Asante, kwa reasoning nzuri ni kweli nimesema sukari ila sijajafafanua ni sukari ipi au kwa kiwango gani.
Kifupi madhara makubwa ya sukari mwilini yanatokana na sukari za viwandani ambazo tunatumia katika vyakula kuliko sukari inayotokana na vyakula.
Iwe ni kiasili kupitia vyakula au ki-artificial, sukari bado ina madhara makubwa ikizidi mwilini, na kwa kuwa ukiishi Tanzania na una kipato cha kawaida kuepuka wanga, chumvi na mafuta mengi yasiyofaa mwilini ni mtihani;
Unashauriwa walahu kula ugali wa mtama (ukiweza kula na unywe uji wake bila kumix na unga mwingine itafaa sana),
Pendelea zaidi kula vyakula chukuchuku, vyakuchemsha bila kutia mafuta, vyakuchoma kama vile viazi, mahindi,samaki n.k lakini siyo nyama,
Kula pia vyakula katika hali yake ya ubichi-ubichi au freshi kama vile matunda, mimea jamii ya mikunde kama vile nuts na mbogamboga, poultry, viungo vya chakula kama vile tunavyotumia katika chai, pilau na katika mapishi ya vyakula mbalimbali, kunywa maji safi na uji fermented au maziwa ya mtindi mara kwa mara kama vinywaji vyako,
Epuka kabisa chai, soda, energy drinks,juisi za viwandani au added sugar majumbani, epuka pombe, epuka vyakula vya GMO na jitahidi kula organic food, pia epuka kwa kiasi kikubwa vyakula vya kukaanga, visivyo na nyuzinyuzi, vyenye chumvi au sukari nyingi.
Mwisho kabisa jijengee utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara, kula kwa muda maalumu na acha ulafi, kula kiasi kinachotakiwa kwa kila mlo.