wanaojua kuendesha biashara Ili kuongeza ufanisi

SoC04 Vitengo vya masoko vya mashirika ya umma na binafsi visimamiwe na wasomi kutoka jamii za wanaojua kuendesha biashara Ili kuongeza ufanisi

Tanzania Tuitakayo competition threads

La3

Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
17
Reaction score
17
Kumekuwa na changamoto ya kukosekana kwa ufanisi katika uendeshaji wa mashirika mbalimbali ya uma na makampuni binafsi hapa nchini Tanzania kwa muda mrefu sasa.

Ndio maana kuna mashirika kadhaa ya serikali yalibinafsishwa mfano, viwanda kama zana za kilimo (zzk) kule Mbeya ambacho hakifanyi kazi hata Sasa, kiwanda cha nguo songwe viwandani Mbeya ambacho kilishafungwa pia (hakuna uzalishaji), Pamoja na viwanda vingine katika mikoa mbalimbali nchini.

Pia kuna wakati ripoti ya CAG ilionyesha shirika la ndege ATCL linajiendesha kihasara.

Changamoto hizi zinasababishwa na ukosefu wa watu sahihi wanaosimamia vitengo vya masoko vya mashirika haya. Idara ya masoko ndio uhai wa makampuni na mashirika haya ya uma na binafsi.

Sasa kunahitajika umakini wa hali ya juu katika kutafuta watu sahihi watakaosimamia vitengo vya masoko na biashara vya mashirika ya uma na makampuni binafsi.

Kuna mashirika mbalimbali ya uma mfano kampuni ya simu TTCL, mashirika ya reli mfano TRC na TAZARA, Bandari, shirika la ndege ATCL, na makampuni mbalimbali binafsi.

Sasa maoni yangu ninayopendelea kuyatoa ni haya; Katika nchi yetu kuna watu kutoka makabila ambayo ni maarufu kwa biashara mfano wachaga, wakinga, waha na pia kwenye kila kabila kuna ukoo ambao ni maarufu kwa biashara.

Lakini pia kuna watanzania wenye asili ya bara Asia ambao ni maarufu kwa biashara nao ni vema wasomi ambao wanatokea jamii yao wakatumika kuendesha vitengo mbalimbali vya masoko vya mashirika haya.

Kama kuna wasomi wa masuala ya biashara kutoka makabila haya ambayo ni maarufu kwa biashara ni vema wakapewa kipaumbele kwa sababu biashara ni kipawa chao walichobarikiwa na MUNGU nina uhakika watafanya vizuri zaidi kuliko watu wa jamii nyingine.

Nini maana yake?
Katika nchi yetu kuna watu wa makabila mbalimbali ambao MUNGU kawabariki vipawa tofauti tofauti mfano wafugaji kuna, wasukuma, wagogo, wabarbaig, wanyamwezi, wasukuma n.k pia kuna wanaoishi jirani na maziwa na bahari ni maarufu kwenye eneo la uvuvi, Wakurya wengi wapo jeshini na polisi. Na makabila mengine kadri MOLA alivyowapa vipawa, wapo wakulima n.k

Sasa ili vitengo vya masoko vya mashirika mbalimbali ya uma na makampuni binafsi vifanye vizuri na kwa ufanisi mkubwa ni vema watu wa kusimamia idara za masoko wawe watu (hasa wanawake) wa jamii hizi maarufu kwa biashara.

Nimesema hasa wanawake wa jamii hizi kwa sababu wanawake wana uwezo mkubwa zaidi wa kushawishi wateja, hivyo basi kama watapatikana kutoka jamii hizi maarufu kwa biashara basi ufanisi katika uendeshaji wa mashirika haya utakuwa mkubwa sana.

Kama ambavyo sio kila mtu anaweza kufanya biashara kwa ufanisi mkubwa pia sio kila mtu anaweza kufanya vizuri kwenye vitengo hivi vya masoko vya mashirika mbalimbali.

