Vitu gani vinavyokufanya umchukie mtu haraka??

Vitu gani vinavyokufanya umchukie mtu haraka??

Hakuna anayejua machungu ya kudhulumiwa pesa kama mtu asiye dhulumu au kuiba cha MTU. Kwa miaka mingi sasa huu mstari mtu akiuvuka huwa sirudi nyuma...it's deadline
Mkuu tupo pamoja inauma sana kudhulumiwa pesa
 
kuniambia uongo, aisee sipendi kabisa hii tabia. nikishakugundua ipo hatari ya mimi kupunguza ukaribu na wewe. tabia nyingine ni dharau na kupenda kutawala mazungumzo, yaani unakuta mtu mnapopiga story yeye tu ndo anapenda aongee, hii ni aina fulani ya dharau pia. uzuri mimi sipendi unafiki, nikishagundua mtu una tabia hizi nakaa mbali na wewe au mara chache naweza nikakuchana ili uamue mwenyewe kujirekebisha kama utapenda.
Mkuu huyo wa kutawala mazungumzo tunaye ofisini yani yy akifika watu wote tunanyongea tunakuwa wapole akikuta mnapiga story zenu anakata anaanza zake na akiona haumjali anakutikisa kabisa mabega. Halafu mbaya zaid ananyesha.
 
Ukiwa mtu wa kuongea wewe tu na huwapi nafasi wenzako nao waongee lzm nikuchukie
Nalog off
 
Mara nyingi mtu anachukia pale anapoona mpinzani wake amemzidi kila kitu na hana uwezo wa kumfikia.
 
Back
Top Bottom