Frank Mazagazaga
Member
- Sep 11, 2018
- 44
- 58
VITU TISA
Kutotolesha mayai si kuweka mayai kwenye boksi lenye taa joto, kama ambavyo Wengi wanajaribu kufanya na kusubiri siku 21:
Tengeneza mfumo.
Ni vitu tisa.
Kwa sababu hapa, tunatengeneza mazingira yanayoleta uhai ndani ya mayai ya kuku, na uhai una tabaka,
na kila tabaka hutaka kushughulikiwa bila kubahatishwa.
KITU CHA KWANZA:
Temperature & Humidity Controller
Mfugaji;
hiki ndicho kioo cha uhai.
Yai halitaki joto unalohisi wewe kuwa linatosha,
Linataka joto lililopimwa.
Halitaki unyevunyevu wa kubahatisha.
Linataka ule unaodhibitiwa.
Na hizi temperature and humidity Controller Controller hufanya kazi ya Kuwasha heater (taa joto) pale joto linapopungua na kuzima heater (taa joto) pale joto linapofikia kiwango sahihi: kifaa hiki kina sesor ya kutambua kiasi cha joto na Unyevu ndani ya incubator bila kukosea.
KITU CHA PILI:
Humidifier
Uhai wa kiinitete ndani ya yai haupo kwenye joto pekee.
Hutegemea pia unyevunyevu sahihi.
Yai likikosa unyevunyevu kiinitete hupoteza maisha pole pole.
Humidifier- hiki ni kifaa kinachozalisha unyevu ndani ya incubator.
Asiyeijua, huweka mayai bila kizalisha unyevu au huweka maji kwenye bakuli matokeo yake unyevu unakua pungufu vifaranga wanafia kwenye mayai.
KITU CHA TATU:
Taa yaHeater /
Taa joto.
Heater sahihi hutoa joto linalotengeneza uhai taratibu, sio linalochoma.
Wengi huua vifaranga kabla havijazaliwa kwa joto hasa wanaoweka Taa joto/heater karibu na mayai wa haraka.
KITU CHA NNE:
Feni
Joto lisiposambazwa huchoma mayai,
Feni ni lazima ndani ya incubator.
Kuhakikisha kila yai linapata fursa sawa ya uhai.
Bila feni, upande mmoja huishi, mwingine hufa.
KITU CHA TANO:
Ugeuzaji wa Mayai
Yai lisilogeuzwa mwili wa kifaranga hugandia na kushikana na yai upande mmoja.
Ugeuzaji Manual Kwa mkono
Mara 3–4 kwa siku.
Usipunguze chini ya mara 2.
Ugeuzaji Automatic
Mfumo hufanya kazi bila kuchoka.
Uhai wa kiini tete katika yai haupendi kukaa upande mmoja.
KITU CHA SITA:
Uchaguzi wa Mayai
Si kila yai linafaa si ila yai lina uhai ndani yake:
Yai lisilotokana na kuku mwenye jogoo—ni ndoto tupu.
Yai lililokaa zaidi ya siku 7–10—limeanza kupoteza uhai
Yai dogo sana au kubwa si sawa
Yai lenye ufa linabeba mauti.
Wengi hawazingatii hapa,
halafu hulaumu incubator.
KITU CHA SABA:
Umeme
Umeme wa uhakika ni mafanikio kwa mchakato.
Mfumo unaoegemea umeme peke yake ni kubahatisha ni vyema kuwa na mbadala (solar)
KITU CHA NANE:
Sehemu ya Kulelea Vifaranga
Vifaranga.
Vinahitaji kuendelea kuishi.
Sehemu baridi, chafu, au yenye upepo huua polepole vifaranga.
Brooder sahihi ni tumbo la pili la uhai Kwa vifaranga.
KITU CHA TISA:
Chakula Bora cha Vifaranga
Usiwape mabaki ya chakula chako.
Chakula ni ujumbe.
Ukilisha hovyo, utakuzaa hovyo vifaranga.
Vifaranga hulipa kile ulichoweka ndani yao.
Hapa hakuna msamaha.
Ukikosa kitu kimoja kati ya hivi tisa,
usiilaumu.
Ukivikusanya vyote tisa,
Ni mafanikio.
Ufugaji sio kubahatisha
Ni kanuni ya uzalishaji.
kile unachoweka, ndicho unachopata na nyongeza.
Na mfugaji aliyejenga mfumo,
hanaga hasara.
Hasara humkuta yule aliyebahatisha.
Anyways…
ufugaji ni mtihani.