Vitu ambavyo Mwanaume au Mwanamke mwenye akili timamu kamwe hawezi kufanya

Vitu ambavyo Mwanaume au Mwanamke mwenye akili timamu kamwe hawezi kufanya

Kwa kukusaidia kiafya ni bora ukaepuka matumizi ya ngano maana ndiyo chanzo cha magonjwa mengi mtambuka yasiyoambukiza yanayotukabili wengi wetu hivi sasa.

Hivyo badala ya kubugia ngano nyingi kisha ukaanza kulalamika uzito uliopotiliza, kiungulia, vidonda vya tumbo, sumu kuzidi mwilini n.k bora ujielekeze kula vifuatavyo;

1. Mayai ni mazuri kwa afya ya ubongo wako.

2. Maji ni mazuri kwa ajili ya afya ya figo zako.

3. Kabeji ni nzuri kwa afya ya Maini yako.

4. Matango ni mazuri kwa afya ya Ngozi yako.

5. Machungwa ni mazuri kwa afya ya utumbo mpana.

6. Karoti ni nzuri kwa afya ya Macho yako.

7. Tangawizi ni nzuri kwa afya ya mapafu yako.

8. Parachichi ni zuri kwa afya ya Moyo wako.

9. Nyama ni muhimu kwa maendeleo ya seli, enzymes na homoni mwilini.

10. Pilipili nyekundu ni nzuri kwa afya ya mapafu.

11. Maharage ya kijani ni mazuri kwa afya ya mifupa.

12. Mazoezi ni mazuri kwa afya ya mwili mzima.

13. Kusoma ni jambo zuri la kiafya kwa ubongo wako.
Aiseee 😝😝😝
 
Vitu ambavyo kamwe MWANAUME mwenye akili timamu hawezi kufanya.

2. Kutumia sukari.

UNAELEWA NINI KUHUSU SUKARI?
Mwalimu wangu wa baiologia alinifundisha kwamba kuna makundi kadhaa ya vyakula likiwemo Wanga au kitaalamu Carbohydrates!

Unavyokataa watu wasitumie sukari, unamaanisha wasitumie Wanga /carbohydrate je hilo linawezekana?

Ungesema Sukari ikizidi ina madhara ningekuelewa
 
Mlokole kama mlokole
Kwani walokole hapa wanahusika vipi?

Hizi ni kanuni za kiafya za kuishi maisha halisia na yenye furaha kamili, kwa kuepuka magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika.

Sidhani kama kuna yeyote anayependa kugeuzwa teja wa kumeza madawa ya kila namna maishani mwake ila kwa sababu za kiafya huwa hatuna budi kuzineemesha hospitali.
 
Ila basi tu. Kwa hiyo,mamkwe hakumbatiwi na mkwewe. Ila, babamkwe anaruhusiwa kumkumbatia mkamwana! Uko sahihi. Maana hapo mshua akikuonjea,usije kulialia
Kwanza kama siyo ukafir wa kizungu na tamaduni za kuiga-iga hiyo dhana ya kukumbatiana inatoka wapi!? Jiheshimuni, salimianeni kwa mikono na mketi kwa heshima, na wa kike apige magoti (kama ina-apply) ndiyo staha, hizi mbwembwe zingine hazifai ndiyo maana hata hizo ndoa zenyewe siku hizi hazina maana.
 

Asante, kwa reasoning nzuri ni kweli nimesema sukari ila sijajafafanua ni sukari ipi au kwa kiwango gani.

Kifupi madhara makubwa ya sukari mwilini yanatokana na sukari za viwandani ambazo tunatumia katika vyakula kuliko sukari inayotokana na vyakula.

Iwe ni kiasili kupitia vyakula au ki-artificial, sukari bado ina madhara makubwa ikizidi mwilini, na kwa kuwa ukiishi Tanzania na una kipato cha kawaida kuepuka wanga, chumvi na mafuta mengi yasiyofaa mwilini ni mtihani;

Unashauriwa walahu kula ugali wa mtama (ukiweza kula na unywe uji wake bila kumix na unga mwingine itafaa sana),

Pendelea zaidi kula vyakula chukuchuku, vyakuchemsha bila kutia mafuta, vyakuchoma kama vile viazi, mahindi,samaki n.k lakini siyo nyama,

Kula pia vyakula katika hali yake ya ubichi-ubichi au freshi kama vile matunda, mimea jamii ya mikunde kama vile nuts na mbogamboga, poultry, viungo vya chakula kama vile tunavyotumia katika chai, pilau na katika mapishi ya vyakula mbalimbali, kunywa maji safi na uji fermented au maziwa ya mtindi mara kwa mara kama vinywaji vyako,

Epuka kabisa chai, soda, energy drinks,juisi za viwandani au added sugar majumbani, epuka pombe, epuka vyakula vya GMO na jitahidi kula organic food, pia epuka kwa kiasi kikubwa vyakula vya kukaanga, visivyo na nyuzinyuzi, vyenye chumvi au sukari nyingi.

