Vitu vingine vinafikirisha sana

Vitu vingine vinafikirisha sana

Igombe fisherman

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Posts
2,178
Reaction score
3,865
Ulishawahi kukutana na dawa ya ugonjwa lakini ukashindwa hata kuamini imewezekana vipi?

Miezi kadhaa hapa nyuma niliamka tu mguu unaumwa kama vile umetenguka. Wakati huo sijakutana na hali yoyote yenye uwezo wa kusababisha majeraha. Muda ulivyokuwa ukizidi kwenda hali ikazidi kuwa mbaya kiasi kwamba hata kutembea tu ikawa shida. Nilitumia dawa nyingi za kuchua na zingine za maumivu lakini wapi. Mguu ukavimba mpaka watu wengine wakaanza kusema nimekanyaga mtego. Nilijikanda madawa na madawa na madawa kama siku 7 lakini hali ilikuwa ile haikubadilika. Sik moja jamaa akaja akaniambia kuwa nijikande na nyasi za mwalilo. Hizi nyasi huwekwa ndani na watu wa kagera kwa ajiri ya kukaa hasahasa kwenye vijiwe vya kahawa na pombe. Nikaamua niende kwenye kilabu cha pombe kuzuga na soda huku nikitumia hizo nyazi kujikanda. Maana alisema nihakikishe tu hizo nyasi zinakanyagwa na watu wengi na nijikande tu bila hata kuzichemsha. Yaani unazoa tu na kujikanda. Nilifanya hivyo pasipo hata imani yoyote kwa jioni ile kisha nikachechemea zangu kwenda kulala. Cha kushangaza kesho yake mguu ulikuwa umepunguza uvimbe kwa kiwango kikubwa sana naumepunguza sana maumivu. Kwakifupi ndani ya siku mbili tu nilikuwa naweza kuvaa viatu na kutembea kama sijawahi kuumwa mguu. Je wewe ulishawahi kuponeshwa na dawa ambayo hata hukuweza kuamini
 
UTII. Mimi najua kanuni moja flani ipo duniani na haina maelezo mengi inataka ufanye tu; nayo ni UTII. Hata kwenye Biblia yule mtu mwenye ukoma alipokwenda kwa Yesu wala Yesu hakumuwekea mikono, ili alimwambia tu kanawe kwenye Birika la Siloamu, alipofanya hivyo ukoma wake ulikwisha akawa safi. UTII.
 
Hebu tuwekee ka picha ka hayo majani
Labda hujanielewa. Hayo majani yanakuwa ndani tu kama kapeti. Yaani yanatumika kama mkeka ndo niliyoambiwa. Ukumbuke huku kagera yapo kila nyumba ya biashara
 
Back
Top Bottom