Vitu viwili vilivyo vitakatifu: Ardhi na uumbaji

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Kuna vitu kamwe havipaswi kuchezewa kunajisiwa wala kuharibiwa kwa namna yoyote ile.. Vitu hivyo ni ardhi na uumbaji

Unajua katika imani nyingi na mitazamo ya kiroho, ardhi na uumbaji huchukuliwa kuwa vitu vitakatifu kwa sababu ni kazi ya mikono ya Muumba.
Na hilo halijaja kwa bahati mbaya bali kuna mambo muhimu yanayofanya ardhi na uumbaji kuitwa vitu vitakatifu kulingana na maandiko na mafundisho ya kiroho:

1. Chanzo cha Uhai na Baraka
Ardhi kama Shahidi: Ardhi inatajwa kuwa na uwezo wa kusikia neno la Bwana (Yeremia 22:29) na hata kutoa ushahidi dhidi ya matendo ya mwanadamu kuanzia kuumbwa kukua hadi kufa

Ardhi huchukuliwa kama hazina ya Baraka, Mafanikio mengi ya mwanadamu, kuanzia chakula hadi makazi, yamefungwa kwenye ardhi. Hivyo basi ardhi Inachukuliwa kuwa chanzo cha baraka ambacho Mungu alikitoa kwa mwanadamu akitumie katika maisha yake hapa duniani

2.Ardhi kwenye uhusiano wa Kiroho na Binadamu..Uumbaji wa Binadamu ....Kulingana na imani ya Kikristo, mwanadamu aliumbwa kwa mavumbi ya ardhi, hivyo kuna uhusiano wa asili na wa kudumu kati ya mwili wa binadamu na ardhi. Yaani huwezi kuvitenganisha hivi viwili

Kumbukumbu za Kiroho: Inasemekana na shuhuda nyingi tu kuwa ardhi ina uwezo wa kutunza "kumbukumbu" za matendo yaliyofanyika juu yake, iwe ni baraka au laana (kama damu ya Habili ilivyolia kutoka ardhini). Ardhi inasikia na ardhi inaona

3. Utakatifu wa Uumbaji
Kazi ya Mungu:
Kila kitu kilichoumbwa—miti, wanyama, anga, na maji—kinaakisi utukufu wa Muumba. Katika kitabu cha Mwanzo, Mungu aliona kila alichokiumba kuwa ni "chema," jambo linalokipa uumbaji hadhi ya utakatifu.

Wajibu wa Utunzaji: Kwa kuwa ni vitu vitakatifu, mwanadamu amepewa dhamana ya kuvitunza na si kuviharibu. Uharibifu wa mazingira, mauaji, kumwaga damu isiyo na hatia vinatazamwa kama kukosea heshima kazi ya uumbaji ya Mungu.

4. Ukombozi wa Ardhi
Katika mafundisho ya kiroho, ardhi inaweza "kuchafuliwa" na dhambi au damu, na hivyo kuhitaji maombi ya toba na ukombozi ili iweze kutoa baraka zake tena.
Viongozi wengi wa kiroho, hufundisha kuhusu umuhimu wa kuitakasa ardhi unayoiishi au kuifanyia kazi.
Wengi hushauriwa kuitakasa ardhi kwa dua na maombi maalum kabla yq kuifanyia chochote kile kwakuwa hujui kabla yako hiyo ardhi ilifanyiwa nini
 
Vip kuhusu maandiko matakatifu
 
D645E5F1-4720-4703-AA92-F5297A3EE1F4.jpeg
 
Back
Top Bottom