Mwisho kabisa jijengee utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara, kula kwa muda maalumu na acha ulafi, kula kiasi kinachotakiwa kwa kila mlo.
 
Tips

1. Unapotembelea hospitalini kupima afya endapo ukiambiwa una Amoeba au typhoid usiangaike mwangalie daktari machoni kwa ujasiri kisha mwambie Ahsante.

Tembelea pharmacy iliyopo jirani na wewe kanunue CIPRO-T. Umeze dozi yako ya siku 5. Achana na pombe pamoja na maziwa na bidhaa zake. Hakika utapona.

2. Ukienda hospitali kisha ukaambiwa una H.Pylori mwangalie daktari usoni kwa ujasiri kisha mwambie Ahsante.

Kisha shika kiguu na njia nenda gengeni nunua kabeji. Ukifika nyumbani tengeneza juisi ya kabeji. Achana na Ngano na Sukari kabisa. Anza pia kujinyima au fanya mfungo. Hakika utapona.

3. Ukipeleka mkeo labour kujifungua na ukaona anapitia wakati mgumu na muda unazidi kuyoyoma, utungu hauji au kuna ka mkwamo mahali. Usijali we toka zako nje elekea wanapouza matunda. Nunua Nanasi moja safi lililoiva vizuri, menya na ummegee kipande hale.

Halafu toka kakae nje bila wasiwasi ukisoma gazeti lako subiri dakika chache kabla ya kuanza kusakwa, "hivi baba wa huyu mtoto kaelekea wapi?"

NB: Hospitali ni biashara na wewe ndiye mteja. Chunga afya yako, hospitali hazipo kulinda afya yako bali kukufirisi.
 
Duh kwani wanaume wanene tuna tatizo gani mkuu?
"Huo UNENE wenyewe ndiyo tatizo lenu mkuu"[emoji23]

mwanaume kamwe upaswi kujiachia ukawa mnene labda itokee tu sababu za kibaiolojia kama vile kurithi vinasaba na kasoro za kihomoni zinazopelekea ongezeko la vichocheo mwili katika kusababisha unene.

Binadamu ni mnyama kiasili na kwa wanyama wote, dume huwa ni mlinzi, mwenye nguvu, mkakamavu, mwenye misuli imara na mwindaji sasa ikitokea dume likawa na sifa tofauti na hizo basi linakosa sifa ya kumvutia jike na haliwezi kuendeleza uzao sababu ya udhaifu.

Back on topic, unene unapelekea matatizo mengi ya kiafya ikiwemo shinikizo kubwa la damu, matatizo ya moyo, kushindwa kupumua vyema, uvuruga mpangilio wa homoni mwilini, kupata maambukizi kwa urahisi, hupelekea mpaka kubadili vinasaba vya mwili na mbaya zaidi ugumba au kushindwa kufanya tendo la ndoa.

Sasa kwa mantiki hii kwanini mwanamke anayejitambua atafute ku-date na mgonjwa wa baadaye, ambaye si tu kuwa wanaweza kutengana mapema maishani sababu ya changamoto za kiafya bali hata mbegu zake dhaifu zinaweza kupelekea mwanamke kuzaa watoto dhaifu na wenye vinasaba vya unene.

Dawa ya ugonjwa wa unene wa kujitakia ni kula tizi, narudia tena kama mwanaume chukia kitambi fanya mazoezi mpaka kieleweke. Fanya kazi ngumu za kiumeni. Tafuta hela kwa bidii ili uishi mahali pazuri na hule mlo kamili. Daima chunga uzito wako kama unahitaji kufaidi uanamme wako. Mambo ya kuhemea juu juu kwenye kifua cha mwanamke mwachie bata.
 
Mimi nadhan mtu aishi kulingana na maono yake,na asivunje sheria za nchi maana kunajambo mtu anafanya halina madhara Kwake WAla Kwa jamii, mfano: mtu kuzaa mtoto moja au wawili, mtu kuvaa pensi,mtu kumwita mpenzi wake swiry,maana lazima WATU tutofautiane na katika tofauti zetu ndo mungu anavutiwa na Sisi angeweza kutuumba kama roboti tukafanana kila kitu lakin hakutaka,mungu wetu siyo WA equality ni wa harmony,sasa wewe kama unataka vitu vyote unavyopenda na wengine wapende
 
Back
Top Bottom