Comrade Ally Maftah
Member
- Nov 6, 2016
- 77
- 271
Na Comrade Ally Maftah
KING OF ALL SOCIAL MEDIA
Katika hii dunia inayokwenda kasi na isiyohitaji kubembelezana, unatakiwa kupata hivi vitu vitatu kwa namna ambayo hutoutweza utu wako.
1. PESA/ MALI
Katika hii dunia hakuna mbadala wa pesa, ili uishi kwa furaha ni lazima uwe na pesa, hivyo basi jitahidi uwe unatafuta pesa kila wakati.
lakini ukishindwa kupata pesa usifanye majaribio ya kuumiza watu au kutweza utu wako, jishushe ujiulize na uanze tena upya.
2. MAHUSIANO/ MAPENZI NA NDOA
Ni muhimu binadamu kumpata mwenzio, na uwe unampenda ila na yeye awe anakupenda/ anakuheshimu/ anakuthamini, kama wewe ni mwanaume umempenda mwanamke hakikisha huyo mwanamke anakuheshimu, anakunyenyekea, anakuthamini kama hana hizo piga chini mapema, kabla hujaingia kwenye misongo ya mawazo.
Ikitokea humpati mtu wa kuendana na wewe kuwa mpole usilazimishe mtu akupende, utajikuta unafanya mambo ya hovyo na yatakugharimu.
3. MADARAKA/ CHEO/NAFASI/ HESHIMA KWENYE JAMII YAKO
Pambana upate nafasi ya kuheshimika kwenye jamii, uwe na uwanja wa kutoa mchango wako kwenye jamii yako, iwe kwenye vyama vya siasa, vyama vya kijamii, nyumba za ibada au kazini. usijiweke nyuma ikitokea kuna nafasi ya uongozi gombea usiogope.
Lakini unapokosa nafasi usilazimishe, utawaumiza wenzako, utaanza chuki na zitakuumiza wewe mwenyewe, kaa jipange kwa nafasi zijazo usinganganie pia endapo uongozi unaelekea kupotea.
ELIMU HII INAKUPA ARI YA KUPAMBANA NA KUPATA MAISHA LAKINI KUWA NA TAHADHARI, KUTAKA KWAKO KUSIJE KUWA KERO KWA WENGINE NA IKAKUUMIZA MWENYEWE.
NDIMI
Comrade Ally Maftah
KING OF ALL SOCIAL MEDIA
0785670227