Vitu nilivyoona ambavyo vinanipa utata nikivifikiria hadi leo

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,042
Reaction score
3,095
Nilivyokuwa shule ya msingi kulikuwa na tabia ya wasichana kuzimia, iliaminika wana majini, wengine walikua wanaoata hadi nguvu ya kusukuma watu wa kubwa na kuwaumiza, au kurusha madawati, au kukimbia hadi kwenye miti mikubwa ( mikuyu )

Nilichokishuhudia nachokumbuka hadi leo, kuna wasichana walikua wanazimia kwa pamoja hatakama wapo sehemu mbalimbali madarasa tofauti na hawaonani, moja akizimia utakuta na mwenzake pia kazimia na wakiamka wanaamka kwa pamoja
 
Darasa letu enzi zile, ilikuwa akiingia mwalimu wa hisabati au English basi,mabinti wawili watatu lazima wamwagike chini. Wasipo kuwepo walimu wa masomo hayo au hakuna viboko vya namba na "speak English only" basi,kuna kuwa shwari kabisa,hakuna mapepo(yana ahirishwa) mpaka keshooo
 
Dah sabra bonge alivotupigisha darasa zima

Kipande cha mtu kilipandisha ety na kuna mwengine kadogo hivi nako kikapandisha weweeee zikapigwa hapo kadogoo si kakaliwa juu bhana wanafunzi sote tunaogopa mpka wakaja walimu
Dah tulipigwa kora darasa zima
 
wanapataga nguvu anaweza kukulenga na dawati
 
Watoto wa siku hz hawapati ata Cha kusimulia nyumbn

Enzi zetu nakumbuka hayo mapepo yaliruka na watoto wa kike Hadi watoto wa walimu waliguswa

Ilifikia muda fulan wazazi walikuwa wanakuja wanakaa shulen kusubiri mtoto wake akishikwa ambebe akamfanyie tambiko nyumbani kwake
 
Nilivyokuwa shule ya msingi kulikuwa na tabia ya wasichana kuzimia, iliaminika wana majini, wengine walikua wanaoata hadi nguvu ya kusukuma watu wa kubwa na kuwaumiza, au kurusha madawati, au kukimbia hadi kwenye miti mikubwa ( mikuyu )

Nilichokishuhudia nachokumbuka hadi leo, kuna wasichana walikua wanazimia kwa pamoja hatakama wapo sehemu mbalimbali madarasa tofauti na hawaonani, moja akizimia utakuta na mwenzake pia kazimia na wakiamka wanaamka kwa pamoja
Aisee
 
Back
Top Bottom