Vitu gani vizuri uliwafanyia wakwe lakini ukaachwa?

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,730
Reaction score
9,088
Mapenzi hayajawahi kumwacha binadamu salama.

Nilimkuta akiwa hana mbele wala nyuma, anakaa kwa wazazi, nikampangia na nyumba, baadaye nikamtafutia kazi, akaanza kunawiri na uzinzi na ufuska vikaja juu.

Nikamsema akajirekebisha. Wazazi wake wakikuwa wanakaa kwenye nyumba ya tope, nikawajengea nyumba ya kisasa, ilipo kamilika wakasema nataka kumtoa kafara mtoto wao ili nikuze biashara zangu, kumbe kuna msichana mwingine wamemtafutia mtoto wao.
 
Pole sana vipi wana Amani kweli?
 
Hivi anayehusika kwenye kuacha au kuachwa, ni wakwe au uliyetongozana nae?

Tuachane na ilo, siku zote hii I'd yako nilikuwa najua ni Ke, ila nilivyoanza kusoma haya maelezo yako, nikaanza kuhisi nilikuwa nakosea, wewe ni Me, ila ulivyohitimisha hapo mwishoni, ndo nikang'amua upya wewe ni Ke.

Anyway,kisicho ridhiki hakiliki. Muache aende.
 
Nimejifunza kitu kuwa hata ufanyeje kama mtu hakupendi hakupendi tu. Acha kubabaika na watu utakuja kunishukuru. .

Ukitoa toa tu usiangalie fadhila nyuma utakuwa na amanita sana. .
Huyu dada hata angemsaidia mama mkwe figo kama angekua anaumwa bado kijana wao kama alikua hampendi asingempenda tu... Nature ya mapenzi "ASIYEKUPENDA unakuta unamuhitaji sana wakati huo ila UNAYEMPENDA hata yeye kwanza hakuwazii kabisa hata ujitoeje kwake"

Karma is real, and sometimes is a real b!tch...
 
Haya ni madini tupu. πŸ‘πŸ‘
 
Mitoto ya siku hizi haina kauli tradition, msimamo na wala hawajielewi ndio maana wazazi wamekuwa na maamuzi makubwa sana juu ya mustakabali wa maisha ya vijana wao
 
Mitoto ya siku hizi haina kauli tradition, msimamo na wala hawajielewi ndio maana wazazi wamekuwa na maamuzi makubwa sana juu ya mustakabali wa maisha ya vijana wao
Malezi chini ya mzazi mmoja, ndio chimbuko la haya. Mara 100 kama baba au mama, mmoja wapo ameachiwa mtoto peke yake, basi ampeleke kwa Babu na Bibi kama wote wapo.

Vijana Bado tupo careless sana kwenye issue za msingi
 
Duh pole sana vipi kama ni kweli karma inawahusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…