Vitu gani vidogo vidogo unavyovitumia umevimiliki kwa muda mrefu sana

Vitu gani vidogo vidogo unavyovitumia umevimiliki kwa muda mrefu sana

[emoji355]

Nilipewa zawadi na Padri wa parokia yetu, baada ya kuongoza mtihani wa dini kiwilaya.

Saa ilitoka [emoji1037], box nilifungua mwenyewe,
Saa nlienda nayo Shule Sec O level, shule nzima hakukua na saa kali km hii.

Wanafunzi wa advance, baadhi walikua wananishawishi niwauziee, baadae nkaona hii ntaibiwa, nkaamua kuirudisha home.
Ile saa nkaweka kwa box lake, na kufungia kwa begi, nilikua naivaa home nikiwa likizo, hata Advance sikuenda nayo.

Nimekuja kuifaidi nikiwa chuo, saa kaliii, ina miaka 13 had sasa.
 
Mkanda wa ngozi na wallet huwa zinadumu sana
Sasa ule mkanda wangu uliodumu haukuwa wa ngozi.
Umetengenezwa kwa materials flani kama ile mikono ya mabegi ya mkononi (duffle bags), ile material wakaijaza vizuri..
Ni miaka inakata tu, Ngoma haizeeki.
 
Aisee mimi katika vitu nimekaa navyo kwa miaka mingi na mpaka sasa bado ninavyo na vinaniwezesha katika service za mwili wangu ni taulo na sanduku la nguo ambalo nimelitumia mara nyingi kuhifadhi documenties.

Kwa kumbukumbu zangu naona kama nilinunuliwa taulo na sanduku nikiwa shule ya msingi huko miaka ya 2005 mpaka namaliza mpaka naenda sekondary mpaka chuo mpaka napata ajira mpaka sasa maishani bado tu navitumia na naona viko vizuri tu labda taulo ndo soon nitaligeuza dekio.
Nimeanza kukatumia ka Sara kangu tangu kana 17yrs mpaka sasa 26yrs na bado kapo vzr
 
Nilinunua mkanda wa kiunoni pale karume sokoni mwaka 2008.

Nauvaa mpaka leo japo sasa nimegain weight umeanza kuwa mdogo.

Ronaldo akistaafu tu mpira nami nitaustaafisha.
Mimi nilinunua mkanda wa ngozi mwaka January 2019 kwa Wamasai, hadi sasa bado upo imara naendelea kuutumia.

Nilinunua TECNO Y6 May 2016 nikaitumia hadi hadi December 2021(miaka 5 si haba)

Binafsi napenda kutumia kitu hadi kiishe kabisa au kipotee ndipo niachane nacho, pia sio muumini wa kuuza vitu bila sababu ya msingi ya kunifanya niuze
 
Back
Top Bottom