Vito vinaweza kukusaidia sana wakati wa vita au machafuko makali

Vito vinaweza kukusaidia sana wakati wa vita au machafuko makali

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Wakati wa vita au machafuko makali mara nyingi thamani ya pesa hupungua kwa kasi sana, au hata kupotea kabisa(mtu anagoma kukupa huduma hata kama una pesa.)

Anajua makaratasi hayo yanaweza kumfia. Lakini ukiwa na kitu kama dhahabu au silver mtu anakuwa na uhakika kuwa thamani yake haiwezi kufa overnight.

Na ikitokea unapanga kukimbia nchi, pesa yako ni ngumu kukusaidia. Nani atapokea pesa ambayo hajui kama kesho itakuwa na thamani? Na nchi unayokimbilia pesa yako haitakusaidia hata kidogo.

Unaweza kuwa na Tsh laki tano, ukafanikiwa kukimbilia labda Kenya, hiyo pesa huko Kenya haitakusaidia kitu sababu mkenya gani atakubali kuchukua pesa ambayo kesho hakuna uhakika kama itakuwa na thamani, au hana uhakika kama kuna mtu mwingine atakubali kuichukua.

Lakini ukiwa na vito, labda vya dhahabu, almasi, Tanzanite, silver nk, unaweza kuvitumia kama fedha huko ulikokimbilia au hata ndani ya nchi sababu thamani yake ipo hasa kimataifa. Kama ni dhahabu au silver hata mkenya ataipokea akijua haiwezi kumfia.

Cheni yako ya silver ya Tsh 50,000 inaweza kukupa msosi wa familia, kukusaidia usafiri na hata kuhonga watu ili kujiokoa.
 
Back
Top Bottom