Iceberg9
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 24,893
- 47,768
Ushuhuda ninao mwenyewe,
Kuna kipindi nilipiga BAN anasa ulizoainisha hapo (Pombe,bangi,sigara ,wanawake na niliacha kujibizana au kutukana mtu aliyenikera, kwa kifupi nilikuwa cool kabisa,sikujihusisha na mijadala wala mabishano yoyote isiyo/yasiyo na tija.
Ndani ya muda mfupi nilijikuta nina amani moyoni,ni ile raha fulani isiyo na kifani, ngozi inanawiri(kunenepa),unakula vizuri,usingizi wa kutosha na kadhalika na unakuwa na nishati chanya (positive energy) na mambo mengi unakuwa unafanikisha kiurahisi.
Nikabaini; Anasa, lugha chafu mdomoni, na mabishano yasiyo ya msingi yanasababisha nishati hasi (negative energy) inayoitesa akili na kunyonya mwili.
Inaonekana mtu wa kutukana sana chalii angu [emoji23]