Ili vitengo vya masoko vya masoko na biashara vya mashirika haya visitetereke vitazame vigezo vifuatavyo;
1. Wanaopewa kazi kwenye eneo la biashara na masoko lazima wawe ni wasomi wa kiwango cha hali ya juu katika masuala ya fedha.
2. Wafuatiliwe wanatokea jamii zipi? Simaanishi wengine hawafai lakini wasomi ambao wanatokea jamii hizi maarufu kwa biashara wana uwezo mkubwa zaidi wa kusimamia idara za masoko kuliko watu wasiotokea kwenye jamii hizi.

Chanzo kikuu cha kuyumba kwa mashirika haya ni kufeli kwa idara za masoko kujiendesha.
Ili kuwe na ufanisi mkubwa katika uendeshaji wa shirika la ndege ATCL ni vema watanzania wenye asili ya bara Asia mfano wahindi, waarabu wapewe kusimamia idara za masoko. Mbona Zimbabwe ilifanya vizuri kwenye kilimo cha mahindi wakati mashamba yanasimamiwa na wazungu, waliponyang'anywa na kupewa waafrika Zimbabwe imekuwa tegemezi Kwa chakula.

Ni vema kuwatumia Hawa watanzania wenye asili ya bara Asia au waafrika wanaotokea jamii maarufu kwa biashara kuendesha kitengo cha masoko cha shirika la ndege na bandari Pamoja na mashirika mengine.

Kwa sababu watu wanaotokea jamii hizi wanaweza kufanya biashara kwa mtaji mdogo na kuiinua biashara kuwa kubwa sana, ni vizuri zaidi wasomi wa masuala ya biashara wanaotokea jamii hizi wakapewa kipaumbele kupewa kazi.

Pia hata ukurugenzi, umeneja n.k ni busara wakapewa kipaumbele wao kuliko hawa wengine wanaofeli kuendesha mashirika mbalimbali hivi Sasa.

Kwa nini wapewe wao?
1. Hawa watu wana nidhamu kubwa ya matumizi ya fedha kwenye biashara zao . Maana yake biashara ni asili yao.
2. Wana uwezo mkubwa zaidi wa kubuni mbinu za kuweza kufanya vizuri kwenye masoko mfano, kutafuta wateja. Hawa hawaoni aibu kutafuta masoko.

Kuhusu uzalendo; ni muhimu kukawepo mifumo imara ya kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya serikali na mashirika yake. ( Mfano; kuanzisha mfumo wa malipo ya serikali wa control number kwenye ticket kwenye mashirika kama Tazara, TRC, ATCL, bandarini.

Kufungwa kwa mifumo ya ulinzi CCTV camera kila mahali sababu nchi hii uaminifu ni sifuri kuanzia maskini kabisa mpaka tajiri.

Kufanikiwa kwa makampuni binafsi kutaongeza wigo wa soko la ajira.
 
Upvote 2
vitengo vya masoko vya masoko na biashara vya mashirika haya visitetereke vitazame vigezo vifuatavyo;
1. Wanaopewa kazi kwenye eneo la biashara na masoko lazima wawe ni wasomi wa kiwango cha hali ya juu katika masuala ya fedha.
2. Wafuatiliwe wanatokea jamii zipi? Simaanishi wengine hawafai lakini wasomi ambao wanatokea jamii hizi maarufu kwa biashara wana uwezo mkubwa zaidi wa kusimamia idara za masoko kuliko watu wasiotokea kwenye jamii hizi.
Niliposoma kichwa cha habari nikataka kuja mbio kupinga. Lakini nashukuru nimesoma yaliyomo.
Kaka umebalansi vizuri, wawe kwanza wasomi halafu ndio asili zao ziwasapoti hapo sawa tu nnaona.

Huwa nnasema meritocracy itawale, tuwapatie watu wanaouweza zaidi kazi wachape kazi husika.
 
Back
Top Bottom