Vitu gan umevipiga “BAN”

Shukran sana mkuu ila kama kuna hela au biashara nishtue mengine niko field kila siku napambana na maisha
Kama dili linaloniingizia hela nikipata nafanya ila mitandao kwa kweli nimewaachia vijana

Alibaba natumia kwa kununua bidhaa ila fb wanasema kuna biashara pia ila wengi wamelizwa
Socializing natoka sana na safari za wiki au wiki mbili nasafiri sana na hizo zinanitosha sana kwani naonana na watu live badala ya emoji za kucheka
 
Piga BAN Anasa ,Pombe,kitimoto,zinaa,Bangi,sigara,unga ,Ps,kuhonga, nk
Ushuhuda ninao mwenyewe,

Kuna kipindi nilipiga BAN anasa ulizoainisha hapo (Pombe,bangi,sigara ,wanawake na niliacha kujibizana au kutukana mtu aliyenikera, kwa kifupi nilikuwa cool kabisa,sikujihusisha na mijadala wala mabishano yoyote isiyo/yasiyo na tija.

Ndani ya muda mfupi nilijikuta nina amani moyoni,ni ile raha fulani isiyo na kifani, ngozi inanawiri(kunenepa),unakula vizuri,usingizi wa kutosha na kadhalika na unakuwa na nishati chanya (positive energy) na mambo mengi unakuwa unafanikisha kiurahisi.

Nikabaini; Anasa, lugha chafu mdomoni, na mabishano yasiyo ya msingi yanasababisha nishati hasi (negative energy) inayoitesa akili na kunyonya mwili.
 
Shukrani sana kwa ushuhuda mkuu
 
Vitu Nilivovipiga ban 2023

1.Marafiki wanafiki[emoji706]
2.Rafiki asiye na faida [emoji706]
3.Xxx.com[emoji706]
4.Instagram [emoji706]
5. Pombe aina ya Bia[emoji706]
Vitu nilivopiga ban toka mwaka 2016
1 marafiki wanafiki
2 facebook
3 instagram
4 tiktok
5 snapchart
6 twitter
7 madem
8 ahad zisizo na maana
9 kusengenya
10 kushobokea mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…