Vitu vinatukwamisha Taifa kusonga mbele, bali yakipungua mambo haya Tanzania ingekuwa tupo mbali mno

Rudi kusoma tena bandiko langu. tunahitaji kuwa na hobby, lakin with moderation.

Impact ya watu kutofanya kazi, unaiona kupitia huduma zitolewazo na serikali!

Muda unao tumika kujadili hobby ni mwingi sana kuliko uzalishaji! na hii inasababishwa na ignorance tuliyo nayo kutokana na kukosa elimu thabiti inayo mjenga mtu kutambua umuhimu wake katika sekta za uzalishaji vs maendeleo ya Nchi yake
 
Kuna genge la watu flani sasa ni wazee, hao wakifa nchi itaamka, sera mpya zinazoenda na wakati zitafikiwa , hao ndio kikwazo cha maendeleo ni miungu watu wenye mawazo mgando ya kutawala na si kuongoza!!

Nakuunga mkono nchi yetu ni kisiwa kwa kufundishana kiswahili shuleni lengo sote tubaki humu humu ili tuwapigie kura, siku zenyewe si nyingi ikizidi sana miaka 70 tunakufa ila wao wanadhani wataishi milele, nonsense kabisa.

Tukijifunza in English from vidudu hadi chuo ni hatari kwao sababu kila raia ataweza kujua mambo mengine mengi yaliyo katika English kutoka kila pande ya dunia na ataweza kuwasiliana na mtu yoyote duniani anaeongea English na kuna vijana wapiga kura watahama nchi. Hilo halitakiwi! Ujinga wa watu ni msaada kwa matumbo ya watu.

Kuhusu kushabikia mpira nadhani hujawaza sana, mpira ni ajira na biashara, tunahitaji kuukuza kina Mzize nao wafurahie kuishi.
 
Mimi nafikiri tatizo letu sio simba na yanga.

Nadhani shida yetu kubwa ni kushindwa kuwajibika kuanzia on a peraonal level, jamii n.k. Mtu akifeli lazima atafute wa kumuangushia lawama.

Tunaamini serikali ndiyo inatakiwa kufanya, nadhani labda ujamaa wetu ambao ni mzuri kwenye kujenga umoja wa kitaifa lakini kiuchumi hatukuupokea kwa usahihi.
 
Uchumi wetu mbovu ndo unaotukwamisha hayo mambo ya simba na yanga sijui lugha ya kiswahili wala sio tatizo, usiyasingizie. Tutafute viongozi walio na mipango thabiti naya muda mrefu kudeal na issues za uchumi, tutatoboa. Wazungu huko kwao wanashabikia mpaka mashindano ya mbio za mbwa lakini kwa sababu ya kuwa smart kichwani kwenye mambo ya uchumi maisha yanaenda vizuri tu.
 
KWa hiyo unaona hisani sio ? Kujengewa barabara ujinga ni mzigo
Ni kazi ya serikali na imefanya,wewe ulitakaje?..haya mnataka tuwafuate wapi mnakotaka kutupeleka!?..watu wenyewe hamna sera,kazi kudandia matukio tu
 
Kitu kinacho tukwamisha nchi hii isisonge kimaendeleo zaidi ya tulivyo sasa ni chama cha kijani na hichi kirusi kime athiri nyanja nyingi sana kwwny system ….. ila ukiwa na D ya somo la Dini huwezi nielewa
 
Ni kazi ya serikali na imefanya,wewe ulitakaje?..haya mnataka tuwafuate wapi mnakotaka kutupeleka!?..watu wenyewe hamna sera,kazi kudandia

Ni kazi ya serikali na imefanya,wewe ulitakaje?..haya mnataka tuwafuate wapi mnakotaka kutupeleka!?..watu wenyewe hamna sera,kazi kudandia matukio tu
Mimi sina chama ni mtu huru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…