Ni kwa uzoefu wangu wa kutumia magari kwa mizunguko ya mjini na safari chache nje ya mkoa, Gari nilizomiliki ni automatic, mafuta petrol, cc 1500 hadi 2500, magari ya kawaida tu, nothing fancy
Hakikisha unatumia oil sahihi na original za gari lako, kama engine inahitaji 10W40, tumia hiyo. Kama gearbox inahitaji Type T-IV, CVT au WS tumia hio. Ni vyema kununua oil kwenye ofisi rasmi za kampuni ya gari lako, mfano Toyota wana ofisi kwenye majiji yote na huuza oil na spea original. Kama haupo karibu ni bora uagize kupitia mtu wa kuaminika au uende kwa dealers wanaotambulika na kampuni. watu wengi wanaharibu engine na gearbox zao kwa kutumia oil feki. oil ya gearbox ni salama zaidi ikinunuliwa kwenye ofisi za kampuni au kwa dealer wa kuaminika, hata kama ni laki 2 na nusu inaweza kutumika hata miaka mitatu bila matatizo kuliko kununua oil feki ya elf 60. oil ya engine unaweza pia kupata mbadala kutoka kwa kampuni zinazotambulika kama Total, lakini ni lazima ununue sehemu inayoaminika. magari ambayo hayana ofisi au viwanda vya oil nchini, kama BMW, Mazda, Nissan na mengineyo, ni muhimu kutafuta njia za kuaminika za kupata oil original. Usidanganywe na bei, oil ya gharama kubwa sio lazima iwe original.
2. MAFUTA ni kilio kinachotesa watu wengi sana, zingatia haya :
3. Usiende garage kama huna muda wa kuisimamia gari yako, ni heri upande bajaji kama umetngwa, ukiwa free peleka gari yako huku ukiwa umeketi pembeni, mafundi wengi usipokuwepo ni ngumu kushughulika na gari yako, pia unawapa uwanja mkubwa wa kuiba vifaa vyako vizima au original wakuwekee feki au vibovu.
4. Kupunguza kero za matrafki hakikisha unatembea na leseni ya udereva, uwe umekata bima, umelipia stika ya nenda kwa usalama, nunua fire extinguisher na triangle.
5. Kuwa gentle kwenye streering kama hakuna ulazima usikate mpaka mwisho, unaweza kurudi nyuma kidogo na kukata upya, hii inasaidia sana steering rack, ni kitu huwa ina gharama kuibadili. Pia hakikisha unatumia mafuta sahihi ya usukani, usijaze tu yoyote, hakikisha yawe maalum ya steering,
6. Chonga funguo wa ziada mapema kama unao moja au umebakiza moja, itaku save sana, ukipoteza funguo ni gharama sana kutengeneza mpya bila sample.
7. Usilete ujuaji au kubahatisha kwenye matengenezo ya gari, Kama huna uhakika wa hatua unazotakiwa kuchukua, peleka gari kwenye gereji au wasiliana na fundi mwenye ujuzi. Epuka kutumia maelezo ya mtandaoni moja kwa moja kwenye gari bila uelewa sahihi, kwani kosa dogo tu linaweza kusababisha hitilafu kubwa na kuongeza gharama. Matengenezo ya gari yanahitaji utaalamu, si majaribio.
8. Usiweke maji kwenye radiator , kuna kimiminika maalum kinachofanya kazi vizuri zaidi kinaitwa coolant, unawza kutumia coolant zinazouzwa na trusted dealers wa kampuni ya gari yako, lakin pia kuna makampuni kama Total wanazitengeneza, nunua sehemu inayoaminika mfano vituo vyao vya mafuta.
9. Matumizi ya mafuta yanategemea sana mazingira ya uendeshaji. Katika miji mingi ya Tanzania, magari huendeshwa kwa mwendo mdogo, mara nyingi chini ya km 50/h, huku yakisimama na kuanza safari tena mara kwa mara kutokana na matuta, mashimo, foleni, watembea kwa miguu, bodaboda na bajaji. Hali hii huongeza matumizi ya mafuta na hivyo si jambo la kushangaza hata kwa gari lenye engine ndogo 1500cc kupata wastani wa kilomita 9 kwa lita. Kwa upande mwingine, viwango vya matumizi ya mafuta vinavyoonekana kwenye tovuti au vipeperushi vya watengenezaji mara nyingi zimepimwa kwenye barabara zenye ubora wa juu, mwendo wa wastani na msongamano mdogo wa magari, ambapo gari linaweza kufikia zaidi ya kilomita 13 kwa lita, ukitaka kuyajua hayo uliza hata madereva taxi, ukienda kwa mafundi wengi yeye mwenyewe unakuta hana gari atakupa vipimo vya google.
10. Tembea na mwendo unaoridhika nao kulingana na uhitaji wako, usiige watu wengine au kutaka kupata approval yao, wapo wanaokimbiza wanawahisha wagonjwa hospitalini, wengine breki zimefeli, wapo wanaoendesha rafu wamelewa, wapo waliochoka na maisha yao, n.k. usiige ige. gari ni chuma lina spea, mwili wako hauna spea, tumeshapoteza watu wengi sana barabarani kwa haya mambo, cool down, umenunua chombo cha usafiri sio mashindano

- a. hakikisha unanunua spark plugs original kwa ajili ya aina ya gari lako, kila gari ina spark plugs zake zimetofautiana joto, urefu, n.k. kama unatumia Toyota nenda ofisi zao au kwa dealers wao nunua plug inayohitajika, plug moja inaweza kuwa ni elf 60 ila zinapiga kazi kwa kilometa laki 1 (miaka zaidi ya 7 kwa mizunguko ya mjini), ni bora kuzidi kununua plugs za elf kumi au 15 unabadili kila baada ya miezi 6 au mwaka na huwa zinakula zaidi mafuta kuzidi original.
- b. Weka mazoea usiendeshe gari ukiwa na mafuta chini ya robo ya tenki. Pampu ya mafuta hufanya kazi vizuri zaidi inapokuwa imezama kwenye mafuta ya kutosha, mafuta hufanya kazi kama kilainishi na pia husaidia kupoza pampu ya mafuta hasa kwenye barabara zetu zenye mitikisiko, matuta na mashimo mengi, hivyo mafuta yakipungua sana yanaweza kusababisha pampu kuvuta hewa na kufanya kazi kwa shida zaidi.
- c. kama gari yako ni used na hujawahi kabisa kusafisha fuel filter ya kwenye pampu nakushauri kaisafishe. kuwa mwangalifu wasikubadilishie motor, inapendeza zaidi wasafishe hapo hapo ukiwepo, huwa ni zoezi la dakika chache tu la kutoa vitu viliyonasa kwenye chujio (filter). hii pia inaweza kuwa suluhisho la gari yako kujizima, kupata shida ya kuwaka, kukosa nguvu, n.k.
- d. Jaribu kujaza mafuta kampuni moja tu, usipende kuchanganya changanya. kama ni total iwe total, kama ni puma iwe puma, kama ni oryx iwe hivyo, n.k. pendelea kujaza kampuni kubwa na vituo vinavyoaminika, kama umechanganya sana nenda gereji hasa zile za kwenye vituo vya mafuta vikubwa waambie wachomoe tenki walimwage mafuta yote uanze upya, makadirio ya huduma hii ni elf 20 hadi 40 (pamoja na kusafisha filter ya pampu).